Kwanini Chawa wengi siku hizi wanakula mihogo Coco Beach? Ni ugumu wa maisha au mihogo inaongeza uwezo wakujipendekeza?

Resilience

JF-Expert Member
Jan 4, 2023
876
4,101
Wasanii wengi wasio na fruiful content wanakesha Coco beach kula mihogo. Akaunti zao utazitambua kwa picha na clips za kusifia hata pasipohitaji kusifia.

Naamini mmiliki wa Chimbo la mihogo hana uwezo wa kiuchumi kuwalipa wasanii hawa kwa wingi wao. Ni aidha wanatumia jina lake kujibrand au yeye anawatumia kujitangaza bila wao kujua au wana punguzo.

Chawa hawa wameanza kuegemea kuijadili siasa na uchumi wa nchi. Lakini wao kama wao sidhani kama wamejipata kiasi cha kuwakosoa waliojipata. Nadhani wangetumia muda mwingi kujitafuta kuliko kutumia majukwaa kama haya ya ulaji mihogo kueneza uchawa.

Naandika kwa nia nzuri tu kuwakumbusha kwamba maisha yanahitaji mambo mengi kuliko ulaji wa mihogo. Wanapaswa waanze kujitegemea na siyo kusubiri wanasiasa wawawezeshe. Wasipojitafuta watatafutwa
 
ulimaliza kuuza mihogo yako yote lakini pale coco maana biashara imekua ngumu kidogo na mfungo 🐒
 
Back
Top Bottom