KWANINI HATUZALISHI GESI YETU?

KWANINI HATUZALISHI GESI YETU?

The redemeer

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2025
Posts
4,780
Reaction score
8,155
----------------------------------

Tanzania ina visima vya gesi asilia kama vile:
👉 Songosongo
👉 Mnazi Bay

Ajabu ni kuwa bado Hatuwezi kuzalisha gesi yetu ya majumbani (Liquified Petroleum Gas). Badala yake tumekuwa waagizaji wakubwa wa gesi kutoka Mataifa kama vile UAE, kenya, India n.k.

MBONA HATUTUMII GESI YETU?

Gesi inayozalishwa hapa Tanzania ni CNG ( Compressed Natural Gas), na sio LPG (Liquified Petroleum Gas).

📌 Compressed Natural Gas na Liquified Petroleum Gas (CNG na LPG ) ni gesi tofauti kabisa kwa muundo wa kemikali, haiwezekani kubadili CNG kuwa LPG kirahisi kwa sababu ni gesi mbili tofauti kabisa.

👉CNG huwa ni Methane (CH4)
👉LPG huwa ni propane ( C3H8)

📌CNG (methane) haiwezi kubadilishwa kuwa LPG (propane/butane) kwa njia ya kawaida au ya kibiashara. Ni gesi mbili tofauti kabisa kwa muundo na matumizi. Gesi ya Tanzania haina mchanganyiko unaoweza kutoa LPG moja kwa moja, na hakuna kiwanda kinachoweza kubadilisha methane kuwa LPG.

KWANI HII GESI TUNAYOTUMIA MAJUMBANI HUTOKANA NA NINI?

Ukweli ni kuwa Mataifa yanayoagiza LPG kama Oryx, Mihan n.k., huchukua hiyo gesi kutoka Nchi zinazochakata mafuta (refineries), Ambapo LPG inapatikana kwa urahisi kama bidhaa ya pembeni (byproduct) wakati wa usindikaji wa mafuta.

Kumbe basi wao huwa tayari wana propane tayari — si methane (CNG) kama ilivyo kwetu Tanzania.

Kwa lugha rahisi kuweza kueleweka ni kuwa, Gesi ya majumbani hutokana na uchakatwaji wa Mafuta asili Na si uchakatwaji wa gesi asili.

LAKINI MBONA TUNA VISIMA VYA MAFUTA HAPA NCHINI?

Ujuwe Tanzania ina visima vya mafuta.

Visima hivi viko hasa maeneo ya
Ziwa Tanganyika (Katavi, Kigoma, na maeneo ya Ziwa Eyasi na Eyasi Wembere Basin).
Lakini ajabu ni kuwa:

👉hata mafuta hatujaanza kuchakata.

👉 Hakuna refinery (kiwanda cha kusafisha mafuta) nchini

Ukiuliza, utaskia mwamba mmoja akijibu:

⏩Kujenga refinery ni gharama kubwa sana. Inahitaji zaidi ya USD milioni 500 hadi bilioni 1, kulingana na ukubwa na teknolojia.

⏩LPG inatokana na usindikaji wa mafuta ya kiwango kikubwa sana.
Unahitaji kiwango kikubwa sana cha mafuta ghafi ili upate hata kiasi kidogo cha LPG.

KWA HIYO TUSEME
TANZANIA HAINA MAFUTA YA KUTOSHA KUJENGA REFINERY?

Unaskia mwamba kutoka kijani akijibu tena na bass nzito nzito:
Tanzania ina mafuta lakini hayatoshi kwa kiwango cha kibiashara cha uzalishaji wa mafuta na bidhaa zake (kama LPG, dizeli, petroli).

Lakini swali linakuja:

Tanzania ina kiwango kidogo cha Mafuta ama ina kiwango kidogo cha nguvu ya utafiti juu ya mafuta?

Nasema hivi kwasababu:

🎯 Taasisi na makampuni ya utafiti wa mafuta nchini Tanzania ni wachache sana, na wengi wao wamepunguza kasi au kujiondoa kabisa kutokana na changamoto nyingi.

🎯Technology inayotumika katika utafiti wa mafuta bado ni duni. TPDC (Tanzania Petroleum Development Corporation) taasisi ya serikali inayosimamia na kuendeleza sekta ya mafuta na gesi nchini haina uwezo wa kifedha wala teknolojia kufanya utafiti wa kina peke yake bila ubia na wawekezaji

Kuna uwezekano mkubwa wa kuwepo kwa mafuta zaidi nchini, lakini hayajachunguzwa vya kutosha

Eneo la Tanzania lina mabonde ya kijiolojia (basins) ambayo kihistoria huashiria uwepo wa mafuta, kama:

👉Rufiji Basin

👉Selous Basin

👉Mandawa Basin

👉Eyasi-Wembere Basin

👉Ziwa Tanganyika Basin

Haya ni maeneo ambayo kijiolojia yanafanana na maeneo yenye mafuta mengi duniani (kama Sudan, Angola, Nigeria).

✅ Hii inamaanisha: mafuta yanaweza kuwepo kwa wingi, lakini hatujayatafuta vya kutosha.

Kwa hiyo tusemeje hapa?
Naoendekeza tuseme hivi:
📌Tanzania haina uhakika wa kuwa na mafuta kidogo — bali ina kiwango KIDOGO CHA UTAFITI na UCHIMBAJI.

NINI KIFANYIKE?

wachumia Tumbo wa kijani waachie ngazi vijana tushike nchi tufaidike na Rasilimali zetu.. Tafiti zifanyike, Viwanda vifunguliwe, bei za bidhaa zishuke, kodi za kishenzi zifutwe, wanunuzi kutoka nje wapatikane, uchumi upande na mwisho kabisa Tanzania tusiwe wanunuzi kutoka nje, bali tuwe wauzaji kwenda nje.
 
Hatukulipa hata ndururu kwenye utafiti hivyo hiyo gesi sio yetu mpaka tutakapomaliza kulipa deni la utafiti.. Kikubwa tuoneshwe mkataba
 
Wenye taaluma zao hapa washushe nondo.
Following.....
 
Utafiti wa mafuta tulianza kabla ya nchi jirani,lakini wenzetu wameanza kuchimba kabla yetu!,kwa aibu kubwa bomba litapitishwa nchini mwetu.

Bonde la ufa katika nchi jirani kuna mafuta,lakini kwetu mkondo huo huo hakuna mafuta.

Baharini mkondo wenye mafuta unatuletea sintofahamu,lakini wenzetu wamekubali kutangaza na kuingia mikataba na makampuni ya uzalishaji.

Tanzania kuna kitu hakipo sawa!
 
Gesi zote za kupikia utoka nje ya nchi kwa sababu utokana na mafuta na sio gesi.
Kuna mafuta na kuna gesi.
Umesoma shule gani? Gesi nje wanaivuna na kuichanganya na mafuta ,ili iwe LPG (liquefied petroleum gas ),ni ile gas ya asili hakuna mpya ..Kuna sababu nyingi ili moja wapo iweze kusafirishwa na kuwa na ufanisi ( in terms ya kuwa na density kubwa,kuweza kuigandamizi ili kuziweka molecules zake pamoja) ..Gas inakuwa compressed kuipa ufanisi wa nguvu zaidi kwa molecules zake kuwa pamoja ,iko too loose kama hewa au kuwa rahisi kusafirishwa.

Topic ya ile ya pressure inakuwa majibu yote.

Watanzania hatuwezi kufanya hizo process ,ni sawa na kusema kufanya packaging ya Gas...Wasomi wapo hapa wanajiingiza kwenye siasa , wenyewe wanasema siasa ni maisha.
 
Umesoma shule gani? Gesi nje wanaivuna na kuichanganya na mafuta ,ili iwe LPG (liquefied petroleum gas ),ni ile gas ya asili hakuna mpya ..Kuna sababu nyingi ili moja wapo iweze kusafirishwa na kuwa na ufanisi ( in terms ya kuwa na density kubwa,kuweza kuigandamizi ili kuziweka molecules zake pamoja) ..Gas inakuwa compressed kuipa ufanisi wa nguvu zaidi kwa molecules zake kuwa pamoja ,iko too loose kama hewa au kuwa rahisi kusafirishwa.

Watanzania hatuwezi kufanya hizo process ,ni sawa na kusema kufanya packaging ya Gas...Wasomi wapo hapa wanajiingiza kwenye siasa , wenyewe wanasema siasa ni maisha.
Siasa ndio biashara ya shortcut inayolipa sana
 
Back
Top Bottom