Kwanini Job Ndugai amejiuzulu Uspika?

Ngamanya Kitangalala

JF-Expert Member
Sep 24, 2012
501
1,214
KWA NINI MHESHIMIWA NDUGAI AMEJIUZURU

Katika siku za karibuni nchi yetu imepatwa na moja ya tukio kubwa kabisa katika medani za uongozi wa kisiasa, tukio hilo ni ile hatua ya aliyekuwa Spika wa Bunge la 12 la jamhuri ya muungano wa Tanzania mheshimiwa Job Yustino Ndugai kujiuzuru nafasi yake hiyo ya uspika wa Bunge

Ni tukio kubwa kabisa katika historia ya siasa zetu hapa nchini, tangu nchi yetu kupata uhuru wake mwaka 1961

Baada ya tukio hilo, kumekuwepo na mjadala mkubwa sana miongoni mwetu sisi wananchi, mijadala ambayo kimsingi inatokana na mazingira yaliopelekea mheshimiwa Ndugai kujiuzuru wadhifa wake huo.

Wananchi wengi, wanajiuliza inakuwaje kiongozi mkuu wa mhimili akajiuzuru katika mazingira ya namna hiyo?

Kwa siku za karibuni kumekuwepo na sitofahamu kati ya mheshimiwa Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania mama Samia Suluhu Hassan na mheshimiwa Job Ndugai aliyekuwa Spika wa Bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania, sitofahamu hiyo ilitokana na hatua ya mheshimiwa Job Ndugai kutoa maneno hadharani yenye kuonyesha msimamo tofauti na serikali, juu ya mikopo ya nje kwa nchi yetu

Ukisoma katiba yetu ya jamhuri ya muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, kwenye ibara ya 63 (2) , inataja Bunge kuwa ndio chombo kikuu cha jamhuri ya muungano kitakachokuwa na madaraka kwa niaba ya wananchi katika KUISIMAMIA na KUISHAURI serikali na vyombo vyake vyote katika utekelezaji wa majukumu yake

Kwa msingi huo, sio jambo la ajabu kabisa kwa Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania kutofautiana kimawazo na mtizamo juu ya uendeshaji wa serikali na Spika wa Bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania

Swali ambalo wananchi wengi tumekuwa tukijiuliza, je ni kwanini kutofautiana huko kimawazo hadharani baina ya viongozi wetu hawa wakuu, imekuwa ni jambo lisilokubalika kabisa hasa ndani ya chama cha mapinduzi?

Turudi kwenye katiba yetu ya jamhuri ya muungano wa Tanzania ya mwaka1977, ukiisoma vizuri katiba yetu hii, utagundua kuna kinaitwa UKUU WA CHAMA( party Supremacy), japo hakijaandikwa moja kwa moja ndani ya katiba, lakini kuna hiyo dhana

Kwanini?

Kwa mfano, kwa upande wa Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania, kwa mujibu wa ibara ya 39, ibara ndogo 1(c) ya katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, inasema sifa mojawapo ya mtu kuchaguliwa kuwa Rais ni lazima awe mwanachama na mgombea aliyependekezwa na chama cha siasa nchini

Maana yake ni nini?

Huwezi kugombea nafasi ya Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania mpaka kwanza uwe mwanachama wa chama cha siasa kilichosajiliwa kwa mujibu wa sheria chini ya ofisi ya msajili wa vyama vya siasa nchini

Kifungu hicho cha katiba, kinaweza kumfanya Rais wa jamhuri ya muungano kuwa anawajibika zaidi kwa chama chake kilichompendeza kwa nafasi hiyo, kuliko hata wananchi waliomchagua kushika nafasi hiyo

Kwa mfano, ukisoma katiba yetu hii, kwenye ibara ya 33(2) inamtambua Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania kama

1. Mkuu wa serikali( Head of the government)

2. Mkuu wa nchi( Head of state)

3. Amiri jeshi mkuu( Commander in chief)

Hivyo Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania, kwa nafasi yake kama mkuu wa serikali na ukirejea ibara ya 39 ibara ndogo ya 1(c) ya katiba ya jamhuri wa muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, inayomtaka Rais kuwa kwanza mwanachama wa chama cha siasa , hiyo inaweza kupelekea chama cha siasa kilichomdhamini Rais kuwa na NGUVU ZAIDI kuliko hata serikali inayoongozwa na Rais huyo

Hapo sasa ndio dhana ya UKUU WA CHAMA( Party Supremacy) inapoonekana

Hiyo ndio sababu binafsi naamini chama cha mapinduzi katika utamaduni wao hawataki kutenganisha kofia hizo mbili za Mwenyekiti wa CCM taifa na Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania

Kwa upande wa Spika wa Bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania, ametajwa kwenye ibara ya 84(1) ya katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania, ambapo inamtaja Spika kama kiongozi wa Bunge

Kwenye ibara hiyo ya 84(1) inatambua Spika wa Bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania, anaweza kuchaguliwa kutoka miongoni mwa watu ambao ni wabunge au watu wenye sifa za kuwa wabunge

Maana yake ni nini?

Ni kwamba kwa katiba yetu hii ya jamhuri ya muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, mtu yeyote hata ambaye sio mbunge anaweza kuchaguliwa kuwa Spika wa Bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania, isipokuwa ni lazima kwanza awe na sifa za yeye kuchaguliwa kuwa mbunge

Sasa ukisoma katiba yetu kwenye ibara ya 67 ibara ndogo 1(b) inataja sifa mojawapo ya mtu kuchaguliwa kuwa mbunge ni lazima kwanza awe ni mwanachama wa chama cha siasa na mgombea aliyependezwa na chama hicho

Katika Bunge letu hili la 12, kwa sasa kuna jumla ya wabunge takribani 392 kati ya hao ni wabunge 11 tu ambao wanaweza kuingia bungeni bila hata ya kuwa wanachama wa chama cha siasa, wabunge hao ni mwanasheria mkuu wa serikali( Attorney General)ambaye kwa mujibu wa ibara 66 ibara ndogo 1(d) ya katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, anatajwa kama mbunge na wabunge 10 wa kuteuliwa na Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania ambao wametajwa katiba ibara ya 66 ibara ndogo ya 1(e)

Maana yake nini?

Katika Bunge hili la 12, takribani ya wabunge 98% ni wabunge ambao LAZIMA KWANZA wawe wanachama wa chama cha siasa na watokane na vyama vya siasa kwa mujibu wa katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania ya mwaka1977

Maana yake, chama chochote cha siasa ambacho kitakuwa na idadi kubwa zaidi ya wabunge ndani ya Bunge, KINAWEZA KUWA NA NGUVU ya kulidhibiti Bunge pamoja na wabunge wake

Hapo sasa ndipo inakuja tena dhana ya UKUU WA CHAMA( Party Supremacy)

Japokuwa katiba yetu, inatoa fursa kwa mtu ambaye sio mbunge kugombea nafasi ya Spika wa Bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania, lakini kwa mujibu wa kanuni za kudumu za bunge toleo la mwaka 2020 kwenye kifungu cha 9 kifungu kidogo cha 2 na 3 ili mtu uweze kugombea nafasi ya Spika wa Bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania, ni lazima jina lake lipendekezwe na chama cha siasa kilichosajiliwa wa mujibu wa sheria ya vyama vya siasa nchni

Maana yake nini?.

Mtu yeyote huwezi kugombea nafasi ya Spika wa Bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania bila kwanza kuwa mwanachama wa chama cha siasa nchini

Hiyo sasa inatoa fursa kwa chama cha siasa kilichotoa Spika kuweza kuwa na nguvu ya kumdhibiti Spika, kuweza kuwa na nguvu ya kuhakikisha Spika na Bunge lake wanaendana na sera , mtazamo na malengo cha chama hicho

Hapo tena inaonyesha dhana ya UKUU WA CHAMA ( party Supremacy)

Ukija sasa kwa upande wa chama cha mapinduzi, ambacho mheshimiwa Job Ndugai ni mwanachama wake

Ukisoma katiba ya chama cha mapinduzi ya mwaka 1977 toleo la mwaka 2017 kwenye ibara ya 103 ibara ndogo ya 1(p), Spika wa Bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania anayetokana na chama cha mapinduzi ni mjumbe wa kamati kuu ya halmashauri kuu ya CCM taifa( Central Commitee)

Ukisoma katiba ya chama cha mapinduzi ya mwaka 1977 toleo la 2017 kwenye ibara ya 104(1) kazi mojawapo ya kamati kuu ya halmashauri kuu ya CCM taifa ni kutoa uongozi wa siasa nchini

Maana yake sera zote za uendeshaji wa serikali iliyo chini ya chama cha mapinduzi uanzia kwanza kanati kuu ya halmashauri kuu ys CCM taifa, na baadae kwenda kikao cha juu zaidi cha halmashauri kuu ya CCM taifa ( National Executive Committee) ambapo kwa mujibu wa katiba ya chama cha mapinduzi ya mwaka 1977, toleo la mwaka 2017 kwenye ibara ya 101 ibara ndogo ya 1(p) Spika wa Bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania anayetokana na CCM naye ni mjumbe wa kikao hicho

Hivyo basi, kwa mheshimiwa Job Ndugai kwa nafasi zake alizokuwa nazo ndani ya chama cha mapinduzi kama mjumbe wa vikao vya juu vya chama cha mapinduzi, hiyo ilikuwa INAMYIMA FURSA YA YEYE KUTOA MAWAZO YAKE HADHARANI yanayotoa mwelekeo wa kupingana na sera za chama chake hata kama mawazo hayo yalikuwa sahihi, kwa sababu yeye anayo sehemu ya kuwasilisha mawazo yake hayo

Kwa maana hiyo, kwa kauli ile ya mheshimiwa Job Ndugai anakuwa anakosa kitu kinaitwa uwajibikaji wa pamoja ( Collective responsibility) na vikao vya juu vya chama chake kwa maana ya kamati kuu ya halmashauri kuu ya CCM taifa na halmashauri kuu ya CCM taifa

Hivyo kulikuwa hakuna njia nyingine yeyote kwa mheshimiwa Job Ndugai zaidi ya yeye kujiuzuru kuwa mjumbe wa vikao hivyo vya juu vya CCM, na njia pekee ambayo angeweza kujiuzuru kuwa mjumbe wa vikao hivyo ni kwa yeye kujiuzuru nafasi yake ya Spika wa Bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania kwa sababu kwa mujibu wa katiba ya chama cha mapinduzi ya mwaka 1977 toleo la mwaka 2017, Spika wa Bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania anayetokana na chama hicho ni mjumbe wa vikao hivyo vya juu vya chama cha mapinduzi

Swali la kujiuliza watanzania

Je kwa mifumo hii ya utawala tuliyonayo sasa, inatoa fursa kwa Spika wa Bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania anayetokana na chama X kuongoza Bunge litakalokuwa na uwezo wa kuisimamia serikali ipasavyo iliyoundwa na chama X ?

Ngamanya Kitangalala
0756 669494
Kngamanya@yahoo.com
 
KWA NINI MHESHIMIWA NDUGAI AMEJIUZURU

Katika siku za karibuni nchi yetu imepatwa na moja ya tukio kubwa kabisa katika medani za uongozi wa kisiasa, tukio hilo ni ile hatua ya aliyekuwa Spika wa Bunge la 12 la jamhuri ya muungano wa Tanzania mheshimiwa Job Yustino Ndugai kujiuzuru nafasi yake hiyo ya uspika wa Bunge

Ni tukio kubwa kabisa katika historia ya siasa zetu hapa nchini, tangu nchi yetu kupata uhuru wake mwaka 1961

Baada ya tukio hilo, kumekuwepo na mjadala mkubwa sana miongoni mwetu sisi wananchi, mijadala ambayo kimsingi inatokana na mazingira yaliopelekea mheshimiwa Ndugai kujiuzuru wadhifa wake huo

Bado mjadala unaendelea!??
 
Yaani mtaandika yote lakini ukweli ni kwamba, ccm imechosha watu katika nchi hii ni hakuna mfano kiasi kwamba hakuna maana ya kuwa na mfumo wa vyama vingi, ni utapeli mtupu.
 
Kwani Barua yake haikutoa sababu (Kwa maslahi marefu ya Chama / Taifa n.k.)

Anyway andiko lako refu sana hapa umekuja na swali au una majibu unatupa ? Tunajua kwamba ameshinikizwa kujiuzulu kwanini ndio nilitegemea labda jibu unalo
 
Hakuna la maana uliloandika hapo, kwamba wewe ndio binadamu mwenye uelewa sana wakati jambo lipo wazi kabisa mkuu. Ni vyema huu uzi uufute unatia aibu tu. Job hana kosa lolote kikatiba labda wangetumia mbinu nyingine. Hii mbinu iliyotumika ipowazi sana na kila mtanzania ameilewa vya kutosha.
 
Hapo hata mimi nitachukua Jukumu kama mlipa Kodi la kwenda Kumpiga Bakora na Makofi kwa kupoteza muda na raslimali za taifa..., In short itakuwa ni upuuzi
Atajitetea tena kuwa barua hakuandika yeye ni mitandao imevumisha.
 
Ili kutimiza matakwa ya katiba ya jmt, kwamba bunge ni chombo cha kuisimamia na kuishauri serikali, basi speaker wa bunge yafaa asiwe wa chama tawala. Liangalieni kwa makini pendekezo hili.
 
Unauliza makofi polisi???ule mhimili uliojichimbia zaid ndyo kila kitu
KWA NINI MHESHIMIWA NDUGAI AMEJIUZURU

Katika siku za karibuni nchi yetu imepatwa na moja ya tukio kubwa kabisa katika medani za uongozi wa kisiasa, tukio hilo ni ile hatua ya aliyekuwa Spika wa Bunge la 12 la jamhuri ya muungano wa Tanzania mheshimiwa Job Yustino Ndugai kujiuzuru nafasi yake hiyo ya uspika wa Bunge

Ni tukio kubwa kabisa katika historia ya siasa zetu hapa nchini, tangu nchi yetu kupata uhuru wake mwaka 1961

Baada ya tukio hilo, kumekuwepo na mjadala mkubwa sana miongoni mwetu sisi wananchi, mijadala ambayo kimsingi inatokana na mazingira yaliopelekea mheshimiwa Ndugai kujiuzuru wadhifa wake huo

Wananchi wengi, wanajiuliza inakuwaje kiongozi mkuu wa mhimili akajiuzuru katika mazingira ya namna hiyo?

Kwa siku za karibuni kumekuwepo na sitofahamu kati ya mheshimiwa Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania mama Samia Suluhu Hassan na mheshimiwa Job Ndugai aliyekuwa Spika wa Bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania, sitofahamu hiyo ilitokana na hatua ya mheshimiwa Job Ndugai kutoa maneno hadharani yenye kuonyesha msimamo tofauti na serikali, juu ya mikopo ya nje kwa nchi yetu

Ukisoma katiba yetu ya jamhuri ya muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, kwenye ibara ya 63 (2) , inataja Bunge kuwa ndio chombo kikuu cha jamhuri ya muungano kitakachokuwa na madaraka kwa niaba ya wananchi katika KUISIMAMIA na KUISHAURI serikali na vyombo vyake vyote katika utekelezaji wa majukumu yake

Kwa msingi huo, sio jambo la ajabu kabisa kwa Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania kutofautiana kimawazo na mtizamo juu ya uendeshaji wa serikali na Spika wa Bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania

Swali ambalo wananchi wengi tumekuwa tukijiuliza, je ni kwanini kutofautiana huko kimawazo hadharani baina ya viongozi wetu hawa wakuu, imekuwa ni jambo lisilokubalika kabisa hasa ndani ya chama cha mapinduzi?

Turudi kwenye katiba yetu ya jamhuri ya muungano wa Tanzania ya mwaka1977, ukiisoma vizuri katiba yetu hii, utagundua kuna kinaitwa UKUU WA CHAMA( party Supremacy), japo hakijaandikwa moja kwa moja ndani ya katiba, lakini kuna hiyo dhana

Kwanini?

Kwa mfano, kwa upande wa Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania, kwa mujibu wa ibara ya 39, ibara ndogo 1(c) ya katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, inasema sifa mojawapo ya mtu kuchaguliwa kuwa Rais ni lazima awe mwanachama na mgombea aliyependekezwa na chama cha siasa nchini

Maana yake ni nini?

Huwezi kugombea nafasi ya Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania mpaka kwanza uwe mwanachama wa chama cha siasa kilichosajiliwa kwa mujibu wa sheria chini ya ofisi ya msajili wa vyama vya siasa nchini

Kifungu hicho cha katiba, kinaweza kumfanya Rais wa jamhuri ya muungano kuwa anawajibika zaidi kwa chama chake kilichompendeza kwa nafasi hiyo, kuliko hata wananchi waliomchagua kushika nafasi hiyo

Kwa mfano, ukisoma katiba yetu hii, kwenye ibara ya 33(2) inamtambua Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania kama

1. Mkuu wa serikali( Head of the government)

2. Mkuu wa nchi( Head of state)

3. Amiri jeshi mkuu( Commander in chief)

Hivyo Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania, kwa nafasi yake kama mkuu wa serikali na ukirejea ibara ya 39 ibara ndogo ya 1(c) ya katiba ya jamhuri wa muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, inayomtaka Rais kuwa kwanza mwanachama wa chama cha siasa , hiyo inaweza kupelekea chama cha siasa kilichomdhamini Rais kuwa na NGUVU ZAIDI kuliko hata serikali inayoongozwa na Rais huyo

Hapo sasa ndio dhana ya UKUU WA CHAMA( Party Supremacy) inapoonekana

Hiyo ndio sababu binafsi naamini chama cha mapinduzi katika utamaduni wao hawataki kutenganisha kofia hizo mbili za Mwenyekiti wa CCM taifa na Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania

Kwa upande wa Spika wa Bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania, ametajwa kwenye ibara ya 84(1) ya katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania, ambapo inamtaja Spika kama kiongozi wa Bunge

Kwenye ibara hiyo ya 84(1) inatambua Spika wa Bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania, anaweza kuchaguliwa kutoka miongoni mwa watu ambao ni wabunge au watu wenye sifa za kuwa wabunge

Maana yake ni nini?

Ni kwamba kwa katiba yetu hii ya jamhuri ya muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, mtu yeyote hata ambaye sio mbunge anaweza kuchaguliwa kuwa Spika wa Bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania, isipokuwa ni lazima kwanza awe na sifa za yeye kuchaguliwa kuwa mbunge

Sasa ukisoma katiba yetu kwenye ibara ya 67 ibara ndogo 1(b) inataja sifa mojawapo ya mtu kuchaguliwa kuwa mbunge ni lazima kwanza awe ni mwanachama wa chama cha siasa na mgombea aliyependezwa na chama hicho

Katika Bunge letu hili la 12, kwa sasa kuna jumla ya wabunge takribani 392 kati ya hao ni wabunge 11 tu ambao wanaweza kuingia bungeni bila hata ya kuwa wanachama wa chama cha siasa, wabunge hao ni mwanasheria mkuu wa serikali( Attorney General)ambaye kwa mujibu wa ibara 66 ibara ndogo 1(d) ya katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, anatajwa kama mbunge na wabunge 10 wa kuteuliwa na Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania ambao wametajwa katiba ibara ya 66 ibara ndogo ya 1(e)

Maana yake nini?

Katika Bunge hili la 12, takribani ya wabunge 98% ni wabunge ambao LAZIMA KWANZA wawe wanachama wa chama cha siasa na watokane na vyama vya siasa kwa mujibu wa katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania ya mwaka1977

Maana yake, chama chochote cha siasa ambacho kitakuwa na idadi kubwa zaidi ya wabunge ndani ya Bunge, KINAWEZA KUWA NA NGUVU ya kulidhibiti Bunge pamoja na wabunge wake

Hapo sasa ndipo inakuja tena dhana ya UKUU WA CHAMA( Party Supremacy)

Japokuwa katiba yetu, inatoa fursa kwa mtu ambaye sio mbunge kugombea nafasi ya Spika wa Bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania, lakini kwa mujibu wa kanuni za kudumu za bunge toleo la mwaka 2020 kwenye kifungu cha 9 kifungu kidogo cha 2 na 3 ili mtu uweze kugombea nafasi ya Spika wa Bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania, ni lazima jina lake lipendekezwe na chama cha siasa kilichosajiliwa wa mujibu wa sheria ya vyama vya siasa nchni

Maana yake nini?.

Mtu yeyote huwezi kugombea nafasi ya Spika wa Bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania bila kwanza kuwa mwanachama wa chama cha siasa nchini

Hiyo sasa inatoa fursa kwa chama cha siasa kilichotoa Spika kuweza kuwa na nguvu ya kumdhibiti Spika, kuweza kuwa na nguvu ya kuhakikisha Spika na Bunge lake wanaendana na sera , mtazamo na malengo cha chama hicho

Hapo tena inaonyesha dhana ya UKUU WA CHAMA ( party Supremacy)

Ukija sasa kwa upande wa chama cha mapinduzi, ambacho mheshimiwa Job Ndugai ni mwanachama wake

Ukisoma katiba ya chama cha mapinduzi ya mwaka 1977 toleo la mwaka 2017 kwenye ibara ya 103 ibara ndogo ya 1(p), Spika wa Bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania anayetokana na chama cha mapinduzi ni mjumbe wa kamati kuu ya halmashauri kuu ya CCM taifa( Central Commitee)

Ukisoma katiba ya chama cha mapinduzi ya mwaka 1977 toleo la 2017 kwenye ibara ya 104(1) kazi mojawapo ya kamati kuu ya halmashauri kuu ya CCM taifa ni kutoa uongozi wa siasa nchini

Maana yake sera zote za uendeshaji wa serikali iliyo chini ya chama cha mapinduzi uanzia kwanza kanati kuu ya halmashauri kuu ys CCM taifa, na baadae kwenda kikao cha juu zaidi cha halmashauri kuu ya CCM taifa ( National Executive Committee) ambapo kwa mujibu wa katiba ya chama cha mapinduzi ya mwaka 1977, toleo la mwaka 2017 kwenye ibara ya 101 ibara ndogo ya 1(p) Spika wa Bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania anayetokana na CCM naye ni mjumbe wa kikao hicho

Hivyo basi, kwa mheshimiwa Job Ndugai kwa nafasi zake alizokuwa nazo ndani ya chama cha mapinduzi kama mjumbe wa vikao vya juu vya chama cha mapinduzi, hiyo ilikuwa INAMYIMA FURSA YA YEYE KUTOA MAWAZO YAKE HADHARANI yanayotoa mwelekeo wa kupingana na sera za chama chake hata kama mawazo hayo yalikuwa sahihi, kwa sababu yeye anayo sehemu ya kuwasilisha mawazo yake hayo

Kwa maana hiyo, kwa kauli ile ya mheshimiwa Job Ndugai anakuwa anakosa kitu kinaitwa uwajibikaji wa pamoja ( Collective responsibility) na vikao vya juu vya chama chake kwa maana ya kamati kuu ya halmashauri kuu ya CCM taifa na halmashauri kuu ya CCM taifa

Hivyo kulikuwa hakuna njia nyingine yeyote kwa mheshimiwa Job Ndugai zaidi ya yeye kujiuzuru kuwa mjumbe wa vikao hivyo vya juu vya CCM, na njia pekee ambayo angeweza kujiuzuru kuwa mjumbe wa vikao hivyo ni kwa yeye kujiuzuru nafasi yake ya Spika wa Bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania kwa sababu kwa mujibu wa katiba ya chama cha mapinduzi ya mwaka 1977 toleo la mwaka 2017, Spika wa Bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania anayetokana na chama hicho ni mjumbe wa vikao hivyo vya juu vya chama cha mapinduzi

Swali la kujiuliza watanzania

Je kwa mifumo hii ya utawala tuliyonayo sasa, inatoa fursa kwa Spika wa Bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania anayetokana na chama X kuongoza Bunge litakalokuwa na uwezo wa kuisimamia serikali ipasavyo iliyoundwa na chama X ?

Ngamanya Kitangalala
0756 669494
Kngamanya@yahoo.com
 
Lakini katika nchi nyingi zenye mfumo wa urais, spika hutokana na chama chenye wabunge wengi; Angalia hata Marekani.
Tatizo letu ni kuwa tuna wabunge maslahi tu - basi, tena maslahi ya kifedha. Kwenye nchi ambazo watu wanaomba kuwa wabunge ili kupata hadhi - hawafuati mshahara, utendaji unakuwa tofauti kabisa.
Halafu nimesikia kwenye kiapo chao eti "sitatumia cheo changu kwa maslahi binafsi" Inashangaza sana. Naomba mwenye kiapo hicho atuwekee hapa ili kiwe rejea.
 
Mfumo ule ule aliotumia kuhenyesha wenzake huenda ndiyo mfumo huo huo uliotumika kwake, no surprises, karma never misses it's destination!
 
Lakini katika nchi nyingi zenye mfumo wa urais, spika hutokana na chama chenye wabunge wengi; Angalia hata Marekani.
Tatizo letu ni kuwa tuna wabunge maslahi tu - basi, tena maslahi ya kifedha. Kwenye nchi ambazo watu wanaomba kuwa wabunge ili kupata hadhi - hawafuati mshahara, utendaji unakuwa tofauti kabisa.
Halafu nimesikia kwenye kiapo chao eti "sitatumia cheo changu kwa maslahi binafsi" Inashangaza sana. Naomba mwenye kiapo hicho atuwekee hapa ili kiwe rejea.
Kiapo kiwe hivi: Nitatumia cheo changu kwa maslahi binafsi na nikishiba nitawadharau na kuwatukana walionipa cheo shetani nisaidie.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom