Kwanini CHADEMA wanauchukia Mwenge wa Uhuru?

Kwanini CHADEMA wanauchukia Mwenge wa Uhuru?

Simiyu Yetu

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2013
Posts
18,949
Reaction score
4,643
Kwa mda mrefu sasa wabunge wa CHADEMA wamekuwa wakiendesha harakati za kupinga mwenge wa uhuru.

Najiuliza chadema wanachukia mwenge wa uhuru au wanachukia shughuri zinazofanywa na mbio za mwenge, Pengine wanadhani mwenge usipopita wao watazidi kuungwa mkono kwenye maeneo mengi.

Lakini imani yangu ni kuwa chadema wanapingana na maendeleo yanayozinduliwa na kufunguliwa wakati wa mbio za mwenge kwani wao ni wapinga maendeleo ili serikali ionekane haijafanya kitu,hizi siyo siasa bali ni kupotoka kwani siyo busara kupinga kila kitu.
 
Hujui kitu. Kuzindua mradi hadi mwenge? Ina maana mwenge ukizimwa huwa hakuna miradi? Hivi wajua mwenge ukiwashwa hadi kuzimwa unatumia sh. ngapi ukimbizwa mikoa yote au ni wachache kupata posho.?
Mkuu we hewa kweli ambacho sijui nini hapo nilijua utatoa data unazojua lakini umetokwa povu tu.
 
Mkuu naamini kwa sasa mtu yeyote yule ambaye sio fisadi lazima atachukia mbiovza mwenge,hivi unajua ni kiasi huwa kinakimbiza huu mwenge,zamani tuliambiwa ulikuwa unamulika ili kutuletea tumaini,hakika kwa sasa sijaona tumaini lolote linaloletwa na mwenge,sijui kama ulishawahi kusoma post moja ililetwa hapa kuonyedha gharama za kukimbiza mwenge katika kawilaya kamoja tu kama sikosei,ni aibu mkuu.......Mwenge umekuwa uchochoro wa vifisadi vya CCM vinavyochipukia huko mikoani,wilayani na kwenye vitarafa,si ndio sifa ya CCM.....kikweli mwenge umepoteza hadhi yake ipo haja ya kuangalia utaratibu wa kukimbiza hii kitu kama ipo haja ya kufanya hivyo.
 
na mleta mada ungeacha ushabiki kwa maccm,ungeelewa kwa nini mwenge hauna faida yoyote zaidi ya kutafuna pesa za watu, lakini kwa mfano mwenge ungewekwa makumbusho huenda ungeliingizia taifa! fedha za kigeni kwa njia ya utalii...
 
Mie sio mwanachama wa chama chochote lakini napinga sana suala la mbio za mwenge. Wananchi wanajichanga wanajenga kadarasa kamoja, harafu unakuja kuzindua mwenge ambao ndani yake watu wamejilipa posho za 80,000 per day times 50 people. Bado wametumia magari waliyojaza mafuta pamoja na gharama za uchakavu. tunatumia milion 10 kwenda kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa choo cha shule? Kwa kweli tubadilike
 
hili liko wazi chadema ni wapinga maendeleo hatushangai kupinga maendeleo yanayofanywa na serikali.
 
Hujajibu swali kwa nini chadema wanaupinga mwenge wa uhuru hata sababu wanazotoa hazina maana.
 
Umempa jibu zuri kabisa 100%. Kwanza huku Kusini kuna malalamiko ya watumishi wa Serekali kukatwa shs 1000/ bila hiari yao.
 
Kwanini CCM wanaupenda Mwenge wa Uhuru? Fikiri kwanza kuhusu faida na hasara yake

CCM is just preserving one among the national emblems, Uhuru torch was introduced symbolically to shine the country and across the borders, to bring hope where there is despair, love where there is enmity, and respect where there is hatred!! we race it across the country to remind us of our roots as a nation...sasa kama unapingana na haya mawazo chanya, nitashangazwa na uzalendo wako.
 
Mkuu naamini kwa sasa mtu yeyote yule ambaye sio fisadi lazima atachukia mbiovza mwenge,hivi unajua ni kiasi huwa kinakimbiza huu mwenge,zamani tuliambiwa ulikuwa unamulika ili kutuletea tumaini,hakika kwa sasa sijaona tumaini lolote linaloletwa na mwenge,sijui kama ulishawahi kusoma post moja ililetwa hapa kuonyedha gharama za kukimbiza mwenge katika kawilaya kamoja tu kama sikosei,ni aibu mkuu.......Mwenge umekuwa uchochoro wa vifisadi vya CCM vinavyochipukia huko mikoani,wilayani na kwenye vitarafa,si ndio sifa ya CCM.....kikweli mwenge umepoteza hadhi yake ipo haja ya kuangalia utaratibu wa kukimbiza hii kitu kama ipo haja ya kufanya hivyo.
Mkuu umepinga nini na umekubari nini,sioni kama kuna gharama zozote za kuendesha mwenge ukilinganisha na faida zinazopatikana.
 
chadema kama waliweza kumsapoti kagame watashindwa kupinga mwenge wa maendeleo na uhuru ambao umekuwa ni chachu ya maendeleo katika maeneo mengi.
 
CCM is just preserving one among the national emblems, Uhuru torch was introduced symbolically to shine the country and across the borders, to bring hope where there is despair, love where there is enmity, and respect where there is hatred!! we race it across the country to remind us of our roots as a nation...sasa kama unapingana na haya mawazo chanya, nitashangazwa na uzalendo wako.
Mkuu hawa bavicha wanahitaji shule kubwa kuyaona haya,lakini tusichoke kuwapa shule.
 
wewe mtoa maada, mwege unaoushabikia ingekuwa vzr kama ungetoa faida zake. maaana kuzindua miradi wewe kwako ndo faida? Weka mada nyingine kuliko kuisema chadema. je hivi wajua mwenge ulichukiwa hata kabla ya chadema kuwepo?
 
Kwa akili yako kweli mwenge ulileta uhuru, matumaini, kuzuia rushwa na vyote vinavyotajwa, kama sio matambiko na ibada za sanamu. Lengo la mbio za mwenge ni kupumbaza watanzania, ma wamefanikiwa kwa hilo
 
Mwenge wa Uhuru ulikuwa na umuhimu kipindi unaanzishwa, ila kwa sasa wangeuweka tu pale makumbusho uangaliwe na watalii..
 
hili liko wazi chadema ni wapinga maendeleo hatushangai kupinga maendeleo yanayofanywa na serikali.

Iam an employee wa taasisi flani( jina kapuni) nimehudhuria sherehe kadhaa za kukabidhiana mwenge, Kaka ni matumizi mabaya sana fedha za umma, unajua escort ya magari yanayozunguka na mwenge? Totally ni matumizi mabaya sana, bado sijazungumzia posho hapo.
 
Back
Top Bottom