Emanueli misalaba
JF-Expert Member
- Dec 12, 2016
- 2,930
- 4,004
Ukichunguza ki undani wengi wanaofunga Kwaresma au Ramadhani, wanafunga ni kama wanajishindisha njaa tu, maana matendo yao hayaendani na wanachokifanya., Ubaguzi, unafiki, u chawa, uzinzi, ufirauni n.k yote haya huwa wanasitisha kwa muda tu baada ya mwezi kuisha wanarudia yale yale.Wana Jf bila shaka mpo salama,
Hongereni kwa majukumu ya kutwa zima ya ujenzi wa uchumi mtu mmoja mmoja, Familia na Taifa,
Bila kuwachosha nijielekeze kwenye hoja yangu,
ala tano, je dhamiri zenu zinawashuhudiaje juu ya hili na Mungu mnayemwabudu anawaangalije juu ya hili?
Hata mimi ningewakata vijana wanaoandika kuajiliwa badara ya kuajiriwa.Wana Jf bila shaka mpo salama,
swala tano, je dhamiri zenu zinawashuhudiaje juu ya hili na Mungu mnayemwabudu anawaangalije juu ya hili?
Unataka ushahidi wa namna ipi?Leta ushahidi.
Mkuu Citizen_37 je na nchi za wenzetu mfano za ulaya hasa Waliotutawala nao wana ubanguzi kama huu kwa raia wao ambao yamkini hawana vyama wako neutral?Ukichunguza ki undani wengi wanaofunga Kwaresma au Ramadhani, wanafunga ni kama wanajishindisha njaa tu, maana matendo yao hayaendani na wanachokifanya., Ubaguzi, unafiki, u chawa, uzinzi, ufirauni n.k yote haya huwa wanasitisha kwa muda tu baada ya mwezi kuisha wanarudia yale yale.
Mkuu Accumen Mo nadhani hujaelewa maswali yangu kiongozokiongozi, hao hao ccm ili uajiliwe inaonyesha uwe upo kwenye system ya uvccm au kwenye system ya chama Kisiwadui.Kama ungelikuwa unajua Zanzibar hawaitaki hiyo CCM hata Mwinyi usingeongea ,kuwepo kwa CCM zenji ni swa na ukoloni mamboleo yaani chama cha bara kitawale zenji..
Haya yote ni laana ya CCM.
Sana kiongozi inasikitisha Sana.Inasikitisha sana
Ndio kwa vile CCM wanatawala kule ,ile Zanzibar ona vile kuna jamii hat kazi hawapati wamebaki kuvua hata wasome kwa sababu ya mfumo wa CCM .Mkuu Accumen Mo nadhani hujaelewa maswali yangu kiongozo, hao hao ccm ili uajiliwe inaonyesha uwe upo kwenye system ya uvccm au kwenye system ya chama Kisiwadui.
Mimi sijaomba kuajiliwa, ila malalamiko kwa vijana ni mengi kuhusiana na kubanguliwa kisa hawajulikani kwa naibu katibu mkuu uvccm Zanzibar.Braza ukiona hukuchaguliwa ulishindwa interview hamuwezi ajiriwa wote.
Ni kweli mwisho wa siku unakutana na watu wameajiliwa baadhi yao vingezo hawana, huduma zao mbovu, rushwa nk nk.Ndio kwa vile CCM wanatawala kule ,ile Zanzibar ona vile kuna jamii hat kazi hawapati wamebaki kuvua hata wasome kwa sababu ya mfumo wa CCM .
Ni kweli mwisho wa siku unakutana na watu wameajiliwa baadhi yao vingezo hawana, huduma zao mbovu, rushwa nk nk.
Ushahidi gani unataka? Serikali haiwezi kuajiri Hizbu.Leta ushahidi.
Wale wazenji japo wachache kuna jamaa hawapati ajira ng'o kwa sababu hawataki CCM
Zanzibar itakombolewa tuWana Jf bila shaka mpo salama,
Hongereni kwa majukumu ya kutwa zima ya ujenzi wa uchumi mtu mmoja mmoja, Familia na Taifa,
Bila kuwachosha nijielekeze kwenye hoja yangu,
Kwa Zanzibar unakuta kuna malalamiko sana chini kwa chini hasa linapokuja swala la kuajiliwa kwenye taasisi za serikali na hata kwenye vikosi mbali mbali za majeshi, Jku, Kmkm, Valatia nk.
1. Unakuta vijana wana sifa zote za kuajiliwa, elimu wako vizuri.
2. Ni raia halali wa nchi.
3. Vipimo vya afya vinaonyesha wako fit.
4. Vitambulisho vyote wanavyo nk.
Lakini tu kwa sababu yeye si mwanachama wa chama Fulani, hana kadi ya umoja wa vijana wa chama na kwenye system ya chama jina lake halionekani basi kijana huyu au vijana hawa majina yao yanaenguliwa kuweza kuendelea na michakato inayofua.
Je mlio madarakani kwa nini mnafanya hivi?
Hawa mnaowaweka kando kisa tu si wanachama mnakuwa mpo sahihi kwa kiasi gani?
Hawa vijana ni raia wa nchi yenu wanazo haki zote za kikatiba juu ya nchi yao ikiwemo kulitumikia taifa lao kwenye nyanja mbali mbali.
Leo hii kwenye baadhi ya taasisi mfano Hospital ya Mnazi Mmoja, baadhi yao wameajiliwa hawana vigenzo lakini tu kwa sababu ni wanachama wa chama chenu wametumika kupiga kura 2015 au 2020 wanapata upendeleo wa kuajiliwa, mwisho wa siku ukienda Mnazi Mmoja hospital unakutana na baadhi ya watoa huduma wenye kauli mbovu kwa wateja, wavivu wa kazi, watoro wachelewaji hawana weledi na kazi zao, hawana ubunifu, wenye sifa wengi wao mnawatupa nje ya mfumo.
Je, mnajenga taifa la namna gani?
Je, Tanzania bara nako haya hayapo maana chama ni hicho hicho?
Watanzania wengi tunajinasibu wacha Mungu kupitia dini zetu, Uislamu, Ukristo nk je dini zetu zinaruhusu ubaguzi?
Kubangua watu kwa sababu ya chama kwenye ucha Mungu ruksa?
Ikifika Kwaresima, Ramadhani full kufunga, swala tano, je dhamiri zenu zinawashuhudiaje juu ya hili na Mungu mnayemwabudu anawaangalije juu ya hili?
Mkuu Erythrocyte lini itakombolewa?Zanzibar itakombolewa tu