Kwanini hizi Pajero zenye plate numbers za herufi AHN au AKH zinaogopwa sana Tanzania nzima?

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,544
108,877
Hizi Pajero nyeupe ambazo nyingi huwa zina plate numbers zenye herufi AHN au AKH ni za Kampuni au Taasisi au Shirika gani hapa nchini Tanzania? Na kwanini Watu wengi sana huwa wanaziogopa japo nyingi sana huwa zinaonekana zina usajili uliokamilika na halali kabisa?

Najua humu JF huwezi kukosa majibu ya uhakika hivyo nitashukuru kama nami pia nikielimishwa kuhusu hayo magari ya Pajero na yenye hizo plate numbers zenye hizo herufi tajwa hapo juu ili nami pia niwe sehemu ya wale ambao wanaziogopa.

Nawasilisha.
 
Wale jamaa group kikosi kazi cha baba bashite wao wakifanya tukio ubatizwa na kuitwa WASIOJULIKANA.

GET WELL SOON LISSU

SWISSME

Maelezo yako bado sijayaelewa vizuri Mkuu halafu ukizingatia Mimi sijui sana Kiswahili chenu huko Tanzania kutokana na Unyarwanda wangu hivyo kama hutojali naomba uniandikie vizuri tu ili niweze kukupata / kukuelewa vyema. Kwa mfano sijui Bashite ina maana gani, pia sijui Group Kikosi Kazi na wasiojulikana hapo umemaanisha nini. Naomba ufafanuzi tafadhali Mkuu.
 
Pajero zamani,kwa sasa Nissan nyeupe

Napishana na hizo Pajero kila Sekunde, Dakika, Saa, Siku, Wiki, Miezi na Miaka na nyingi zikiwa na hizo hizo plate numbers zenye hizo herufi tajwa hapo juu lakini hizo Nissan zako huwa naziona kwa nadra kama siyo kwa kubahatisha mno!
 
Maelezo yako bado sijayaelewa vizuri Mkuu halafu ukizingatia Mimi sijui sana Kiswahili chenu huko Tanzania kutokana na Unyarwanda wangu hivyo kama hutojali naomba uniandikie vizuri tu ili niweze kukupata / kukuelewa vyema. Kwa mfano sijui Bashite ina maana gani, pia sijui Group Kikosi Kazi na wasiojulikana hapo umemaanisha nini. Naomba ufafanuzi tafadhali Mkuu.

Kamuulize LISSU,ROMA MKATORIK,MWAMDISHI WA HABARI,BENN SAANANE,ALFOSO MAWAZO,CLOUDS FM, na wengine wamefungiwa kwenye viroba na kutupwa majini.

Swissme
 
Kamuulize LISSU,ROMA MKATORIK,MWAMDISHI WA HABARI,BENN SAANANE,ALFOSO MAWAZO,CLOUDS FM, na wengine wamefungiwa kwenye viroba na kutupwa majini.

Swissme

Samahani kuna ' logical connection ' gani kati ya hayo maelezo yako na umiliki wa Gari hizo aina ya Pajero zenye plate numbers zenye herufi AHN na AKH? Kuna mahala popote labda nimeulizia kuhusu hao sijui akina Lissu, Roma Mkatoliki, Mwandishi wa Habari, Ben Saanane, Alfonso Mawazo, Clouds fm na waliofungwa katika Viroba na kutupwa majini?
 
Hakuna shida hapo hata kidogo. Ni kuwa serikali magari yake mengi ni kutoka Japan na ilitokea kuwa mzigo mkubwa Wa magari ya idara za serikali kwa wakati fulani ilikuwa pajero Mitsubishi zile za milango mitano. Na rangi ya serikali ktk majengo au magari ni nyeupe. Kuogopwa hapo ni suala jingine halihusiani na magari.
 
Mkuu swali lako mbona simpo tu, hizo gari huwa zinafanya kazi ya kuwachukua wanachuo (mademu) na kuwapeleka kunywa Juisi Pombe Maembe
 
Wale jamaa group kikosi kazi cha baba bashite wao wakifanya tukio ubatizwa na kuitwa WASIOJULIKANA.

GET WELL SOON LISSU

SWISSME
Zile zilikuwa za Maafisa Usalama wa mikoa na wilaya....na nyinine zilikuwa makao makuu. wengi wameshauziwa kwasababu zimechoka, japo zipo chache bado zinadunda.

Ogopa Nissan nyeupe inayo Patrol, Landcruiser nyeupe msumari yenye mkonga na Noah nyeusi.

Nabii Tito......sio mimi.
 
Hizi Pajero nyeupe ambazo nyingi huwa zina plate numbers zenye herufi AHN au AKH ni za Kampuni au Taasisi au Shirika gani hapa nchini Tanzania? Na kwanini Watu wengi sana huwa wanaziogopa japo nyingi sana huwa zinaonekana zina usajili uliokamilika na halali kabisa?

Najua humu JF huwezi kukosa majibu ya uhakika hivyo nitashukuru kama nami pia nikielimishwa kuhusu hayo magari ya Pajero na yenye hizo plate numbers zenye hizo herufi tajwa hapo juu ili nami pia niwe sehemu ya wale ambao wanaziogopa.

Nawasilisha.
usalama wa Taifa ni taasisi ya siri huko kwenu mijini tu, lakini sisi wa mikoani tunazijuwa ofisi za DSO na mpaka kituo cha basi zinazopita hapo kituo kinaitwa usalama hasa watu wa Mwanga watanielewa vizuri.

Hizo Pajero wanazotumia zinajurikana ila kwa sasa wana magari ya kisasa kama Nissan Patrol, hizo Pajero hazitumiwi tena na maofisa wa ngazi za juu.
 
Back
Top Bottom