muda wa ukombozi
Senior Member
- Jun 28, 2013
- 129
- 118
Rais wa Jamhuri ya Muungano aliunda aliunda tume ya kuchunguza mchanga unaosafirishwa na ilibaini kuna upotevu wa kiasi kikubwa cha fedha kwa mwezi ni bilioni 829.4 x 12 x miaka 18= zaidi ya tirilioni 800 huko.
Rais akaja kuridhia mapendekezo ya kamati na kusisitiza kwenye hili watz tushikamane tuweke sasa pembeni siasa tuwepamoja kwenye hili la madini.
Mbunge wa zamani kafulila kamsifia Rais, wabunge waliowengi wamsifia rais wetu isipokuwa Rais wa TLS, yeye ameenda kinyume na rais wetu akisema tukipelekwa kwenye zile arbitration za kimataifa tutaumbuka ingawa anakiri na katoa mfano kwenye andiko lake kuwa process yote ya kampuni flani inafanyika Japan.
kwahiyo anakiri mapungufu yote, fedha zinazopotea, kitu ambacho anashauri rais wa TLS ni kuwa vingetengenezwa vinu kwanza, na mikataba ingefanyiwa "addendum" ndipo mambo haya yangeendelea, kwa kifupi fikra zake ku deal na hii issue imeishia hapo, zaidi ni kuilalamikia serikali kwamba itaingia katika mgogoro ambao haitabaki Salama.
Mbunge wa mtwara naye ni upinzani amekuja na express obligation na implied obligation kwenye ambapo ukimsoma unaona kabisa kuna kiutafiti kidogo amekifanya ambacho ni cha kiuzalendo.
Sasa nashangaa sana kwanini tusifanye tafiti, tukashawishi nchi za huko wajue jinsi tnavyoibiwa?
Kwenye hili ata tukishindwa hizo kesi kwsb ya hizo bogus treaty bado ulimwengu utajua kwamba tunaibiwa kwsb ya ubongolala wetu.
Kwanini lissu usiwe pamoja na serikali ukiwa kama rais wa TLS kwenye kutangaza hili, ulimwengu mzima ujue tumeibiwa sana na ikibidi tutumie hiyo implied obligation kusaka haki, tuangalie wananchi wanaozunguka migodi hiyo bado wanaishi kwenye umasikini mkubwa dunia lazima ijue, machimbo mengine madini yameisha hakuna faida iliyopatikana zaidi ya umasikini kuongezeka, Hawa watu kutumia idhaifu tulionao kujinufaisha wao na kuacha Tanzania kuendelea kutegemea misaada toka kwao ambayo haikidhi mahitaji bado kuna upungufu mkubwa wa madawa mahospitalini, bado upangaji wa bejeti unakuwa mgumu ukilinganisha na fedha zilizopo.
Kwanini kwenye baadhi ya mambo tusiwe pamoja tukaachana na sasa ambao hazina afya kwa taifa?
Kuliko kila kitu kikitokea mnatuchanganya tu maandiko tofauti tujitahidi tisivuragane kwenye mambo ambayo yanatija kwa taifa.