Kwanini CHADEMA haichukuliwi hatua za kisheria? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwanini CHADEMA haichukuliwi hatua za kisheria?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mkwele, Mar 28, 2011.

 1. M

  Mkwele JF-Expert Member

  #1
  Mar 28, 2011
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 206
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Source: Tovuti ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)
  Orodha ya Mafisadi (List of Shame)

  B. USHIRIKI KATIKA KUTOA MAAMUZI YA KIFISADI

  11. RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE

  Rais Jakaya Kikwete amekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuanzia Desemba 2005. Kabla ya kuwa Rais, Mheshimiwa Kikwete alikuwa Waziri wa Mambo Nje na Uhusiano wa Kimataifa kuanzia 1995 hadi 2005, Waziri wa Fedha 1994 hadi 1995 na Waziri wa Maji, Nishati na Madini kuanzia mwaka 1990 hadi 1994. Kama Waziri wa Maji, Nishati na Madini, Mheshimiwa Kikwete alishiriki moja kwa moja katika kusaini mikataba mibovu ya madini na makampuni ya madini ya kimataifa ambayo kwayo taifa limeendelea kupoteza utajiri mkubwa na kuinyima Serikali uwezo wa kifedha wa kuhudumia wananchi. Kwa mfano, mnamo tarehe 10 Aprili 1990, Major Jakaya Mrisho Kikwete aliingia mkataba wa madini ya kampuni ya SAMAX Limited ambapo kampuni hiyo ilipewa leseni ya kuchimba dhahabu katika eneo la Lusu, Wilayani Nzega Mkoa wa Tabora. Matokeo ya mkataba huo, maelfu wa wachimbaji wadogo wadogo wa dhahabu waliokuwa eneo hilo waliondolewa kwa nguvu na vikosi vya FFU na bila ya kulipwa fidia yoyote. Hadi leo wananchi hao hawajalipwa fidia yoyote licha ya miaka zaidi ya kumi ya kufuatilia haki zao. Baada ya kutwaa utajiri wa dhahabu wa eneo hilo, SAMAX Limited iliuza eneo hilo kwa kampuni ya Ashanti Goldfields ya Ghana kwa dola za Marekani milioni 253. Ashanti Goldfields nao wakauza eneo kwa kampuni ya Resolute Limited ya Australia kwa kiasi kisichojulikana cha fedha za kigeni. Resolute Limited ndio waliojenga na wanamiliki Mgodi wa Dhahabu wa Golden Pride ulioko eneo la Lusu, Nzega hadi sasa na ambao ulifunguliwa mwezi Novemba 1998.

  Mnamo tarehe 5 Agosti 1994 Luteni Kanali Jakaya Mrisho Kikwete aliingia tena mkataba na kampuni ya madini Kahama Mining Corporation Ltd., kampuni tanzu ya kampuni ya Sutton Resources ya Canada. Ijapokuwa mkataba huu unaonyesha wazi kwamba ulikuwa unahusu eneo la Butobela Wilaya ya Geita Mkoani Mwanza, mwezi Agosti mwaka 1996 Kahama Mining Corporation wakisaidiwa na vikosi vya FFU walivamia eneo la Bulyanhulu, Wilaya ya Kahama Mkoani Shinyanga na kuwaondosha kwa nguvu watu takriban laki nne waliokuwa wakiishi na kuchimba dhahabu katika eneo hilo. Baada ya kutwaa eneo hilo kwa nguvu za kijeshi, Sutton Resources iliiuza Kahama Mining Corporation na Bulyanhulu kwa Kampuni ya Dhahabu ya Barrick Gold Corporation ya Toronto, Canada kwa dola za Marekani milioni 280. Leo hii Bulyanhulu ni moja ya migodi tajiri kwa dhahabu katika Bara la Afrika.

  Maandamano kidogo wanasema ni uchochezi, je list of shame sio uchochezi? Au IKULU inachelea kuibua mengi kama watawapeleka chadema mahakamani? Tujadili wanajamvi....
   
 2. Vin Diesel

  Vin Diesel JF Gold Member

  #2
  Mar 28, 2011
  Joined: Mar 1, 2011
  Messages: 8,401
  Likes Received: 736
  Trophy Points: 280
  kwa jina lako tu sitarajii uandike lolote jema kuhusu Mh Rais.
  nashauri kama una hoja uwe unaileta na source yake kwani hapo ndipo utakapodhihirisha ugreat thinker wako.
   
 3. Speaker

  Speaker JF-Expert Member

  #3
  Mar 28, 2011
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 6,357
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Hakuna mwenye ubavu wa kuwachukulia hatua za kisheria labda mipasho sawa wanaweza
   
 4. k

  kilolambwani JF-Expert Member

  #4
  Mar 28, 2011
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 395
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Wapelekwe mahakamani kwa lipi baya walilolitenda? Au kwa kosa la kueleimisha wananchi juu ya hatima ya nchi yao na kutujulisha mafisadi, au na wewe ni fisadi?
   
 5. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #5
  Mar 28, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  FALSAFA NZURI YA CHAMA CHA SIASA NI SHARTI IAKISI JAMII HUSIKA NA
  UHALISIA WA MATUMAINI / NDOTO ZAO, MAZINGIRA WANAMOISHI,
  URAHISI KUKUMBUKIKA / KUELEWEKA KWA FALSAFA YENYEWE NA YENYE KUENDANA VILIVYO NA KIPINDI KATIKA MAISHA WANAMOISHI

  Nitangulie kuwapa hongera sana sana tena sana CHADEMA kwa kuweza kuibuka na falsafa ambayo kiujumla ni sura halisi ya matakwa ya Wa-Tanzania na safari yetu ndefu kama jamii moja katika maisha haya.

  Hakika kwa ufahamu wangu falsafa ya CDM imekidhi misingi yote muhimu kiasi cha kutosha kututambulishia kwamba CHADEMA ni watu gani katika jamii yetu, wanaamini katika lipi na siku zote tuwafanyie tathmini katika uendeshaji wa shughuli za kila siku katika taifa hili huku wananchi tukizingatia misingi gani hasa zinazotambulika rasmi.

  Ndio, Falsafa ya Chama Cha Siasa si sawa na mtu kufanya ziara binafsi kwenye mbuga za wanyama kokote duniani. Wala Jambo hili halipigiwi KOFULI MLANGONI kwamba haukua nalo jana leo hii ukitangaza kuwa nalo basi ni kosa la jinai - laa hasha!! Hivyo mtu kusema kwamba labda kwa kuwa Mwenyekiti Mstaafu, Mhe Edwin Mtei, katika mahojiano yake na vyombo vya habari pengine miaka 5 iliyopita hakulitaja falsafa ya Chama; hiyo peke yake hakizuii chama kuweza kupiga hatua zaidi kwa KUJIPA SURA HALISIA kisiasa nchini.

  Kiukweli, kupokezana kule kete la majukumu ndani ya Chama na hiyo ndio maana tunasema CHADEMA ni cha Wa-Tanzania wote na wala si mali ya mtu binafsi kama vilivyo vyama vingine vya mifukoni hapa nchini hivyo kama Mzee Mtei aliweza kutekeleza hatua fulani muhimu kwa uhai wa chama hiki basi nasisi Vijana Wa-Tanzania wenye mali yao tunaendelea kukamilisha mengine na mengi zaidi mazuri bado yako njiani yanakuja - kaeni mkao wa ushindi kote nchini!!

  Nielewavyo mimi, falsafa ya Chama Cha Siasa kwa maelezo miepesi ni UJUMLA WA MAWAZO NA FIKRA yanayotafuta kumtambulisha mtu na au Chama na kile anachokiamini, kupenda kuliona likitendeka kwa jamii yake na kwamba yuko tayari kuwekeza muda na rasilmali nyinginezo muhimu kuendeleza fikra na mawazo hayo kwa faida na maendeleo ya jamii katika ujumla wake.

  le majibu ya maswali ya msingi kama vile; (1) nyinyi kama Chama cha siasa wananchi tuwatambueni kuwa muu akina nani hasa?? (2) mnaamini katika mambo yepi hasa ambayo lasimamia ambayo ndiyo itakayokua ni chimbuko na muongozo wa shughuli zenu zote kiutendaji kama chama.

  Na kwa mantiki hii ndipo nako tunapotangaza kwamba ni mwisho wa SIASA ZA MKUMBO huku tukifungua ukurasa mpya wa siasa za kisasa zenye kuegemea misingi ya wazi na iliotukuka mioyoni mwa Wa-Tanzania tuliowengi.

  Hadi hapo nawashauri vijana wenzangu kote nchini na wananchi kwa ujumla kwamba maadam sote tumeshajionea madhara makubwa yalioletwa na falsafa mpya ya Chama fulani nchini; falsafa ya 'Kasi Mpya, Nguvu Mpya na Ari Mpya' pasipo kuelewa hasa dira zima ya wapi tunakopelekwa kama taifa, na hatimaye kutokea ajali ya mwaka kisiasa ambapo chama hicho hivi sasa kimeparaganyika vipande 200 kidogo, ni muda muafaka sote tukajiunga CHADEMA leo hii na wala si kesho.

  Hakika CHADEMA pekee ndiyo nyumba salama kisiasa kwa watu wa rika zote, dini zote, rangi zote, jinsia zote na daraja zote za uelewa sawa na vile ambayo hata Marehemu Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere aliiona na kutuambia kwa kinywa kipana sote nchini.
   
 6. anti-fisadi

  anti-fisadi JF-Expert Member

  #6
  Mar 28, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 369
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  aisee, hili jeshi la FFU ndio linatumika hivi...halafu eti ndio tunasema hii nchi ni salama! unaondoa raia laki 4 kwa ajili ya kuwanufaisha mafisadi na wageni kibao,unawaacha hao raia wengi (maskini) bila kuwalipa fidia yoyote; haf mnadai hii nchi ina amani?? kweli??

  inasikitisha...
   
 7. M

  Mkwele JF-Expert Member

  #7
  Mar 28, 2011
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 206
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0

  Thread umeanza kuisoma katikati ndio maana hukuona source, next time acha kukurupuka.
   
 8. M

  Mkwele JF-Expert Member

  #8
  Mar 28, 2011
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 206
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0

  Duuuh! Huku ielewa thread, rudia tena kuisoma.
   
 9. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #9
  Mar 28, 2011
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  wana ubavu wa kuwashitaki?wathubutu waone cha moto
   
 10. M

  Mkwele JF-Expert Member

  #10
  Mar 28, 2011
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 206
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Wakati wa Mkapa serikali ilikuwa inakurupuka kuwashitaki wanasiasa kama Mtikila na Mrema kwa sababu wamekashifu Rais hata kama ni kweli lkn sasa hivi ni ngumu kwani wananchi tumeamka, ukimpeleka mtu kama Dr. Silaa mahakamani basi kila kitu kitajulikana au mchezo mzima ulichezwa sirini na mafisadi utajulikana ndio maana serikali yetu hii ni nyonge kwelikweli.

  Hivi kwa ufisadi wote waliofanya kwanini bado wapo madarakani wanatuongoza na kutumia kodi kutoka kwenye mishahara yetu. Jamani mimi inaniuma!!
   
 11. sweetlady

  sweetlady JF-Expert Member

  #11
  Mar 28, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 16,982
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  tehe, tehe, tehe! Thnx! Umeifnya cku yng ianze vzr!
   
 12. m

  mmaroroi JF-Expert Member

  #12
  Mar 28, 2011
  Joined: May 8, 2008
  Messages: 2,536
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Hawana ubavu wa kuchukua hatua kwa chadema kwa kuwa ni mafisadi na chadema wanasema ukweli.
   
 13. NG'OMBE

  NG'OMBE JF-Expert Member

  #13
  Mar 28, 2011
  Joined: Mar 26, 2011
  Messages: 362
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Nani aanze kuchukua hizo hatua za kisheria? maana serikali yote hakuna aliye msafi.
   
 14. IsangulaKG

  IsangulaKG Verified User

  #14
  Mar 28, 2011
  Joined: Oct 14, 2010
  Messages: 702
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 45
  Serikali imenyambuliwa sana kwenye List of Shame...Hawana cha kufanya watalalama tu!
   
 15. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #15
  Mar 28, 2011
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,121
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  mwenye makosa ndiye huchukuliwa hatua za kisheria. CDM wametenda kosa gani kisheria?
   
Loading...