Kwanini Dr Ndalichako asijiuzuru?

Status
Not open for further replies.
Kwa taarifa yako Mwalimu wangu Dr. Ndalichako ameleta mabadiliko makubwa sana katika Baraza la Mitihani. Jambo kubwa kabisa alilolifanya ni kuziba mianya ya wizi wa mitihani. Kumbuka kabla Dr. Ndalichako hajaingia baraza la Mitihani mitihani ilikuwa ikiuzwa kama njugu lakini kwa sasa wizi wa mitihani haupo tena. Bado tunawahiaji sana Wazalendo kama Dr. Ndalichako. Huwezi kumhukumu Dr. Ndalichako kwa tatizo la kiufundi ambalo linaweza kumtokea MTU yeyote unless ndugu yako barubaru unaagenda nyingine. Wazalendo katika nchi hii ni wachache na DR. Ndalichako ni mmoja wao. Tumhukumu kwa haki. Mimi nasema hivi bado tunamuhitaji na hakuna sababu ya msingi ya yeye kujiuzulu.
 
Hakuna sababu ya kujiuzulu!
 
Hivi Kwanini Sheikh yule asiye na Msikiti ana asiye Mtanzania Alhaji Ponda Issa Ponda asigombee uraisi ? Maana wafuasi wake wako wengi Tanzania......
Wa kumshangaa ni yule anayehoji kuhusu mtu kuitwa au kuwa Sheikh bila ya Msikiti (wa kuongoza)!
Anayewaongoza Waislamu Msikitini katika swala zao tano za kila siku huitwa Imaam! sio Sheikh. Imaam kiujumla ni Muislamu yoyote yule aliyebalehe anaweza kuwa Imam na sio lazima awe Sheikh.

Halafu tuna Muadhini (si lazima awe Sheikh) ,"Daiyah" mwenye kuita watu katika Uislamu(si lazima awe Sheikh) n.k.

Kosa la kuchanganya Usheikh na Uimamu au Muadhini au Daiyah ninaweza kulielewa kama litafanywa na John, Joyce au Joseph...Lakini mtu mwenye kudai kuwa na ilmu halafu kuangukia kaika kosa kama hili?! mhh.
 

wewe ndo hujui ki2 unakurupuka 2 @ madudu cjui matope??
Tatizo lako hujui maana ya kiongozi bora na muwajibikaji.
Kwa kifupi ngoja nikusaidie.
Kiongozi bora ni yule anayekubali kuwajibika endapo tatizo likitokea kwenye kitengo chake ili aipe uhuru tume itayoundwa kumchunguza.
Hichi ndicho wanachokikosa viongozi wengi humu nchini kwa kuwa ving'ang'anizi pale wanapofanya makosa au kuhisiwa.
Chukua mfn uliotokea miezi kadhaa iliyopita Barclays na sehemu nyingi 2 hapa Duniani.
Daima ntampongeza Lowasa kwani alifanya kitendo cha kishujaa sana. Badilika ndg sio kuwakumbatia viongozi wasio waadilifu ktk kazi zao. Kuachia ngazi ukiharibu kazi ni muhimu kwa taifa hili lililojaa viongozi wasio waadilifu.
 
Kwanini Dr Shukuru Kawambwa asijiuzulu ?.

Haitakuwa busara kwa Dr Shukuru Kawambwa kujiuzulu kwa sababu HILI BARAZA LA MITIHANI ni entity yenye sura ya Muungano.

Ukirejea kwenye Article of Union utaona Wizara ya Elimu ya Dr kawambwa inafanya kazi mpaka kigamboni kwani kuna Wizara kama hiyo huko Zanzibar lakin Baraza la mitihani la Taifa lipo moja tu.

Ndio maana nikabainisha wazi Baraza hilo lina sura ya Muungano na nikabainisha wazi kuwa ili sura hiyo iwe wazi ni lazima uwekwe utaratibu ule wenye sura ya Muungano kama zilivyo wizara za muungano au mashirika na taasisi za Muungano kama ilivyo BOT.

Kwa msingi huo Katibu Mtendaji mkuu wa Baraza hili ndio wa mwisho kimamlaka na Kauli ya naibu waziri wa Elimu (Muungano) haina nafasi Znz kwani nako kuna waziri pia.

kama una ziada mkuu ongezea hapa.

 
Leo nimekumbuka maneno ya Rais Kikwete pale aliposema kuwa kuna baadhi ya wakurugenzi na watendaji wake wanafanya madudu kwa makusudi ili waziri husika aadabishwe, kwahiyo huyu mama ni mmoja wapo, ni vema nae akawajibishwa!
 
Leo nimekumbuka maneno ya Rais Kikwete pale aliposema kuwa kuna baadhi ya wakurugenzi na watendaji wake wanafanya madudu kwa makusudi ili waziri husika aadabishwe, kwahiyo huyu mama ni mmoja wapo, ni vema nae akawajibishwa!

Kwa hiyo wewe unamwamini sana Kikwete?
 

Nikuulize kitu kimoja mkuu, kwanini ilipozama meli zanzibar Mv SKAGIT aliewajibika ni waziri? kwani yeye ndie alikuwa anaendesha meli ile? jibu lake ni kwasababu yeye ndio mtendaji wa mwisho katika wizara ile, kwa upande wa visiwani, sasa leo limetokea hili NECTA ndalinacho pia anatakiwa kujiuzuru
 
Ndalichako sio politicians ni mtendaji,mbona mnazunguka why not shukuru kawambwa waziri au kwa sababu anatoka bagamoyo????
 

unatakiwe uwe great thinker ndugu, basi kwa mantiki usemayo ya viongozi wa juu kuwa wakristo, yale ya sensa na kipengele cha udini yangewekwa.
 

Mkuu, hata kipindi cha Ndalichako mitihani iliwahi kuibiwa kwa kiwango cha juu, hata akatakiwa kujiuzulu. Alifanya press conference kukataa kujiuzulu. Mimi si support kujiuzulu kwa Ndalichako kwa hili la mitihani ya Islamic knowledge lakini si sawa kumuita ni mzalendo wa kweli. Angekuwa mzalendo wa kweli angejiuzulu mitihani ilipoibiwa baada ya kutoka Dr. Nkumbi.
 

Mkuu nakuunga mkono, hata hivyo haiwezi tu kuishia kwa Dr.Ndalichako kujiuzulu,lazima twende zaidi ya hapo. Kuna uzi nimepost kwenye jukwaa la siasa-moved to Jukwaa la Elimu na sasa topic Closed.[h=2](NECTA na matokeo batili ya mtihani somo la Islamic Knowledge!)[/h]Hii ndio Tanzania yetu na Religious Inbalance!
 
Nimependa hiyo ya Ponda

Halafu, hlili swala la mtihani wa dini kuwekwa ktk baraza la taifa... WHY , si watu waazishe mabaraza yao ya kidini, watoe mitihani yao.

Why kutumia pesa zetu, kugharimia mitihani ya KIDINI????
 
sasa kwa kuwa sasa umepata somo, na kuelewa kwanini, heading yako haikuwa hivyo kwamba waziri wa elimu na mkurugenzi wa Necta wajiuzuru au kufutwa kazi?
mbona hao makafir bila kujali itikadi zao kwnye suala la Daudi Mwangosi wamesema wazi wazi bila kuficha kitu kwamba nchimbi , mwema na kamuhanda waondoke bila kujali huyu ni muungwana na yule ni kafiri. ukiweka vitu vyako namna hii unakuwa objective na sio subjective, halafu hili la kusema murugenzi akitoka upande huu, naibu upande huu, je ratio ya upande huu na huu ipoje? maana ukiwa msomi mambo yako lazima yawe ya kisomi somi.
 

acha uzuzu wewe soma kwanza.
 
kwa hiyo necta itakuwa chini ya wizra gani? ya muungano iliyo chini ya ofisi ya makamu wa raisi? basi huyo waziri ajiuzulu, maana hakuna chombo chote tanzania hii kisicho chini ya wizara fulani?
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…