Kwanini binadamu ni viumbe pekee wa aina yetu hapa duniani?

Kwanini binadamu ni viumbe pekee wa aina yetu hapa duniani?

Stephen Ngalya Chelu

JF-Expert Member
Joined
Oct 31, 2017
Posts
8,288
Reaction score
18,571
Nimekuwa nikijiuliza hili swali kwa muda mrefu na leo nimeamua niulize humu ili nipate pia mawazo yenu. Viumbe wengi waliopo duniani wamekuwa na maumbo ya kufanana japo wapo kwenye species tofauti.

Mfano; mbwa, ng'ombe, mbuzi, kondoo ni viumbe wa species tofauti lakini kwa kiasi fulani wanafanana kimuonekano. Wote wana miguu minne, wana mikia, wana masikio yaliyotokeza juu nk.

Ndege, wapo species tofauti tofauti ila wanafanana kwa maumbo yao na vitu vingi vinavyoendana na hivyo. Na mifano inaendelea na kuendele kwa viumbe wengine.

Lakini ukija kwa binadamu sisi ni species moja tu. Hakuna viumbe wengine wa species tofauti ambaye ana mwonekano kama wetu. ni sisi tu.

Kwa nini?
 
Back
Top Bottom