LAZIMA NISEME
JF-Expert Member
- Apr 5, 2015
- 232
- 260
Serikali msipomdhibiti JOSEPH OLESHANGAY mapema basi mjue anakwenda kutengeneza kundi hatari la UASI kwa Jamii ya Wamasai hapa nchini.
Naomba niwatahadharishe Rais Dkt. SAMIA SULUHU HASSAN na Serikali yako kuwa makini sana na kijana niliyemtaja hapo juu.
Siku za hivi karibuni Wakili huyu ambae pia ni Mwanaharakati kwa kushirikiana na Wanaharakati wenzake pamoja na baadhi ya Asasi za Kiraia ambazo zimesajiliwa kufanya kazi katika eneo la Ngorongoro wamekuwa mstari wa mbele kupinga kuhamishwa kwa Jamii ya Wamasai kutoka katika eneo la Hifadhi ya Ngorongoro na kwenda katika Kijiji cha Msomera kwa madai kuwa wananyanyaswa na kuangamizwa.
Katika uchunguzi wangu hivi karibuni Bw. Joseph Oleshangay amekuwa akiwaandaa kisaikolojia baadhi ya watu kupitia akaunti yake ya mtandao wa Kijamii ya 'X' Kwamba wanataka kuwa na Taifa huru la Wamasai yaani MAASAI LAND ili wajitawale na kuwa na Serikali yao kama ilivyo Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kitu ambacho ni UASI wa moja kwa moja.
Na kibaya zaidi jambo hilo linapewa nguvu na Asasi 3 hapa nchini ikiwemo anayofanyia kazi LEGAL AND HUMAN RIGHTS CENTRE (LHRC), The Pastoralists Indigenous Non Governmental Organization's Forum (PINGO's Forum) na Pastoral Women's Council (PWC) wakishirikiana Susanna Nordlund (Mwanaharakati) Kwa pamoja wanawachochea Jamii ya Wamasai wadai ardhi ya Maasai ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Na katika kuhakikisha hili linafanikiwa, Tayari Bw. JOSEPH OLESHANGAY ameandaliwa siku ya tarehe 16/03/2024 aapishwe kuwa LAIGWANAN wa Jamii hiyo ili aweze kuwa na nguvu ya Kimila na kuweza kusikilizwa kwa Mataifa ya Ulaya ambayo yamekuwa mstari wa mbele kumpa nafasi ya kumsikiliza juu kwa madai ya kuwa jamii yake inanyanyaswa na Serikali ya Tanzania.
Na hivi sasa ninavyoandika makala hii tayari kuna wageni kutoka mataifa ya Ulaya na Marekani wapo njiani kuja kushuhudia kusimikwa kwa Bw. Joseph kuwa kiongozi wa kimila ili wakamilishe azma yao ya kutaka jamii hiyo kuanzisha Nchi yao kwa kwani wao pia wamekuwa sehemu ya kudhamini zoezi hilo kupitia Asasi nilizozitaja hapo juu.
Wito wangu kwa Serikali ya Dkt. SSH na Wasaidizi wake, wasipolidhibiti mapema jambo hili bila kutarajia Bw. Joseph Ole Shangay anakwenda kutengeneza Waasi ndani ya jamii ya Wamasai na kundi hilo linaweza kuwa hatarishi kuliko makundi mengine ya uasi katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati.
Nitoe wito kwa Mamlaka husika kuhoji uhalali wa shughuli zinazofanywa na Asasi ya PINGOS, PWC, THRDC, na LHRC ndani ya Hifadhi ya Ngorongoro na tena baada ya kuona Wamasai hao wanaohama kwa hiyari kwenda Msomera hizo Asasi zimejiongeza kwenda kusajili ili kufanya shughuli zao katika eneo la Msomera hii yote ni kuendelea kuwa karibu na Jamii hiyo ili waweze kuwashawishi wadai kuwa na ARDHI YA MAASAI ndani ya nchi ya Tanzania.
Mungu Ibariki Tanzania!