Kwanini haya yanafanyika Zanzibar?

kwanza kabisaa acha upotoshaji 🐒

pili, malalamiko ni yako binafsi usisingizie chini kwa chini 🐒

hakikisha una vigezo stahiki tajika sio siasa unazo jaribu kuziingiza kwenye masuala nyeti na muhimu sana kwa maslahi mapana ya usawa na haki SUK na JMT..

Pili ya Mungu ana panga na kuratibu Mungu mwenyewe kwa wakati wake muafa, na wala hakawii wala kuchelewa kuitimiza ahadi yake kwa kila mja wake....
 
Ndio kwa vile CCM wanatawala kule ,ile Zanzibar ona vile kuna jamii hat kazi hawapati wamebaki kuvua hata wasome kwa sababu ya mfumo wa CCM .
Ni mfumo mbaya wa kibaguzi, mapinduzi yalifanyika miongoni mwa mambo ilikuwa ni wa Africa wana wa nchi Zanzibar kubanguliwa kwenye huduma mbalimbali ikiwemo elimu, leo hii umepindua unaendeleza yale yale ya mkoloni.
 
Upotoshaji upi?

Una uhakika gani kwamba ni malamiko yangu binafsi?

Uko wapi usawa kwenye kuajili hasa kipindi hiki cha vijana kuajiliwa kwenye vikosi?

Fanya research japo dogo juu ya wanaochwa,
Au wewe ni miongoni mwao hao wenye kuhakikisha hadi uwe mwanachama, uwe na kadi ya chama, uwe kwenye data ya chama uvccm?
 
Lakini tu kwa sababu, hana kadi ya umoja wa vijana wa chama na kwenye system ya chama jina lake halionekani basi kijana huyu au vijana hawa majina yao yanaenguliwa kuweza kuendelea na michakato inayofua.
Je mlio madarakani kwa nini mnafanya hivi?
kumbe inshu ipo serious, kuna mtu aliniambia ameenda azam marine kutuma kadi ya chama iende zanzibar.
ila mtoa mada usijeeneza uvumi kama hauna taarifa za kweli, chonde chonde.
 
unaendelea kukiri kwamba hayo ni manunguniko yako binafsi 🐒

hakuna haja ya utafiti,sababu utaratibu wa usahili mpaka selection uko wazi na huru sana..

una vigezo stahiki huwezi achwa, ikiwa huna vigezo check fursa nyingine ndugu, hamna haja ya kubabaika kwasabb vigezo haviwez kubadilika kwasabb yako 🐒

huwezi toboa ukianza kusingizia vyama hali yakua vigezo vimekutupa mkono 🤣


upotoshaji na kutafuta huruma havina maana yeyote 🐒
 
Mimi nawashauri vijana wote chukueni kadi za ccm. Najua wengi ni kama mimi- kadi au vazi la ccm linaniletea kinyaa, ila we ichukue iweke mahali ambapo hutaiona mara kwa mara. Ukisikia issue yoyote ambayo kuna dalili ya upendeleo kwa wanaccm, ibukanayo. Lakini moyoni una msimamo wako thabiti wa kisiasa, na kwenye chaguzi kura zako zielekeze pale moyo wako unapenda.
 
Mkuu unataka sema kwa sasa kuna dhambi mpya ya uchawa [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Kuna watu watakubishia tuu au watadai ushahidi, lakini hii kitu kama haija kukuta huwezi kuamini labda akuambie mtu wako wa karibu sana.
Nishawahi ulizwa hili swali, "UNA KADI YA CHAMA" [emoji15][emoji15] sikutegemea mazingira kama yale kuulizwa vile. Nkamwambia sina. Kitambulisho cha "MZANZIBARI MKAAZI" je? Sina. Nna "NIDA" na "CHA KUPIGIA KURA", eti aah.. sasa kile si cha "BARA" nkaishiwa pozi..
 
Wana mbinu zao za kukutumia na hata kujiridhisha,
 
Na hawajifichi, mtu yupo kwenye usafiri wa public anaongea wazi wazi kabisa kwamba "hata uwe na connection na mtu mkubwa wa serikalini au kwenye taasisi akutengenezee connection ya kazi, kama huna kadi ya chama na haupo kwenye system makao makuu Zanzibar ya uvccm au Chamani Kisiwadui jina lako litakosa sifa litatupwa kule"
 
Eeh..

Samahani, kazi ilikua inahusiana na kitu gani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…