Kwanini ilinibidi niache Shule

Kwanini ilinibidi niache Shule

Kwa jina naitwa Michael Luoga (chuma masofa ) mzawa wa Songea mkoani Ruvuma

Mimi ni mtoto wa kwanza wa familia ya watoto 5 mimi ni mtoto wa familia ya kipato cha chini nimezaliwa mwaka 2000 nikapata elimu ya msingi katika Shure ya msingi madizini Songea mwaka 2015 nikahitimu na mwaka 2016 nikajiunga na Shule ya Sekondari Rondoni Songea maisha ya Shule yalikuwa mazuri nikamaliza mwaka wa Kwanza mwaka wa pili ulipoanza nkaendelea na masomo ila ilipo fika mwenzi wa nne niliacha shule

Sababu zilizonifanya niache shule

1. Niliona walio na elimu wakihangaika mtaani na hasa alikuwa binamu yangu aliekuwa kasomea masuala ya ardhi anazurula mtaani

2. Hali ya kimaisha ya familia yalikuwa magumu sana hivyo mahitaji ya Shule mzazi akuweza kukizi japo aling'ang'ana nisome tu hivyohivyo, nakumbuka niko form one nilienda Shule kiugumu sana na naingia form two mdogo wangu anaenifuata naye anaingia form one dah nikaona game hili gumu nikaamua kujivua japo nilipingwa Sana.

3. Nilipima nikaona elimu ya mtaani inalipa kwa haraka endapo kama ntakuwa makini na serious na maisha

Maisha baada ya kuacha shule
Nilianza harakati za kutafuta hela ili nikajifunze udereva nilipoanza hizo harakati nakumbuka kulikuwa kuna kanisa linajengwa kata ya Lizaboni Songea nikapata ajira ya kumimina zege lakini Mungu si Athumani siku ya pili alifika kaka yangu mtoto wa mama mkubwa na tukaongea akanichukua nikaenda kujifunza kutengeneza sofa na safari nyingine ikaanzia hapo.

Maisha kuanza kwenye ufundi yalikuwa na changamoto nyingi na majaribu ila nlikomaa nayo na hatimae nikawa fundi lakin lavel ya kiasi tu pale nikaanza kupata fedha kidogo kidogo ndipo baadae kidogo nikapata nafasi ya kwenda wilaya ya Mbinga kufanya kazi kwenye ofisi za Uncle Sam furniture TZ, nIkafanya kazi kwa mUda wa miezi kadhaa lakini nako nikafeli tena, nilikosa malipo ya muda wote nliofanya kazi zaidi ya posho tu dah ikawa changamoto tena maana nilitegemea muda niliofanya kazi pale ile pesa ndio ingekuwa mtaji wa kufungua ofisi yangu lakini nikaangukia pua dah kwa leval ya ufundi niliyokuwa nayo ilikuwa ndogo basi nikajitosa tena kwenda kujifunza zaidi nikaenda kujifunza kazi tena kwa Novath Samwel mmiliki wa Bravo sofa sets.

Mwanzo maisha nilioishi na jamaa zangu kina Novath yalikuwa mazuri na wala sikujutia swala la kujifunza zaidi tukaenda enda lakini mbele ikawa changamoto tena kama kutengwa na kila rafiki wa mwanzo wa ofisi nilizokuwa nafanya kazi na watu wa karibu na pia ikafika kipindi hata hao watu niliokuwa nao kwa muda huo nao kutoelewana nao na kufikia mwaka 2019 ikabidi niondoke nikaja zangu Mafinga pasipo kujua namfata Nani wa ndugu wa jamaa wa karibu

Maisha ndani ya Mafinga yakawa magumu tofauti na nilivyotarajia nilichoamini nimeumbwa Wala sijajiumba hivyo maisha ni mzunguko iko siku nitapata tu nikasonga kibishi na baada ya miezi miwili nikafanikiwa panga chumba na baada ya hapo nikakutana na kampani ya kamkopo nikafungua ofisi na mpaka sasa naendelea vizuri na ninapata umaarufu wa kazi nzuri za fanicha so now nmewashika na wengine mkono wengine hata siwajui lakini naishi nao tukisaka chapaaa

Ushauri
Ukiona elimu haifai usilazimishe kwa kumridhisha mzazi au mwalimu fanya lengo lako kwa wakati na pia marufuku kukata tamaa maana ukikubali kushindwa basi utarudi nyuma mara kumi zaidi lakini sikushauri uache shule hapana soma Kwanza.

Na kingine riziki yako inavyokuja basi huvuta misuli ya akili ielekee uko ukijiona unafaa basi na wanadamu watakuona unafaaa so thanks I love u

With Michael luoga chuma ...maneger c.m.f sofa sets mafinga
Support vijana kwanza... Luck angel crew dancer
Saport pinga ukatili ..nasoma kwanza

View attachment 1541054
Kazi inapendeza! Mafanikio mema!
 
Hongera sana
Tatizo vitoto vya shule na vigraduate vya kibongo vimejaa humu jf haviwezi kukuelewa
Kama hii ni stori yako ya kweli, unayaweza
Kama ni shule hata mimi nimeisoma na sio kibongobongo lakini bado naona kama nilipoteza muda.
Mafanikio yako yana mwanga ndani yake, watakuja kuomba kazi kama kwa Chibu.
 
Lengo ni kutomboa tu, so pambana ya hela yote na uwapuuze hawa walimu wa lugha wa jf.
 
Hongera sana
Tatizo vitoto vya shule na vigraduate vya kibongo vimejaa humu jf haviwezi kukuelewa
Kama hii ni stori yako ya kweli, unayaweza
Kama ni shule hata mimi nimeisoma na sio kibongobongo lakini bado naona kama nilipoteza muda.
Mafanikio yako yana mwanga ndani yake, watakuja kuomba kazi kama kwa Chibu.
Mie najichekeaga tu Kuna mjamaa fulani anaitafuta PhD lakini maisha aloyonayo🤸🤸!na anaamini siku mambo yatakuwa poa..haya maisha bila kutuliza akili utaenda hata havard lakini kitaa kitakutema tu usipokuwa makini!
 
But yule mwenye uwezekano wa kumiliki ela ndefu ni yule ambae anaingia risk katika kuwekeza.Ukiwa umeajiriwa huwezi kupanga jambo likatimia sababu umelimitiwa na aliekuajiri na muda ni mchache Umri unaenda.
Inategemea wapo walioanzia kuajiriwa wakajiajiri
 
Mie najichekeaga tu Kuna mjamaa fulani anaitafuta PhD lakini maisha aloyonayo🤸🤸!na anaamini siku mambo yatakuwa poa..haya maisha bila kutuliza akili utaenda hata havard lakini kitaa kitakutema tu usipokuwa makini!


Si unaona mwenyewe wasomi wengi wanaingia CCM na elimu zao ili kieleweke,
kwa sisi wa kusoma na kazi hata kieleweki
 
Hongera sana
Tatizo vitoto vya shule na vigraduate vya kibongo vimejaa humu jf haviwezi kukuelewa
Kama hii ni stori yako ya kweli, unayaweza
Kama ni shule hata mimi nimeisoma na sio kibongobongo lakini bado naona kama nilipoteza muda.
Mafanikio yako yana mwanga ndani yake, watakuja kuomba kazi kama kwa Chibu.
Hakuna msomi duniani mwenye muandiko huu.
 
Huu ni uthibitisho kuwa kweli uliacha shule, ila endelea kupambana

WATAKAOKUJA KUKUOMBA OWAONYESHE NJIA, NI WALE WALIOSEMA HUTOBOI - FidQ
Acheni ujuaji kwa hyo ww hapo kwenye neno "usilazimishe" umeweka Red colour kwamba imekosewa au? ulitaka napo aandike usirazimishe?
 
Back
Top Bottom