Setfree
JF-Expert Member
- Dec 25, 2024
- 5,527
- 7,121
Siku hizi kuna dhambi nyingi zilizopachikwa majina mazuri au ya kisasa. Kwanini? Hii ni hila ya shetani ya kuzipunguzia uzito au kuzipa uhalali katika jamii. Kwa njia hiyo shetani anawafanya watu waone kuwa dhambi ni kitu cha kawaida, cha kuvutia, au cha kupendeza na hivyo wanavutwa kutenda dhambi bila kuona haja ya kutubu. Hatimaye waangamie milele bila kujua.
Hizi hapa ni baadhi ya dhambi zilizopewa majina mazuri ya "kistaarabu" au "ya kisasa" kiasi kwamba wanaozifanya badala ya kujuta wanazifurahia:
1. Uzinzi/Zinaa → “Mapenzi/Mahusiano"
Uzinzi umepachikwa jina jipya kuwa ni mahusiano ya kimapenzi. Hata hivyo majina hayo mapya hayaufanyi uzinzi kuwa halali. Amri ya Mungu iko palepale: usizini(Kutoka 20:14) na wazinzi hawataurithi ufalme wa Mungu.
2. Kutoa mimba(kuua) → “Afya ya uzazi”
Kutoa mimba hujulikana kama afya ya uzazi au uhuru wa mwanamke, lakini ni kuua uhai usio na hatia. Amri ya Mungu ya usiue (Kutoka 20:13) haiwezi kubadilishwa na jina hilo jipya.
3. Ushoga na usagaji → “Mapenzi ya jinsia moja”/“Orientation”
Uovu huu unaofanywa kinyume na maumbile unajulikana sana kama love is love. Mashoga Mungu anawaona. Tubuni uovu wenu (Warumi 1:26–27)
4. Ulevi → “Kunywa kilauri”/“Kupiga Tungi"/"Ku-chill”
Ulevi umepewa majina yanayokifanya kilevi kionekane kuwa ni burudani, kumbe ni dhambi itakayowapeleka watu wengi jehanam (1 Wakorintho 6:9–10)
5. Uongo → “Chai"/"Kupiga Kiswahili”
Uongo huonekana kama maneno ya hekima ya kujiokoa katika hatari, lakini ni mtego unaowanasa watu dhambini.(Ufunuo 21:8)
6. Wizi → “Kupiga dili”/“Kusogeza”
Mtu anajua kuiba ni dhambi lakini anasema anachukua chake mapema (Kutoka 20:15)
7. Uchawi → “Nguvu za asili”
Mtu anamloga mwenzake lakini anasema amempiga matukio! (Kumbukumbu 18:10–12)
8. Kiburi → “Kuji-brand”/“Self-confidence”
Kiburi hufichwa katika jina la kujiamini, lakini ni chanzo cha anguko (Luka 14:11)
9. Usengenyaji na fitina → “Udaku”/“Kupiga mdomo”
Kumchafua mtu kwa ulimi, kumebatizwa kuwa ni kupiga story (Wagalatia 5:19–21)
“Ole wao wausemao uovu kuwa mema...” (Isaya 5:20)
Shetani ana hila nyingi. Anawashawishi watu wazivalishe dhambi suti, ili waendelee kuzivaa na kujiona kuwa wako safi kumbe dhambi hizo zinawapeleka upotevuni.
Dhambi ni dhambi. Let us call a spade a spade. Ukiita pombe "kinywaji" bado ni sumu tu, itakuua. Ukiuita uzinzi “mapenzi,” bado tu unavunja amri ya Mungu.
Tushtuke kiroho. Tusikubali dhamiri zetu zipumbazwe na majina mapya ya dhambi. Tuitaje dhambi kwa jina lake halisi, ili tuikimbie na kutubu, tusamehewe.