Kwanini hakuna picha ya mtume wetu Muhammad (SAW)

USSR

JF-Expert Member
Jul 15, 2015
5,098
2,000
Nafahamu alizaliwa Macca akakuzwa na wazazi wake akasoma na kuishi kama wanadamu wengine mpaka umauti ulipomfika akazikwa kama nabii na mtume.

Amekuwa mtu maarufu sana tangu mtoto kwa nini hawakumchora picha ya kumbukizi ili vizazi vijavyo vimuone ndio kwa nini hakuna picha.

Walimfahamu dada zake, kaka zake, wajomba na mashangazi hata rika lake alilokuwa nalo kwanini hata kwa maelezo asichorwe tu, kwa nini inakatazwa na tunaambiwa yeye alikuwa mtu wa watu na mnyenyekevu, alipendwa?

Je watoto/wajukuu hawajui baba/babu alikuwa anafananaje ili watunze kumbukumbu kwa nini hakuna picha hata ya kuchora?

Manabii na mitume wote tunaziona picha zao za kuchorwa ila sio huyu mwamba wa miamba Mohammed SAW kwa nini?

USSR

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom