Kwanini hiki chuo kisijengwe ARUSHA?

Mtoto wa Mkulima

JF-Expert Member
Apr 12, 2007
681
126
Hii dhana ya kuwa kila kitu kifanyike dar bila kuangalia strategic location nadhani ni matatizo ya kimaamuzi. Serikali inampango wa kujenga chuo kipya na cha kisasa cha utalii Dar. Mimi kwa moani yangu ningependekeza hiki chuo kijengwa Arusha ambako ndio kuna mandhari ya kitalii au badi Bagamoyo. Hii nadhani ninjia moja wapo ya kupunguza idadi ya watu Dar na kujenga ajira nnje ya Dar. Sio lazima kijengwe Arusha tuu lakini nasugest kisijengwe Dar.
 

Naikubali hii 100%, kila kitu Dar na miji mingine itapanuka vipi kama hawataweza kusambaza huduma kama hizi mikoani. Angalia sasa hivi Dodoma inavyokuwa kwa kasi ni kwasababu za msingi za wanaojua kupeleka huduma za kijamii kama hizi za vyuo huko. Huyu Maghembe nae tutaanza kutia mashaka na visions zake naona kama anaenda kwa nguvu za upepo hamna maamuzi ya maaana anayoyafanya.

Halafu eti ndio Prof? Hivi huduma hizi ni lazima ziwe Dar peke yake jamani? Mbona hawa watu hawaambiliki au ndio mnataka tuwe kama Ufilipino kuandamana nchi nzima. Kwanza acha tusubiri tuone kama atabakia hapo wizarani itakapofika January tarehe za kati ya mwezi.

Mikoa kama Ruvuma, Rukwa, Singida, Lindi, Mtwara, Kigoma, Shinyanga, Tanga itakuwa lini kama Dar???????
 
Hawa wanapenda tu kongeza msongamano wa magari Dar!
Kwani Dar kuna utalii gani wa maana? Kijengwe- Bgy, Moshi, Arusha ambako ndo kuna watalii wengi!
 
mbona watu mwashindwa kuelewa hicho chuo ni kwaajili ya watali? ama cha mafunzo yautali?isomen maada muielewe msikurupuke oforo
 
kijengwe Lindi au Mtwara,Lengo ni kuongeza kasi ya Maendeleo ya Mikoa hiyo!
 
Kitakuwa pale mjini nyuma ya International House. Kwa sasa panatumika kama sehemu ya kuoshea magari.
 
mbona watu mwashindwa kuelewa hicho chuo ni kwaajili ya watali? ama cha mafunzo yautali?isomen maada muielewe msikurupuke oforo


Bwana huku sio kukurupuka. Chuo ni cha utalii hivi wewe unaweza kujenga chuo cha uvuvi DODOMA? Nyie mmezoea kufanya mambo kwa nadharia tuu na ndio maana practicaly?


Hawa wanafunzi wanatakiwa wa practice, kuna mambo ya camoing, kuna mambo ya tour guiding, kuna mambo ya field.

Tusiwe tunafikiria ndani ya mipaka tuu chuo kama hiki kina mambo mengi wachumi wanaita tricle down effect. Okay hebu tupe sababu ni kwanini wewe unaona hiki chuo kinafaa kiwe Dar?
 
Mtoto wa wakulima, Kuntakinte na MZalendo
Nilimuuliza Blandina Nyoni swali hilohilo alipotoka kwenye mkutano wa kuutangaza utalii China. Alisema hiyo ni requirement waliyotoa WTO, Tanzania haikuwa na ujanja ila kukubali. Lakini possibility kubwa ni huenda kikajengwa kibaha au Bagamoyo (not exactly Dar).
Lakini still kuna maswali mengi ya kujiuliza kama kweli hiki ni chuo cha utalii, maana sio rahisi mtu akaamua tu kuizawadia Tanzania kuijengea Chuo hiki, eti Tanzania imeonesha juhudi katika kuvutia watalii. Lakini ukinagalia ukweli wa mambo Kenya,Zimbabwe, Misri na Afrika Kusini zimefanya kzi kubwa zaidi na ya maana zaidi. Sijui ni kwanini Tanzania, na kwanini WTO walisisitiza karibu na Dar es salaam
 
To be exact kwa nini kisijengwe Karatu ambayo ndyo gateway ya kuingia Ngorongoro na Serengeti? Maamuzi mengine jamani!!Dar watu magari machinga tunasongamana. Kila kitu Dar kila Dar. Kunani???
 
The other option, kwanini wasizungumze na Chuo Kikuu cha Arusha na kusaidia kuwa na Kitivo cha Utalii kwenye Chuo hicho..?
 
Siku hizi kuna mkoa mpya wa Manyara..ambapo ni center nzuri tu,na kuna vivutio vingi vya utalii..na vile vile hakuna chuo hata kimoja hata cha ualimu au VTC! sijui kwa nini hawafikirii diversification..
 



Mkuu unajua ndio hivyo omba omba hana la kuchagua. Kama donor ndio wameshaamua hivyo inamaana jamani serikali haina maamuzi ya kupendekeza? Duh sasa hizi ndizo adha za kuzunguka duniani kuomba misaada maana huna sauti nayo. Unajua kama huna ile ownership na mradi wala hauwezi kuwa sustainable na hili ni tatizo la miradhi mingi ya donors haidumu. Sasa jamani kweli wakituambia tukajenge chuo cha ubaharia dodoma tutakubali tuu kwa sababu wao wamesema?


The other option, kwanini wasizungumze na Chuo Kikuu cha Arusha na kusaidia kuwa na Kitivo cha Utalii kwenye Chuo hicho..?


Bwana hii nayo ni option nzuri na wangeenjoy economies of schale ya facilities za chuo cha arusha. Inaweza tuu ikawa kama fucult tuu. Najua chuo cha uhasibu Arusha sasa sio chuo cha uhasibu tena maana wanatoa hadi shahada za computer sayance. Lakini mwanakijiji hapa kuna institutional conflict kwani hiki chuo cha Arusha ni cha Wizara ya fedha, na hiki kipya ni cha wizara ya Utalii.

Siku hizi kuna mkoa mpya wa Manyara..ambapo ni center nzuri tu,na kuna vivutio vingi vya utalii..na vile vile hakuna chuo hata kimoja hata cha ualimu au VTC! sijui kwa nini hawafikirii diversification..


Ni kweli kabisa mzee na hii ingechangia maendeleo ya hayo maeneo sasa wakubwawao kila kitu wanataka bongo maya be kuna kaugonjwa kakupenda bongo na ndio maana serikali imeshindwa kuhamia Dodoma.
 
1. Kiwanda cha kukata Alamasi kilijengwa Iringa kwa sababu za kisiasa- wakati almasi inachichwa Shinyanga- je leo TANCUT Almasi iko wapi?

2. Hiki chuo cha Utalii kijengwe sehemu yenye watalii na vivution vya vya watalii- mimi Dar siungi mko mkono- Arusha, Moshi (hata Zanzibar)- ni ok
 
mshaambiwa ni conditon hiyoo tuliyopewa...so twardui kwenye speed ile ile modern ukoloni!!ardhi yetu lakini twaambiwa cha kufanya with our ardhi n where to build our things..
may b watalii wa kichina waliona utalii dar es salaam si mwaona wengi walivyojaa kariakoo??
 
Jamani hii kitu ndio tulikuwa tunaijadili wenzetu wa Kenya nadhani wana vision kuliko sisi.

 
hivi Kuntakinte, wewe ndiye yule Flana worrior, au ni mwingine. ninapenda sana jina lako, nikikumbuka na vile huyu jamaa alivyokuwa shujaa. it is just a mere jock.

mimi ninaona chuo hiki kisipelekwe dar. hawa watu vipi.?akini?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…