Kwanini jina la Apson Mwangonda?

Kwanini jina la Apson Mwangonda?

Apson anachezewa kama mwanasesere na Lowasa
 
mim sioni kama kuna shida mbona wanajeshi wanastaafu wanapewa ukuu wa mkoa na wilaya...... muacheni mzee Apson atumie ujuzi wake.
 
Leo hii mbona anashambuliwa huyo tu wakati kuna waastafu kibao wapo ktk siasa za bongo au kisa lowassa!!
 
huyu anaendlea na kazi yake kama kawaida,hasa kuhakikisha Lowasa haingii ikulu,anatoa siri zote zinazohusu mipango ya Lowasa

mmh hilo nalo neno inawezekana jamaa ndiye anayeisambaratisha ukawa au?
 
mim sioni kama kuna shida mbona wanajeshi wanastaafu wanapewa ukuu wa mkoa na wilaya...... muacheni mzee Apson atumie ujuzi wake.
 
Jina lake linatajwa kwakuwa ni maradona katika siasa za Tanzania.Anao ujuzi mkubwa katika fani.
Anyway mi sikujua kuwa Tanzania iko kwenye vyama vingi vya siasa.
Mnataka afe njaa akisubiri fadhila...badala ya kutumia ujuziwake.
Mnajua Sarakikya analipwa elfu hamsini kwa mwezi? Jamani acheni kudhalilisha watu.
Hivi mtu akiwa amestaafu miaka 9 iliyopita bado anatakiwa tu akae nyumbani akisubiri kufa hata kama anaujuzi?
Mbona Dr Kitine baada ya kustaafu aliendelea kuwa waziri na kujihusisha na siasa?
Vipi Dr Mahiga aliyeenda kugombea ubunge Iringa Mjini?

Asante mkuu, watu hawataki kumuongelea Dr. Kitine kwa sababu yupo ccm. Juzi tu alikuwa anagombea uraisi, na hakuna thread iliyoanzishwa kwa ajili yake. Au mahiga huko Iringa? Tuache ujinga. Naichukia ccm na watu wote wanaowaza kiccm ccm. Nchi sio ya ccm hii
 
George Bush senior alikuwa mkuu wa CIA ...and then akagombea uraisi baadae...sasa huyu anayekuwa mwenyekiti wa campaign ndio issue?

Vladmir Putin kabla ya kuwa raisi alipata kuwa spy boss wa FSB ( Zamani KGB ) hapo napo jee.?

Hawa jamaa wamekosa point.
 
Ni hatari sana kubadili mwelekeo wa mashua kuielekeza mwelekeo unaopingana na upepo na hasa upepo wenyewe ukiwa ni wenye hasira....
 
mwandishi hana hata uelewa naona katumwa tu na pengine njaa kali inamskuma, na labda kapewa kitu kidogo na baba riz ili aanze kuchafua watumishi wasitaafuvna huu ni uchonganishi na uhuni tu: ndugu yangu uchonganishi wako haukusaidii: chuki binafsi yako juu ya Lowassa haitakusaidia; sasa je ikitokea EL akashinda utaanza kumchonganisha na akina nani tena? au utakuwa ndumila kuwili kama
 
Makala mufilisi ayumkini mwandishi katumwa tu hakuna jipya hapo au kwa sababu Lowassa yupo kati kati ya mtajwa hapo?
 
Kwa hiyo ni sawa Maiga,Kitine kugombea uraisi kupitia ccm ila inakuwa nongwa kwa apson kuunga mkono mgombea uraisi wa upinzani
 
Mbona hatwambii wanajeshi wastafu kuwa wakuu wa mikoa na wilaya??

Nakufahamisha hivi, baada ya vita ya kgera, ilionekana dhahiri kuwa wakuu wa mikoa ya kanda ya ziwa waliogopa vita hivyo kuonyesha ulegevu mkubwa kwa hofu hiyo. Ndipo Mwl Nyerere alipopitisha sheria ya kuwa na wakuu wa mikoa ambao ni wanajeshi. mf. Kulikuwa na Nsa Kaisi kule Kagera na alifanya vizuri sana. Pia kwa ranki ya brigedia (cheo muhimu sana jeshini) ilikuwa ni lazima wafanye kazi za kiraia baada ya kustaafu.
 
Hata Robert Mboma alihusishwa na kutaka kugombea ubunge , naye je!
Njeru kasaka je mbona humtaji na kaina IGP mstaafu Mahita je mbona aligombea ubunge. Serikali ilishatoa nafasi kwa mfanyakazi kujiongezea kipato kwa kazi mbadala tangu henzi za Mzee Ruksa.
 
Tatizo ni njaa inakuwa kali sana baada ya kustaafu. Kama mtu hana uvumilivu lazima anafanya mambo ya kushangaza kama Mzee Apson. Ingekuwa vizuri akajitoa kwenye siasa. Watu wa karibu yake wangemshauri mapema asije akajiharibia maisha yake ya uzeeni. Vilevile labda tuangalie upya sheria kama kuna uwezekano ibadilishwe ili watu wanaokuwa viongozi wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama wazuiwe kujiingiza kwenye siasa. Tuangalie na nchi nyingine wanafanyaje.

Kama kazi imemshinda Othman mumrudishe yeye muache kulialia

Rais mwenyewe anamgombea wake anamuunga mkono yeye mstaafu kwa miaka mingapi sasa kwanini asiwe na mtu wake.
 
Back
Top Bottom