Kwanini jina la Apson Mwangonda?

Kwanini jina la Apson Mwangonda?

singidadodoma

JF-Expert Member
Joined
Nov 11, 2013
Posts
4,394
Reaction score
1,538
JULAI, mwaka 2012, aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa Tanzania, Apson Mwang'onda, alinukuliwa na Gazeti la Nipashe, akimjibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Kazi Maalumu, Profesa Mark Mwandosya, baada ya waziri huyo kuelekeza tuhuma zake za masuala ya siasa kwa mkurugenzi mkuu huyo.


Majibu ya Mzee Apson yalikuwa yakikabili kile kilichoandikwa na Profesa Mwandosya kupitia kitabu chake; "Sauti ya Umma ni Sauti ya Demokrasia" ambamo alikuwa akionyesha namna Apson alivyoshiriki kumchezea rafu za kisiasa.

Mwandosya katika kitabu chake hicho alidai kwamba alihujumiwa na Apson katika mbio za kuwania urais mwaka 2005 na vile vile aliendelea kumhujumu katika harakati za kuwania nafasi ya ujumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa Mkoa wa Mbeya, mwaka 2007.


Angalau katika majibu yake, Apson aligusia suala la maadili ya kazi yake. Kwamba kuhusu kumsaidia Mwandoysa kuusaka urais mwaka 2005, ilikuwa ni vigumu, kwa kuwa; "maadili ya kazi yake hayamruhusu."

Alisema; "Mimi siwezi kuwa mkuu wa Idara, eti nimuunge mkono kwenye uchaguzi wa urais, maadili ya kazi zangu hayaniruhusu hivyo."


Leo hii, kuelekea Uchaguzi Mkuu hapo Oktoba, 2015, jina la Apson Mwang'onda linaibuka tena katika mijadala ya siasa za ushindani wa kuisaka Ikulu.


Jina hili lilianza kuhusishwa na mbio binafsi za Lowassa akiwa ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na sasa, kwa namna fulani linaendelea kuhusishwa na Lowassa huyo huyo akiwa ndani ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).


Apson kwa sasa ni Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa mstaafu, mwenye kuendelea kula matunda ya kazi yake hiyo ambayo bila shaka, aliifanya kwa umahiri mkubwa na anastahili pongezi. Kazi ambayo kwa nukuu yake hapo awali, aliifanya kwa kuzingatia maadili na vile vile kwa sasa, anastahili kuendeleza maadili, nidhamu na unyenyekevu wake huo katika wakati huu wa maisha yake ya kustaafu.


Naam, katika maisha yake ya kustaafu kama mmoja wa wakuu wa masuala ya ujasusi nchini bado, kwa sababu za maana na muhimu, anapaswa kuendelea kuheshimu kiapo chake cha kudumu. Kiapo ambacho anapaswa kukiheshimu kwa kadiri ya maisha yake. Hata hivyo, kutokana na jina lake kuendelea kuhusishwa na mikakati ya binafsi ya kusaka urais ya mmoja wa wasaka madaraka hayo makubwa zaidi nchini, heshima yake kwa kiapo chake hicho katika maisha yake ya kustaafu inatia shaka.


Kutajwa mara kwa mara kwa Mzee Apson katika mapambano binafsi ya kisiasa miongoni mwa makundi ya wanasiasa kunafifisha nidhamu ya kiapo chake hicho na kwa kweli hatua hiyo inapandikiza nakisi kubwa mno katika muktadha wa kutii mamlaka ya juu.Ni sawa na kusema, baada ya kustaafu, Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa anaweza kuishi maisha kwa kadiri anavyotaka, ikiwamo hata kuthubutu kupuuza mamlaka ya juu zaidi, kwa wakati husika.


Hebu tafakari, hali inakuwaje pale Mkurugenzi Mkuu mstaafu (A) wa Idara ya Usalama wa Taifa anapoamua kutumia uzoefu wake wa kijasusi kumpigania mwanasiasa binafsi (A) na vile vile, Mkurugenzi Mkuu mstaafu (B) naye anaamua kutumia uzoefu wake wa kijasusi kumpigania kufa au kupona mwanasiasa (B)? Hali itakuwaje Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama (A) aamue kutumia uzoefu wake kumpigania kufa au kupona mwanasiasa (A) katika kuisaka Ikulu na kisha Mkuu (mstaafu) wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama (B) aamue kumpigania mwanasiasa (B)?

Katika muktadha huo, najiuliza kwa nini jina la Mzee Apson linatajwa?


Na kwa kweli, wakati najiuliza hivyo, natambua kwamba wapo viongozi wakuu wa kitaifa wa vyombo vya ulinzi na usalama nchini ambao maisha yao ya kustaafu ni mfano bora kwa wenzao waliochukua nafasi zao.

Kwa mfano, hakuna shaka yoyote kwamba Jenerali Mirisho Sarakikya, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama (mstaafu) amekuwa mmoja wa wakuu wa kupigiwa mfano wa namna ya kuishi kwa nidhamu ya kuheshimu kiapo katika maisha ya kustaafu.


Nina uhakika, pengine siku moja akiwa amekwishakwea Mlima Kilimanjaro kwa mapenzi yake mwenyewe, na akiwa huko akasikia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anapita jirani na anga la mlima huo, atapiga saluti ya utii.

Kwa maana nyingine, atakuwa anaendeleza nidhamu ya kijeshi katika maisha yake ya kustaafu.
Hakuna mgombea urais ambaye mbio zake zimehusishwa na Sarakikya. Hakuna mgombea urais ambaye mbio zake za kuisaka Ikulu zimehusishwa na Jenerali (mstaafu) George Waitara.


Wanatii viapo vyao, hawataki kutumia uzoefu wao kufaidisha kundi binafsi la msaka madaraka kwa gharama za ustawi wa nchi. Wanaweza kutumia uzoefu wao kutoa ushauri katika mamlaka husika na si kwa genge binafsi la kusaka madaraka.


Wanatambua wakifanya hivyo watakuwa wameweka rekodi (precedent) mbaya- tena mbaya kabisa- kwa vizazi vijavyo vitakavyokuwa na majukumu waliyowahi kuyashika nchini.

Nawasifu hao na wengine wengi nchini, kwa kuwa sikusikia majina yao yakitajwa, nimeshangaa kusikia jina la Mzee Apson likitajwa mara kwa mara kwenye michuano binafsi ya kisiasa miongoni mwa wanasiasa. Najiuliza kwa nini? Kuna lengo gani?


Kwa kiongozi wa ngazi ya juu mfano wa Apson, maisha yake ya kustaafu yanapaswa kubeba deni kwa taifa.

Ni deni kwa taifa kwa sababu alitumia nguvu, akili, na kila mbinu kulitumikia kwa heshima kubwa taifa lake na kwa hiyo, baada ya kustaafu, taifa nalo ni lazima lilipe deni hilo na deni husika linaweza kulipwa kwa njia nyingi ikiwamo kuhakikisha anapata, bila vikwazo, stahiki (privileges) zake kama bosi mstaafu.


Hata hivyo, inawezekana vipi kuvumilia kutoa stahiki husika kwa mhusika ambaye tayari sehemu ya jamii inabeba tafsiri tofauti dhidi yake – tafsiri inayofanana na mtu anayekusudia kuukata mkono unaomlisha.

Katika maisha yake ya kustaafu yeye bado ni alama ya idara aliyowahi kuitumikia.

Ndivyo ilivyo, kwamba ingawa amestaafu lakini bado anaendelea kuwa alama ya taasisi hiyo katika maisha yake hayo ya kustaafu.


Bado swali liko pale pale; kwa nini Apson? Kwa nini sio wengine? Kwa nini siyo Waitara au Sarakikya ingawa wao walikuwa wakuu wa majeshi ya ulinzi na usalama? Hakika, nadhani ni wakati sasa kwa mamlaka husika kuchukua uamuzi wa kubadili mwelekeo wa mashua ili kufika katika kituo stahili.


Kubadili mwelekeo wa mashua inawezekana kuliko kubadili mwelekeo wa upepo unaovuma baharini au ziwani.

Aliwahi kusema Jimmy Ray Dean, mwanamuziki, mfanyabiashara na mtangazaji wa televisheni kwamba; "I can't change the direction of the wind, but I can adjust my sails to always reach my destination."


Chanzo: Raia Mwema Toleo la 417
5 Aug 2015
 
Ina maana ikatokea tu wewe kufanya kazi kwenye 'idara' basi unakuwa umekwisha uza utu wako(sold your soul) kwa hiyo department. Kwamba angekuwa anamsupport mgombea wa chama tawala ingeonekana haina shida ingechukuliwa yupo sawa kabisa anatii kiapo chake. Lakin kwasababu anamsupport mtu ambae sio ccm inaonekana anakiuka kiapo. Come on, watanzania wa leo sio wajinga hivyo.

After all this is democratic country. Je, kiapo chake kilikuwa kinamzuia maisha yake yote asijihusishe na siasa, je katiba inasemaje kuhusu haki za kila raia. CCM imeingia woga kwasababu mtu anaejua mambo mengi yao kwa mara ya kwanza hayupo nao. Poleni
 
Tatizo ni njaa inakuwa kali sana baada ya kustaafu. Kama mtu hana uvumilivu lazima anafanya mambo ya kushangaza kama Mzee Apson. Ingekuwa vizuri akajitoa kwenye siasa. Watu wa karibu yake wangemshauri mapema asije akajiharibia maisha yake ya uzeeni. Vilevile labda tuangalie upya sheria kama kuna uwezekano ibadilishwe ili watu wanaokuwa viongozi wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama wazuiwe kujiingiza kwenye siasa. Tuangalie na nchi nyingine wanafanyaje.
 
Jina lake linatajwa kwakuwa ni maradona katika siasa za Tanzania.Anao ujuzi mkubwa katika fani.
Anyway mi sikujua kuwa Tanzania iko kwenye vyama vingi vya siasa.
Mnataka afe njaa akisubiri fadhila...badala ya kutumia ujuziwake.
Mnajua Sarakikya analipwa elfu hamsini kwa mwezi? Jamani acheni kudhalilisha watu.
Hivi mtu akiwa amestaafu miaka 9 iliyopita bado anatakiwa tu akae nyumbani akisubiri kufa hata kama anaujuzi?
Mbona Dr Kitine baada ya kustaafu aliendelea kuwa waziri na kujihusisha na siasa?
Vipi Dr Mahiga aliyeenda kugombea ubunge Iringa Mjini?
 
Mkuu hao jamaa huwa hawastaafu na ndio maana Top Spy Iran mmoja alipohsiwa kutaka kumsaidia Mrema wa upinzani tunajua kilchotokea.

Kwa suala la Lowasa kwa kweli wengi liwapa kizungumkuti.
 
Ina maana ikatokea tu wewe kufanya kazi kwenye 'idara' basi unakuwa umekwisha uza utu wako(sold your soul) kwa hiyo department. Kwamba angekuwa anamsupport mgombea wa chama tawala ingeonekana haina shida ingechukuliwa yupo sawa kabisa anatii kiapo chake. Lakin kwasababu anamsupport mtu ambae sio ccm inaonekana anakiuka kiapo. Come on, watanzania wa leo sio wajinga hivyo. After all this is democratic country. Je, kiapo chake kilikuwa kinamzuia maisha yake yote asijihusishe na siasa, je katiba inasemaje kuhusu haki za kila raia. CCM imeingia woga kwasababu mtu anaejua mambo mengi yao kwa mara ya kwanza hayupo nao. Poleni

Hans Kitine alikuwa ni mkurugenzi wa Usalama wa Taifa na ameingia kwenye siasa na akawa mbunge na akawa waziri na amegombea Urais akakosa.

Waandishi njaa kama Dilunga wanatia aibu fani ya habari.

Cc: Pasco jackton Manyerere Mzee Mwanakijiji maggid
 
Last edited by a moderator:
APSON ni FUSKA wa kupenda pesa. Hivi kweli Mkurugenzi Mstaafu wa Idara Nyeti kama hiyo ya Usalama wa Taifa siyo alipaswa kukaa mbali kabisa na maswala ya siasa. MBAYA kabisa anajihusisha na Mtu ambaye anatuhumiwa na UFISADI. KITENDO tu cha kutuhumiwa kwa UFISADI ni kigezo tosha cha APSON kukaa mbali na LOWASSA , lakini kwa kwa sababu tu tamaa ya pesa anaweka UTANDO WA BUIBUI MACHONI NA MASKIONI na kujifanya hajui uchafu wa LOWASSA.
 
Hivi kujihusisha na siasa tafsiri yake ni kuwa mwanasiasa wa upande wa upinzani? Kama ni kujihusisja na siasa ni nani anayewapeleka huko? Siyo Serikali na CCM?
Huyo mwandishi anajua Kinana ni nani? Membe? Pinda? Vipi kuhusu wakuu wa wilaya na wakuu wa mikoa?
Naona mwandishi wa makala haya amejiminya sana kiakili na kiupeo.
By the way Don't mess up with Apson, never under estimate himi.
 
Ni kwa sababu tu inasemekana yuko bega kwa bega na mgombea wa upinzani, Edward Lowassa. Nadhani hili ndilo tatizo na kasoro kwa upande wako mwandishi wa Makala hii!

Lakini umesahau kwamba kuna mtu ambaye amewahi kuwa na cheo na wadhifa kama huohuo, yeye si tu kaonesha mapenzi yake kwa mgombea flani bali anashiriki siasa za moja kwa moja na aliomba ateuliwe na CCM agombee Urais!.....Huyu si mwingine bali ni Hans Kitine!!!

Na laiti kama ulimsikiliza siku anatangaza rasmi kuingia ktk kinyang'anyiro hicho, ni kana kwamba mtu ambaye hajawahi kushika wadhifa nyeti kama huo ndani ya serikali hiyohiyo inayoongozwa na chama hichohicho alichokuwa anaombea ridhaa ya uteuzi!!

Tatizo hapa si mtu au cheo cha mtu, bali ni utaratibu wetu wa kujiongoza na kujitawala kupitia Katiba yetu, hauko sawa!

Mwacheni Apson Mwang'onda aelekeze mapenzi yake ya kisiasa kwa mtu anayemtaka. Tena mimi ningependa afanye vile kwa uwazi tu bila kuficha kitu!!
 
George Bush senior alikuwa mkuu wa CIA ...and then akagombea uraisi baadae...sasa huyu anayekuwa mwenyekiti wa campaign ndio issue?
 
APSON ni FUSKA wa kupenda pesa. Hivi kweli Mkurugenzi Mstaafu wa Idara Nyeti kama hiyo ya Usalama wa Taifa siyo alipaswa kukaa mbali kabisa na maswala ya siasa. MBAYA kabisa anajihusisha na Mtu ambaye anatuhumiwa na UFISADI. KITENDO tu cha kutuhumiwa kwa UFISADI ni kigezo tosha cha APSON kukaa mbali na LOWASSA , lakini kwa kwa sababu tu tamaa ya pesa anaweka UTANDO WA BUIBUI MACHONI NA MASKIONI na kujifanya hajui uchafu wa LOWASSA.

Lowasa ni clean ndio maana apson anamsapot...swala la kukatwa ni mabifu ya kifamilia
 
Ina maana ikatokea tu wewe kufanya kazi kwenye 'idara' basi unakuwa umekwisha uza utu wako(sold your soul) kwa hiyo department. Kwamba angekuwa anamsupport mgombea wa chama tawala ingeonekana haina shida ingechukuliwa yupo sawa kabisa anatii kiapo chake. Lakin kwasababu anamsupport mtu ambae sio ccm inaonekana anakiuka kiapo. Come on, watanzania wa leo sio wajinga hivyo. After all this is democratic country. Je, kiapo chake kilikuwa kinamzuia maisha yake yote asijihusishe na siasa, je katiba inasemaje kuhusu haki za kila raia. CCM imeingia woga kwasababu mtu anaejua mambo mengi yao kwa mara ya kwanza hayupo nao. Poleni

well said
 
Ni kwa sababu tu inasemekana yuko bega kwa bega na mgombea wa upinzani, Edward Lowassa. Nadhani hili ndilo tatizo na kasoro kwa upande wako mwandishi wa Makala hii!

Lakini umesahau kwamba kuna mtu ambaye amewahi kuwa na cheo na wadhifa kama huohuo, yeye si tu kaonesha mapenzi yake kwa mgombea flani bali anashiriki siasa za moja kwa moja na aliomba ateuliwe na CCM agombee Urais!.....Huyu si mwingine bali ni Hans Kitine!!!

Na laiti kama ulimsikiliza siku anatangaza rasmi kuingia ktk kinyang'anyiro hicho, ni kana kwamba mtu ambaye hajawahi kushika wadhifa nyeti kama huo ndani ya serikali hiyohiyo inayoongozwa na chama hichohicho alichokuwa anaombea ridhaa ya uteuzi!!

Tatizo hapa si mtu au cheo cha mtu, bali ni utaratibu wetu wa kujiongoza na kujitawala kupitia Katiba yetu, hauko sawa!

Mwacheni Apson Mwang'onda aelekeze mapenzi yake ya kisiasa kwa mtu anayemtaka. Tena mimi ningependa afanye vile kwa uwazi tu bila kuficha kitu!!

huyu jamaa hajiewelewi, mwambie Jaji Agustino Ramadhani alikuwa wa CCM au Serikali.....?
 
Back
Top Bottom