Kwanini CHADEMA wanashabikia muungano uvunjike?

TOURMALINE

Senior Member
Jan 4, 2013
125
24
Tangia rasimu ya katiba mpya itoke, imeonekana chadema wanashabikia muungano uvunjike na kuwe na serikali tatu.Kwanini chadema wanashabikia jambo hili?
 
maoni ya wananchi ni serikali tatu kwa mujibu wa rasimu ya katiba.Chadema haina msimamo zaidi ya ule kutoka kanisani.Msimamo wa kanisa ni aidha serikali moja au muungano uvunjike.Na msimamo huo umeangaliwa kwa maslahi ya kueneza dini

HNi kwa sababu wananchi hawataki Muungano! CHADEMA is just sauti ya Watu.

TUMBIRI (PhD Candidate, MBA(UDSM), Bcom(UDSM), PCM(Mzumbe High School - 2[SUP]nd [/SUP]Overall Best Student in Form Six National Exams),

In Journey to Arusha!
 
Tangia rasimu ya katiba mpya itoke, imeonekana chadema wanashabikia muungano uvunjike na kuwe na serikali tatu.Kwanini chadema wanashabikia jambo hili?
Chadema kimekua chama kinachowakilisha mawazo ya wananchi wengi wa Tanzania. Kwa hiyo hayo ni mawazo ya wananchi walio wengi.
 
Wewe kwa nini unautaka muungano???eleza faida na hasara zake.Halafu akili zako changanya na za wengine basi aliyekwambia ukiwa na serikali tatu ndio kuvunja muungano nani???
 
maoni ya wananchi ni serikali tatu kwa mujibu wa rasimu ya katiba.Chadema haina msimamo zaidi ya ule kutoka kanisani.Msimamo wa kanisa ni aidha serikali moja au muungano uvunjike.Na msimamo huo umeangaliwa kwa maslahi ya kueneza dini
Ni kwa sababu wananchi hawataki Muungano! CHADEMA is just sauti ya watu.
 
ni kipi hasa tunafaidi kutokana na nuungano zaidi ya mzigo wa kuwabeba wazenj wasiobebeka?
 
maoni ya wananchi ni serikali tatu kwa mujibu wa rasimu ya katiba.Chadema haina msimamo zaidi ya ule kutoka kanisani.Msimamo wa kanisa ni aidha serikali moja au muungano uvunjike.Na msimamo huo umeangaliwa kwa maslahi ya kueneza dini

Hayo ni maoni ya Tume ya Katiba siyo maoni ya Wananchi. Maoni ya Wananchi yanapatikana kwa kupigwa kura ya Maoni na kura hizo kusimamia na Tume huru.
 
Binafsi sina shida na aina yeyote ya muungano itakayoonekana kuwa sawa na pande zote mbili. Iwe serikali moja, mbili hata tatu ni sawa tu. Nina sababu mbili tu za kuupenda na kutojali sana aina ya muungano wetu.

1- Ni muungano pekee ambao bado uu hai hapa Afrika baada ya wengi kushindwa kama wale wa Senegambia.

2- Tupo katika hatua za kuungana (integration) na nchi nyingine za Adrika mashariki kwa hiyo baada ya miaka ishirini toka sasa, muungano wa Tanzania utakua ndani ya muungano mkubwa zaidi wa kifederali Inshallah.
 
...imeonekana chadema wanashabikia muungano uvunjike na kuwe na serikali tatu.Kwanini chadema wanashabikia jambo hili?
Ongeza na swali hili:
...imeonekana Tume ya Katiba inashabikia muungano uvunjike na kuwe na serikali tatu. Kwanini Tume ya katiba inashabikia jambo hili?
 
Kwani kusema unataka Serikali tatu unataka kuvunja Muungano au kuumarisha?
 
kwani huo muungano ukivunjika ni dhambi? cuf na ccm ndo wanavunja muungano
Tangia rasimu ya katiba
mpya itoke, imeonekana chadema wanashabikia muungano uvunjike na kuwe na
serikali tatu.Kwanini chadema wanashabikia jambo hili?
 
ni kipi hasa tunafaidi kutokana na nuungano zaidi ya mzigo wa kuwabeba wazenj wasiobebeka?

hebu tuwekee wazi mkuu.zanzibar inabwebwa kwa namna gani?ukishindwa hapo usizungumze kitu usichokijua
 
maoni ya wananchi ni serikali tatu kwa mujibu wa rasimu ya katiba.Chadema haina msimamo zaidi ya ule kutoka kanisani.Msimamo wa kanisa ni aidha serikali moja au muungano uvunjike.Na msimamo huo umeangaliwa kwa maslahi ya kueneza dini
Dos Santos
Huu msimamo wa Kanisa uliupata wapi? Labda ungetoa pia msimamo wa Msikiti.
 
Tangia rasimu ya katiba mpya itoke, imeonekana chadema wanashabikia muungano uvunjike na kuwe na serikali tatu.Kwanini chadema wanashabikia jambo hili?

Wanajua Kuwa ZNZ Wanainyonya bara kwani ni fedha nyingi zinatumika kubembeleza Muungano huku zenji wakilalamika sana hivyo njia sahihi ya kuepuka lawama ni kuwaacha zenji wawe Nchi Jilani
 
Me nahis muungano utakufa ccm tanganyika wakibwagwa chini na cdm ..kitaeleweka 2015 mbivu au mbichi
 
wewe unaetaka muungano, unatokea nchi gn? na je hyo nchi ipo? tunaitaka tanganyika kwanza.
 
Tangia rasimu ya katiba mpya itoke, imeonekana chadema wanashabikia muungano uvunjike na kuwe na serikali tatu.Kwanini chadema wanashabikia jambo hili?
Ni fikra mfu kudhani kuwa na Serikali tatu ni kuua muungano, mbona watu waliposema twende Serikali moja CCM kwa kutaka kupeana vyeo wakasema hapana wakati ndiyo hasa ungekuwa muungano badala ya kiini machi kilichopo. Rais wa Zanzibar anachaguliwa DOdoma kioja cha karne hiki. Tulipigania uhuru ili tuitawale Zanzibar?
 
Back
Top Bottom