Kwanini hayati Baba wa taifa alikubali mfumo wa vyama vingi licha ya wengi kukataa?

Si kweli kwamba wengi walikataa kwa maana ya kutotaka vyama vingi,bali walitaka vyama vingi bila kujua wanavitaka,kwa mfano wengi walitaka chama kimoja kiendelee lkn wagombea uraisi wawe wawili,sasa huwezi kuwa na chama kimoja lakini kiwe na sera mbili au wagombea wawili,utakua unataka vyama vingi lkn hujijui,,,,,,hii ndiyo nyerere alitumia

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kagera war is the source of all bad things in our country.
Hali ilivyokuwa ngumu nchini baada ya vita ya Kagera ndipo Nyerere akaamua awatii Imperialists na sera zao.
 
Ni wananchi wote walihojiwa au ilikuwa ni sample ya wanaccm?
Hapo sasa! Ukweli mabadiliko tunayo yaona sasa ni kwa sababu ya vyama vingi vya siasa vinavyoleta changamoto kwa watawala,na kuwasukuma wafanye kazi pasipo wao kupenda,nasikitika kuona vyama vya upinzani vinapigwa vita,hii itarudisha nyuma uwajibikaji wa watawala,na hivyo maendeleo kuyasikia kwa wengine.mfano tunashuhudia bungeni wabunge wa chama tawala wamekuwa wa kila kitu ndiooooi,na kupiga meza,hatimaye wakajikuta wanapitisha mikataba mibovu ya madini na kuitia serikali umasikini.Na kama bunge lingekosa wabunge wanaotoka vyama vingine vya upinzani tusingeshuhudia Leo hii hatua wanazochukua watawala katika utekelezaji majukumu.Mimi naweza kuwaita wapinzani ni kama"CATALYST" ya maendeleo ya nchi hii.
 
Wingi wa kura si hoja! Hii siri wapinzani hawajaijua japo ndo msingi ulioanzisha upinzani nchini.
 
Hapo sasa! Ukweli mabadiliko tunayo yaona sasa ni kwa sababu ya vyama vingi vya siasa vinavyoleta changamoto kwa watawala,na kuwasukuma wafanye kazi pasipo wao kupenda,nasikitika kuona vyama vya upinzani vinapigwa vita,hii itarudisha nyuma uwajibikaji wa watawala,na hivyo maendeleo kuyasikia kwa wengine.mfano tunashuhudia bungeni wabunge wa chama tawala wamekuwa wa kila kitu ndiooooi,na kupiga meza,hatimaye wakajikuta wanapitisha mikataba mibovu ya madini na kuitia serikali umasikini.Na kama bunge lingekosa wabunge wanaotoka vyama vingine vya upinzani tusingeshuhudia Leo hii hatua wanazochukua watawala ktk utekelezaji majukumu.
CCM ni wapuuzi mkuu
 
Nakumbuka enzi hizo nilikuwa kidato cha tano wakati tume ya jaji Francis nyalali ilipokuwa inapita kukusanya maoni.nilishiriki kwenye mkutano wa hadhara wilayani worth ambapo yeyote aliyejulikana anauelewa kidogo au busara aliombwa kuchangia.Nilisikiliza hoja za wazee waliopanda jukwaani na kutoa yao ya moyoni.Asilimia 99 walipendekeza Mfumo wa Chama kimoja uendelee.Kwamba upinzani ni vita.Lkn matokeo yake mwl.Nyerere alisema ni lazima mfumo wetu ubadilike hata kama wengi wamepinga.Sababu aliyoitoa ni kwanza uelewa duni wa Watanzania juu ya mageuzi na pia huwezi kwenda kinyume na matakwa ya ulimwengu wa sasa.Nina imani kama hayati baba wa taifa angekuwapo leo tungekuwa na katiba mpya tena ile ya Warioba na siyo ile iliyochakachuliwa na ccm.Ccm ni walewale!
 
Nakumbuka enzi hizo nilikuwa kidato cha tano wakati tume ya jaji Francis nyalali ilipokuwa inapita kukusanya maoni.nilishiriki kwenye mkutano wa hadhara wilayani worth ambapo yeyote aliyejulikana anauelewa kidogo au busara aliombwa kuchangia.Nilisikiliza hoja za wazee waliopanda jukwaani na kutoa yao ya moyoni.Asilimia 99 walipendekeza Mfumo wa Chama kimoja uendelee.Kwamba upinzani ni vita.Lkn matokeo yake mwl.Nyerere alisema ni lazima mfumo wetu ubadilike hata kama wengi wamepinga.Sababu aliyoitoa ni kwanza uelewa duni wa Watanzania juu ya mageuzi na pia huwezi kwenda kinyume na matakwa ya ulimwengu wa sasa.Nina imani kama hayati baba wa taifa angekuwapo leo tungekuwa na katiba mpya tena ile ya Warioba na siyo ile iliyochakachuliwa na ccm.Ccm ni walewale!
Hahahahaha! Tatizo elimu ilikuwa ndogo kwa walio wengi,nakumbuka mwaka 2010 nilikutana na binamu yangu mmoja hivi, shule imempiga chenga, akaniambia kuwa wameambiwa na viongozi wa CCM kuwa vikishinda vyama vingine nje ya CCM basi nchi itatokea vita,hivyo wachague CCM,na kweli somo lilikuwa limemkolea sana.na tayari ulikuwa humuelezi kitu kuhusu sijui CUF,sijui CHADEMA,hivyo mtu kama huyu ukimsimamisha lazima aseme uwe mfumo wa chama kimoja tu.bila Ku "reasoning"wala nini?
 
Tatizo la hii nchi ni CCM .
Mwalimu aligundua Tatizo akaamua kung'atuka na kukaa pembeni.
Akatamani vije vyama vingine viweze kuondoa tatizo au hata kusaidia kuokoa jahazi.

Mwalimu alionana mbali sana.
Hata uchaguzi wa mwaka 2015 jina CCM halikuingia kwenye kinyang'anyiro. Mgombea wa chama hicho alijua tatizo akaamua kutumia uwezo na mbinu na jina binafsi ili kupunguza tatizo na akafanikiwa kujipatia ushindi mnono.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni kweli Mwinyi ndiyo alikuwa madarakani lkn wakati huo Nyerere alikuwa bado alikuwa na sauti ya mwisho ktk mambo mengi.Yeye ndo aliyetoa hoja zilizopelekea mfumo kubadilishwa la sivyo kama ingekuwa wengi wape basi asilimia 80 ya watu wote walitaka chama kimoja.baada ya Mwl Nyerere kuongea akaua hoja zote za awali kama ilivyokuwa kawaida yake.Ni sahihi kusema bila yeye mfumo usingebadilika.Mzee Mwinyi kama walivyo viongozi wengine wa ccm hawana ubavu wa kukataa asilimia 80 ya watu wao.
 
Huu mfumo ulishaanza kujadiliwa kitambo back 1992 sasa ikabidi wananchi washirikishwe...kilichotokea ni kwamba wananchi wengi hawakuridhia kwa kile wengi walihisi mfumo wa vyama vingi uachochea vita na watz niwaoga wavita..ukitilia maanani ile 1994 ndo vita vya kimbari vya Rwanda vilikuwa vimeshamiri na wakimbizi walikuwa wengi sana kila kona so wananchi kuhofia hilo lisijekuwatokea wakakataa huo mfumo.
 
Back
Top Bottom