Kwanini CHADEMA hawaongelei fedha za escrow?

Itaonekana wanamuunga ZITTO mkono, ni Kheri kwao bil. 200 zisirudi lakini si kumuunga mkono Zitto

Hivi hili sakata la escrow liliibuliwa na Gazeti La CITIZEN,Kafulila au Zitto? Mbona mnalitumia kisiasa sana ninyi msiojitambua?
 
Mbona hili swala cdm wanalipigia kelele kila siku?wewe unauliza chadema ipi?
 
Hivi hili sakata la escrow liliibuliwa na Gazeti La CITIZEN,Kafulila au Zitto? Mbona mnalitumia kisiasa sana ninyi msiojitambua?

Mimi wala si mwanasiasa, sina kadi ya chama chochote ila naipenda UKAWA, una lingine...?
 
jaribu walau kufanya research kabla haujaanza kutoa hoja.
 


Mkuu wanaongelea juzi nilikuwa musoma na nilihudhuria mkutano wao walikuwa wamejipanga wabunge waliokuwepo walijigawa wengine waliongelea katiba wengine wliongelea kukatwa kwa misaada na wengine waliongelea issue ya ESCROW kwa undani, pia MNYIKA ALILIELEZEA VIZURI WAKATI AKIWAKILISHA MAONI YA UPINZANI
 
Hii ni balaa kama hoja imeibuliwa na Zito c hoja hata kama ina mashiko haina maana? Basi siasa inatupeleka papaya.
 
Dr slaa pia alishaliongelea,na yeye ndiye aliyesema pesa za escrow siyo by 200,ni zaidi ya bn 400

Katibu Mkuu na Mwanasheria mkuu waliitisha mkutano na waandishi wa Habari

Katika hili nafanya kazi kwa karibu na ndugu David Kafulila nje ya Bunge kuhakikisha umma unaelewa kila kinachoendelea na pia ku-mobilize public dhidi ya serikali na mafisadi wote

Tumeitisha Mkutano na waandishi wa habari tukiwa na vijana wa vyama vyote na pia watumishi wa Umma pale Travertine Hotel

Tuendelee kuunga mkono kampeni "IPTL-Bring Back Our Money"
 
Sioni kama kuna ukweli. Kwanza ufisadi wa Escrow uliibuliwa na Kafulila na siyo Zito. Pia viongozi wa CHADEMA wameunga sana mkono vita dhidi ya ufisadi huo lakini utambue pia kuongelea kiundani zaidi hutegemea zaidi ushahidi ulio nao. CHADEMA wanamwunga mkono Kafulila lakini bado Kafulila ndiye kiongozi mkuu maana ndiye aliyeibua na ndiye mwenye nyaraka mbalimbali.

Mwezi uliopita tu, Mnyika alisema kuwa atapeleka hoja binafsi bungeni kuhusu Escrow. Hivi ulitaka CHADEMA wafanye nini zaidi ili uweze kujua kuwa ni wadau muhimu katika kupinga ufisadi wa Escrow. Vita yoyote huwa ina kiongozi, na katika hili la Escrow kiongozi ni Kafulila, sisi Watanzania wote tupo nyuma yake tukimwunga mkono kwa uwezo wetu wote lakini pia lazima tuwe makini, ukitaka uwe mbele ya Kafulila, unaweza ukakosa silaha ambazo Kafulila anazo, na tunaopigana nao wakiona uliyetangulia huna silaha wanaweza kukupiga kiurahisi na kundi lote likatawanyika.

Hapa ni lazima tutambue kuwa hii vita ina kiongozi na kiongozi huyo ni Kafulila, na tukishinda, credit ya kwanza ni kwa Kafulila, tusimpokonye uongozi huu bali tushirikiane naye.

we ndo umeongea kitu nilichokua nacho kichwan..big up mkuu
 

Kwani Zitto wa chama gani?
 
Citizen ni channel ilopitisha tu habari,there are politicians who fed them with info

Kama ndivyo bac wakupewa hongera ni kafulila na wala sio Zito coz tulimsikia kafulila akiliongelea bungen. Zito kabaki kuliongelea facebook.
 
Labda mkuu ulitaka hilo jmmbo liongelewa kwa namna gani ili urudhike? Pia hivi Sugu na Zitto (sahau kuhusu mahakama) ni wabunge wa chama kipi?
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…