Bowie
JF-Expert Member
- Sep 17, 2016
- 4,373
- 6,084
Mheshimiwa Rais Magufuli ameunda tume mbili ili kuchunguza mambo yanayohusiana na mchanga wa dhahabu. Jana wakati CAG akitoa ripoti bungeni alisema makampuni haya huwa yanasema yanapata hasara.
Hizi tume mbili zilizoteuliwa na Rais zingefaa kuchunguza zaidi kwa undani zaidi mikataba yote ya hizi kampuni kwa undani, leo mtumishi wa serikali na mfanyabiashara mdogo na mkubwa anawajibika kutoa kodi wakati kampuni inachimba dhahabu inadai inapata hasara. Hizi kamati zinatakiwa zichunguze idadi ya kilo ya dhahabu iliyosafirishwa. Hii kampuni ya ACACIA ilishawahii kudanganya idadi ya dhahabu inayochimba na kusafirisha kwahiyo si kampuni ya kuaminika.
Mikataba ya Gesi pia ipitiwe kwani hawezekani Gesi ichimbwe hapa na kampuni ya kigeni halafu tunauziwa kwa bei kubwa utafikiria tumeagiza Qatar. Tume hii ichunguze kama uchimbaji na usafirishaji umeanza huko baharini makampuni haya yalipowekeza.