Kwanini hujikubali jinsi ulivyo?

ladyfurahia

JF-Expert Member
Joined
May 10, 2011
Posts
14,758
Reaction score
9,592
Habarini wanajamvi wenzangu

Leo nimeona niseme nanyi mambo kadha wa kadha ambayo mwanadamu
anashindwa kuyafanya kutokana na dhana potofu iliyojengeka mawazoni
mwake, kwamba hawezi fanya kitu hicho, anajiona mnyonge na duni sana
maskini wa mawazo na mpunjufu wa moyo kutokana ile dhana ya kutokuji-
KUBALI jinsi vile alivyo.

Kwanini watu wengi siku hizi hasa vijana hawana mwitikio wa kujituma
kwa nguvu zao ili kujipatia kipato kinachotakiwa kwao na familia zao.
Kwanini wanawake wengi wamekuwa watu tegemezi walio duni kimawazo
kinguvu na kiakili pia. Kwanini watu wanashinda hata mambo madogo
kuyafanya mpaka amwite mchina toka korea, japan aje kufanya hilo jambo
pasipo yeye mwenyewe kuwaza, kubuni na kulitekeleza hilo jambo?

Kimtazamo wangu naona ile hali ya KUTOJIKUBALI ndiio inayofanya mtu
ajione kuwa hawezi na wala hakuumbwa kufanya jambo hilo anabaki
mdumaza kiakili, kiroho na kimwili pia. Marafiki zangu nawaomba msiwe
watu wa aina hiyo wasiojikubali wao wenyewe jinsi walivyo.
Rafiiki hebu jikubali na ujisemee moyoni kuwa unaweza kufanya
mambo makubwa yasiyotamkika kwako yakawezekana na utakuwa
mshindi zaidi ya washindi. Nawapenda

ciao
 
ungetoa hilo neno wanawake ningekuelewa zaidi.
 
kwani ulikuwa unamaanisha kipengele hichi
Kwanini wanawake wengi wamekuwa watu tegemezi walio duni kimawazo
kinguvu na kiakili pia. Kwanini watu wanashinda hata mambo madogo
kuyafanya mpaka amwite mchina toka korea, japan aje kufanya hilo jambo
pasipo yeye mwenyewe kuwaza, kubuni na kulitekeleza hilo jambo?

akitoea kwani kuna ubaya gani mbona mm naona point yake ni nzuri sana wala hajataja kwa ubaya bestito?
ungetoa hilo neno wanawake ningekuelewa zaidi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…