Kwanini CHADEMA?

Kwanini CHADEMA?

Mkulia

JF-Expert Member
Joined
Apr 26, 2012
Posts
375
Reaction score
95
Imekuwa ni jambo la kawaida kwa serikali hii ya Jk kutoa lawama kwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) hasa inapotokea migongano kati ya wananchi na serikali. Ni mara kadhaa Rais mwenyewe au watendaji wake utawasikia wakidai kuwa CHADEMA wanahusika na migongano hiyo. Kwa mfano katika mgomo wa walimu,madaktari na hata vurugu za karibuni kule Mtwara juu ya suala la gesi serikali ilielekeza lawama kwa CHADEMA kuwa ndiyo chanzo cha matatizo yote hayo. Sasa sielewi ni kwanini serikali inakiona CHADEMA kuwa ndiyo chanzo cha matatizo hayo? Au watendaji wa serikali wanaamini kuwa watanzania ni mazuzu kiasi cha kushindwa kujitambua?
 
me naona hapo msemo wa Paka Akiwa Hakimu Panya ashindi Kesi unahusika.
 
Wana weweseka tu, si unajua hata taifa stars ikifungwa na Timu ya taifa ya BRAZIL, utawasikia wanatoa sababu za kufungwa as if walidhani kuwa wangeshinda. CCM haina uwezo wa kupambana na CHADEMA tukiondoa polisi na usalama wa taifa, ndiyo maana kila kitu kinachofanyika wanahisi kuwa CHADEMA wako nyuma yake kwa sababu ndiyo chama pekee ambacho kinaweza kuwahamasisha watu wakahamasika kutekeleza maazimio ya chama. Ni halali kwa ccm kufikiri kuitupia lawama CHADEMA, hawana namna nyingine, upeo wao umeishia hapo, wao wameicha kufikiri kuwa matatizo ya watz yamepelekea watz kuichukia nchi yao, wao wanaona adui yao mkubwa na mchonganishi wao na watz ni CHADEMA. Hizo zote ni dalili za dola inayoanguka.
 
Kama namwona Mkuu wa kaya!..hana wasiwasi, anatabasamu tu huku yuko katika maandalizi ya safari zake za ughaibuni. CCM oye!
 
Ikifikia mahali baba mzima analalamika anaonewa na mtoto mdogo, jua baba kashikwa pabaya.
 
Nahisi wanaweza hata kusema kuwa mgogoro wa kule Geita wa kidini CDM wanahusika!!
 
waachie nchi, ukiona mtu kaja kaishawishi familia yako na kutambua kuwa huwa unaitesa cha muhimu ni kuacha kuitesa familia ama ukimbie familia ukaanzishe maisha mapya huko mbele ya safari.
 
Kwani haujui kuwa hata Mbaazi zikikosa maua huzingizia jua?
 
ninashukuru vurugu za kidini zimetokea mwanza na sio moshi au arusha vinginevyo sijui ingekuwaje.kweli mungu sio madame b kawaumbua hadharani na udini wao walioupalilia
 
Kwa sababu ni tishio kwao,hivyo kwa mawazo yao wanawaza wakisingizia kila kitu kibaya kinafanywa
na CDM wanaweza kuichonganisha na wananchi,kitu ambacho their wrong wanazidi kuipandisha chati CDM"
 
Mioyo yao imejaa hofu......siku zote ujasiri au hofu kwa yeyote hutegemea zaidi kile mtu husika alichokitenda......matendo yao yamekuwa msingi wa hofu katika mioyo yao, na hii inaweza ikawa nguzo muhimu zaidi katika kuelekea ama kukifikia kifo chao(CCM).........binafsi sitaki niuaminishe moyo wangu kuwa CDM ndiyo njia pekee ya taifa hili kukombolewa kutoka mikononi mwa hawa mafisadi, ila uwepo wake ni muhimu pia katika kuchochea fikra za ukombozi katika TAIFA hili
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom