Allen Kilewella
JF-Expert Member
- Sep 30, 2011
- 18,278
- 33,880
Tume ya Jaji Fransici Nyalali iliposema kwamba asilimia themani (80%) ya watanzania wanapendelea kubakia kwenye mfumo chama kimoja lakini wanapendekeza mabadiliko kadhaa yafanyike kwenye CCM, wana CCM wengi walitafsiri kwamba watanzania wamekataa mfumo wa vyama vingi. Kama si uelewa wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, leo hii tusingekuwa na vyama vingi.
Mwalimu alisema kwamba, watanzania wanapendelea kubakia kwenye mfumo wa chama kimoja, lakini "lakini" zao ni nyingi sana kiasi kwamba haiwezekani kufanyike marekebisho kwenye Katiba ya CCM na CCM ikabakia ilivyo kama CCM. Mwalimu alisema mapendekezo mengi yanakwenda kinyume na mtizamo, falsafa na Itikadi ya CCM.
Mwalimu akashauri kwamba hao wenye hizo "lakini" wapewe jukwaa nje ya CCM ambako watapata fursa ya kufuata falsafa, Itikadi na mitazamo yao hiyo isiyofanana na CCM. Jambo rahisi la kutafsiri mapendekezo ya Tume ya Jaji Nyalali ukawa ni mzigo mzito sana kwa wana CCM.
Kwa mujibu wa katiba yetu ya Jamhuri ya Muungano Tanzania, hakuna mahali popote panapoelezwa majukumu na wajibu wa chama kinachokuwa madarakani, lakini kwa kuwa CCM ni wagumu kuelewa mambo rahisi, kila wakati wanadhani serikali ya Tanzania ni mali yao. Utawasikia wakisema "Sisi CCM ndiyo tumekuajiri" "Hii ni serikali ya CCM" "Mwenyekiti wa chama chetu ni Amiri Jeshi Mkuu usimchezee" Yaani jambo rahisi tu la kujua kwamba serikali ni mali ya watanzania wote limewashinda kuelewa.
Nitaendelea kuweka mambo rahisi ambayo wana CCM inakuwa vigumu kuyaelewa!!