Kwanini Campaign yoyote ile ikianzishwa na Clouds tv na radio inafana ila kwa wengine huwa zinafeli?

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
59,949
119,214
Sijawahi kuona Campaign yoyote ile inaanzishwa ama na Clouds tv au Clouds fm radio halafu isipate mashiko na kufanikiwa kwa kiasi kikubwa sana. Lakini cha kunishangaza kama hata siyo kunisikitisha ni kwamba kuna Media zingine zikianzisha tu jambo fulani hata liwe dogo au kubwa katika Jamii halifanikiwi.

Je naomba kuwaulizeni Wadau hivi hawa Clouds Media Group kupitia hizi brands zao kubwa za Clouds tv na Clouds fm radio kwanini hufanikiwa mno katika kila wanachokianzisha katika Jamii yetu na kwanini washindani wao wengine ( namaanisha Media zingine ) wao huwa hawafanikiwi kama wao?

Clouds Media Group ( CMG ) niwashukuruni na niwapongezeni sana kwa kuwa juu Kiushandani.

Nawasilisha.
 
Nyie ma media nyingine mmerundika mapopoma kibao hawana ubunifu hata chembe. Unategemea Shabani Kissu au Richard Leo au Marini Hassan akawa na ubunifu gani. Mapopoma wamezidi kwenye media. Lakini pia Ruge yuko vizuri kichwani huwezi mlinganisha na lile popoma lenzio Li Ze Mananiiiiz
 
Kwa maoni yangu clouds media group ni kama timu bora kabisa ya mpira wa miguu ambayo kila mchezaji mwenye kipaji anataka kuichezea kwa maana hiyo wanachukua best talent kutoka kila pembe ya Tanzania ndo maana unaona wanafanikiwa.
 
Sijawahi kuona Campaign yoyote ile inaanzishwa ama na Clouds tv au Clouds fm radio halafu isipate mashiko na kufanikiwa kwa kiasi kikubwa sana. Lakini cha kunishangaza kama hata siyo kunisikitisha ni kwamba kuna Media zingine zikianzisha tu jambo fulani hata liwe dogo au kubwa katika Jamii halifanikiwi.

Je naomba kuwaulizeni Wadau hivi hawa Clouds Media Group kupitia hizi brands zao kubwa za Clouds tv na Clouds fm radio kwanini hufanikiwa mno katika kila wanachokianzisha katika Jamii yetu na kwanini washindani wao wengine ( namaanisha Media zingine ) wao huwa hawafanikiwi kama wao?

Clouds Media Group ( CMG ) niwashukuruni na niwapongezeni sana kwa kuwa juu Kiushandani.

Nawasilisha.
Una hisa na Clouds Media Group??
Una nyuzi nyingi humu kuwafagilia, au wee ndo Shaffih Dauda nini??
 
Iko hivi.

●Kampeni nyingi za media zingine hua wanaiga kutoka clouds. Wanarudia kitu ambacho clouds wamekifanya kwa ufanisi wa juu.

●Clouds wana team imara sana, huwezi kuta vilaza wanaendesha campaign ama kitu chochote. Media zingine wanafanya vitu kwa mazoea, unakuta mtu km bikira wa kisukuma anatangaza taarifa ya habari.

●Clouds wanajua maana ya biashara - huwezi kufanya biashara bila kuwa na network. Hawa jamaa hua wanajitahidi kilamba watu miguu kadri wawezavyo.

●Clouds wanafahamu nini wananchi wanataka, hawafanyi vitu wanavyotaka wao. Mf ishu ya DAB, walijua kucheza na hisia za watu baada ya kuona DAB anaweza kuwadidimiza kibiashara, wakatafuta njia nzuri ya kumpiga chini. Kwa kufanya hivyo wanaongeza ushawishi wao huku kitaa, so campaign zao zinakua na muitikio mkubwa.

●Clouds kuna watoto wa mjini - kina ruge wale wasikie tu hivi hivi, wanajua sana kupika majungu ya under carpet kuwadidimiza washindani wao.
 
Kwa maoni yangu clouds media group ni kama timu bora kabisa ya mpira wa miguu ambayo kila mchezaji mwenye kipaji anataka kuichezea kwa maana hiyo wanachukua best talent kutoka kila pembe ya Tanzania ndo maana unaona wanafanikiwa.

Na ukiona Mtu yoyote anaichukia Clouds Media Group jua ana matatizo ya Kutukuka kabisa ya akili na fikra.
 
Una hisa na Clouds Media Group??
Una nyuzi nyingi humu kuwafagilia, au wee ndo Shaffih Dauda nini??

Ukijua au usipojua itakusaidia nini Mkuu? Halafu mbona na Wewe unaonekana kuichukia sana Clouds Media Group hata nyuzi zako nyingi nyingi tu zinazowahusu huwa unawakandia / unawasiliba sana. au Wewe ndiyo Majizo kama siyo Ssebo nini?
 
Labda ungetaja hizo campaigns za media nyingine zinazofanana na za Clouds ambazo unaona kwenye hizo media nyingine hazijafanikiwa.

Si Clouds hawahawa walichemka kwenye mchakato wa kumpigia debe Lowassa alipokua CCM.Nakumbuka walifanya live coverage pale Arusha wakati Lowassa anatangaza nia.Mc alikua Kibonde,walitengeneza jingles nyingi sana kila muda unasikia tangazo

Hii ni moja ya media campaign waliyochemka vibaya.
 
ruge sio wa sport sport

Hakuna Kichwa ninachokikubali Tanzania nzima ukikiondoa cha Nyerere, Baba GENTAMYCINE na huyu Ruge Mutahaba. Ingekuwa ni katika mpira basi Ruge Mutahaba angekuwa ni Lionel Messi kwani Jamaa anajua halafu ni Fundi vile vile. Tanzania ya leo inawahitaji akina Ruge Mutahaba 1000 tu nchi ipige hatua kubwa na za haraka mno za Kimaendeleo. Ruge huwa napishana nae katika UPOPOMA wake mwingine tu ila katika masuala ya Upambanaji na Maendeleo ya Kijamii namvulia Kofia na namkubali sana.
 
Ndugu yako RC alisema yeye ndio aliwapa ma idea ya Dar mpya na Ruge ni mtunga ngonjera tu ndio anachoweza

Basi kwa kukusaidia tu na kwa taarifa yako na kwa faida ya MAPOPOMA wote ni kwamba tokea alipokuwa Mkuu wa Wilaya hadi Mkuu wa Mkoa hivi Think Tank wa Paul Christian Makonda ni Ruge Mutahaba na mafanikio mengi ya Kiwilaya na Kimkoa ambayo yalionekana na hata kuanzishwa na Makonda nyuma yake alikuwepo Ruge Mutahaba na kwa bahati nzuri sana hata ukweli huu mwenyewe Paul Makonda anaujua. Sipendi niende in to details juu ya hawa Wawili ila fahamu ya kwamba aliyekuwa Champion wa Development ideas zote za Makonda ni huyo Ruge Mutahaba. Naomba niishie hapa tafadhali.
 
Labda ungetaja hizo campaigns za media nyingine zinazofanana na za Clouds ambazo unaona kwenye hizo media nyingine hazijafanikiwa.

Si Clouds hawahawa walichemka kwenye mchakato wa kumpigia debe Lowassa alipokua CCM.Nakumbuka walifanya live coverage pale Arusha wakati Lowassa anatangaza nia.Mc alikua Kibonde,walitengeneza jingles nyingi sana kila muda unasikia tangazo

Hii ni moja ya media campaign waliyochemka vibaya.

Unaonekana Wewe ni kama vile unatokea katika Media outlet moja hapa Tanzania. Haya hebu tuambie Wewe hako Ka media kako kamefanikiwa katika Kampeni gani ya Kimaendeleo hapa mjini au nchini Tanzania ili tuweze kufanya mlinganisho wa Kimantiki. Ukiona Mtu anaichukia Clouds Media Group hasa brands zake kuu mbili za Clouds tv na Clouds Radio jua ana matatizo kidogo katika Nyaya zake za Utimamu wa akili Kichwani.
 
Daah ila umezidi aisee ha ha ha
 
Back
Top Bottom