Kwanini binadamu hawezi kuumba mtu?

Kwanini binadamu hawezi kuumba mtu?

Shy land

JF-Expert Member
Joined
Jul 28, 2013
Posts
6,245
Reaction score
2,848
Katika maswala ya uumbaji wa binadamu jinsi anavyoelezwa kwenye vitabu vya Mungu kwamba binadam aliumbwa kwa udongo hii hoja ni kweli kabisa.

Hii hoja ni sahihi kwa sababu ya kwamba mwili wa binadamu ni udongo kutokana vyakula na Oksijeni anavyotumia katika maisha yake inatokana na mimea ambayo maisha yake kwa asilimia kubwa inategemea udongo.

Kwahiyo; Ng'ombe, kuku, na wanyama wote wanaoliwa nyama zao ni udongo.

Kwa hiyo mmea umesimama kama mashine ya kuchota kile kinachofaa kwenye udongo na kukitegeneza ili kiweze kujenga na kutegeneza mwili wa binadam kwa taratibu maalum.

Wadau na Wanasayansi wa JF, Hivi ni kweli hakuna uwezekano wa kutengeneza mwili wa binadamu kwa kutumia virutubisho muhumu vinavyopatikana kwenye vyakula tunavyokula.

Mungu alituumba kwa mfano wake, why tusiweze kuuumba na sisi mwili wa binadamu?

Nawasilisha.
 
Haiwezekani kwasababu hatuna elimu hiyo tutaishia kutengeneza marobot na kuchanganya mbegu za viumbe kusubiri msaada wa Mungu kiwe
 
Kwanini Mungu hawezi kumuumba Mungu mwingine mwenye uwezo zaidi yake?!
 
Akili ya Mungu ni kama maji ya bahari
Akili ya mwanadamu ni kama tone kwenye kisoda
Hivyo haiwezekani
 
Kwa sababu haiwezekani

Hili ni wazo ambalo ukifikiri kwa hali ya kushidwa kweli utaliona huwezi na ni ngumu pia kutokea.

hakuna jambo ambalo limefanikiwa hapa duniani kwa kukosa utajiri wa kuwaza na kutafakari. lazima uwe na utajiri wakuwaza ndio upate kitu kipya

kwa nini ishidikane kutegeneza mwili wa mtu, hata ambao hauko hai??

Nasema hivyo nikiwa na mawazo chanya kabisa kwamba unaweza ukafata na kutegeneza kifaa kinacholingana na mfumo wa uzazi wa mwanamke kwa lengo la kupata sehemu zuri yakupatia kiumbe.

kifaa hicho kishategenezwa tunafaata taaratibu za virutubisho vinavyotakiwa kupewa ili mashine ili itegeneza kiumbe,

kwa kuanzia unaweza ukatoa kiumbe ambacho kimekufa lakin kiwe na nyama na mifupa baadaye tutatafuta namna ya kuweka uhai.
 
Akili ya Mungu ni kama maji ya bahari
Akili ya mwanadamu ni kama tone kwenye kisoda
Hivyo haiwezekani

Akili ya Mungu ni kama ya binadam kwa sababu alituumba kwa mfano wake.
 
mh hizi bangi mnazovuta sijui zinalimwa wapi?? au ndo zinatoka mapango ya amboni?? noooo itakuwa ni visiwa vya tanganyika na zimbabwe
 
Hili ni wazo ambalo ukifikiri kwa hali ya kushidwa kweli utaliona huwezi na ni ngumu pia kutokea.

hakuna jambo ambalo limefanikiwa hapa duniani kwa kukosa utajiri wa kuwaza na kutafakari. lazima uwe na utajiri wakuwaza ndio upate kitu kipya

kwa nini ishidikane kutegeneza mwili wa mtu, hata ambao hauko hai??

Nasema hivyo nikiwa na mawazo chanya kabisa kwamba unaweza ukafata na kutegeneza kifaa kinacholingana na mfumo wa uzazi wa mwanamke kwa lengo la kupata sehemu zuri yakupatia kiumbe.

kifaa hicho kishategenezwa tunafaata taaratibu za virutubisho vinavyotakiwa kupewa ili mashine ili itegeneza kiumbe,

kwa kuanzia unaweza ukatoa kiumbe ambacho kimekufa lakin kiwe na nyama na mifupa baadaye tutatafuta namna ya kuweka uhai.

Kila la heri
 
Miongoni mwa maswali ya kwanini ambayo yanachekesha ni kama yafuatayo:
Kwanini binadamu ana miguu miwili
Kwanini Mungu aonekani
Kwanini Binadamu wanakufa
Kwanini Mungu aliumba wanaume na wanawake
Kwanini damu ni nyekundu n.k
Jingine la kuchekesha ni hili hapa:
Kwanini binadamu hawezi kuumba mtu,
Jamvi haliishi vituko, hivi unafikiri kuna mtu atakayeweza kujibu hilo swali unaloliuliza? Kajipange bwana mdogo wa Shinyanga.
 
mh hizi bangi mnazovuta sijui zinalimwa wapi?? au ndo zinatoka mapango ya amboni?? noooo itakuwa ni visiwa vya tanganyika na zimbabwe

Umenisaidia Comment Yangu,kwamba Binadamu Aumbe Binadamu? Kweli Hizi Ni Bangi Za Kisiwa Cha Migingo,au Shibe Iliyopitiliza,kama Binadamu Hawezi Kuumba Hata Mbwa Tu Au Hata Nyoka,au Hata Sisimizi Leo Ije Kuwa Binadamu? This is Crazy Mind.
 
Binadam ndiye anayeumba mwingine baada ya Mungu kuumba yule wa kwanza. Mwanaume alipewa uwezo wa uumbaji.Mbegu za mwanaaume ndio zenye uhai.
 
Katika maswala ya uumbaji wa binadamu jinsi anavyoelezwa kwenye vitabu vya Mungu kwamba binadam aliumbwa kwa udongo hii hoja ni kweli kabisa.

Hii hoja ni sahihi kwa sababu ya kwamba mwili wa binadamu ni udongo kutokana vyakula na Oksijeni anavyotumia katika maisha yake inatokana na mimea ambayo maisha yake kwa asilimia kubwa inategemea udongo.

Kwahiyo; Ng'ombe, kuku, na wanyama wote wanaoliwa nyama zao ni udongo.

Kwa hiyo mmea umesimama kama mashine ya kuchota kile kinachofaa kwenye udongo na kukitegeneza ili kiweze kujenga na kutegeneza mwili wa binadam kwa taratibu maalum.

Wadau na Wanasayansi wa JF, Hivi ni kweli hakuna uwezekano wa kutengeneza mwili wa binadamu kwa kutumia virutubisho muhumu vinavyopatikana kwenye vyakula tunavyokula.

Mungu alituumba kwa mfano wake, why tusiweze kuuumba na sisi mwili wa binadamu?

Nawasilisha.

Mwanaume na mwanamke wakijamiiana siku ya mwanamke kushika ujauzito basi hapo ndipo binadamu anakamilisha uumbaji wa mwanadamu mwingine. Wewe unataka mwanadamu aumbwe kama production ya magari au soda kiwandani? Kwa maneno mengine ni kwamba kiwanda kiko kati ya mwanaume na mwanamke, na hasa nadhani kiwanda kiko ndani ya mwanamke, yaani womb.

Je, unafahamu kuwa energy tunayoipata na muhimu kwa binadamu inatokana na Jua, rejea biology yako ya o-level topic ya food chain utapata majibu.
 
Miongoni mwa maswali ya kwanini ambayo yanachekesha ni kama yafuatayo:
Kwanini binadamu ana miguu miwili
Kwanini Mungu aonekani
Kwanini Binadamu wanakufa
Kwanini Mungu aliumba wanaume na wanawake
Kwanini damu ni nyekundu n.k
Jingine la kuchekesha ni hili hapa:
Kwanini binadamu hawezi kuumba mtu,
Jamvi haliishi vituko, hivi unafikiri kuna mtu atakayeweza kujibu hilo swali unaloliuliza? Kajipange bwana mdogo wa Shinyanga.

Mkuu uwezekano wa binadam kuumba mtu upo.
kwa sababu zifuatazo.
1, unatakiwa kufuta mawazo ya kwamba huwezi.

2 kusoma na kuelewa mfumo wa uzazi wa mwanamke kwa uhakika.

3, kubuni kifaa kinachofanana na kufanya kazi kama mfumo wa uzazi wa mwanamke.

4, kutabua vitu na virutubisho muhimu zinawoweza kupeleka ili zile kiumbe kinachotoke kijitoe hewa zote pamoja na virutubisho.

nb. haya ni moja ya mawazo kama ukiyafanyia kazi unaweza kuwa mwanasayansi wa kwanza dunian kuumba kiumbe hai, kwa majaribio unaweza ukaanza na panya.
 
Mwanaume na mwanamke wakijamiiana siku ya mwanamke kushika ujauzito basi hapo ndipo binadamu anakamilisha uumbaji wa mwanadamu mwingine. Wewe unataka mwanadamu aumbwe kama production ya magari au soda kiwandani? Kwa maneno mengine ni kwamba kiwanda kiko kati ya mwanaume na mwanamke, na hasa nadhani kiwanda kiko ndani ya mwanamke, yaani womb.

Je, unafahamu kuwa energy tunayoipata na muhimu kwa binadamu inatokana na Jua, rejea biology yako ya o-level topic ya food chain utapata majibu.

Mwanamayu hakuna kisichowezekana tunaweza tukaichota hiyo energy ya jua pamoja na virutubisho vyote kwa mitambo maalamu tukaipelekea mashine yetu tuliyoiumba kwa mfumo wa uzazi wa mwanamke, matokeo yake tunapata kiumbe.
 
Last edited by a moderator:
Binadam ndiye anayeumba mwingine baada ya Mungu kuumba yule wa kwanza. Mwanaume alipewa uwezo wa uumbaji.Mbegu za mwanaaume ndio zenye uhai.

Binadamu anao uwezo wa kutegeneza bengu za kiume kwa utalaam malaam, kwa nini asiweze kutegeneza mashine ya kutegeneza kiumbe kwa taaratibu ya kibailojia zaidi.
 
Kama sisi wengine tumeshindwa kumtengeneza binadamu si ndo wewe uchukue hiyo fulsa ??????????? si misifa hiyo utakayo hipata
 
Binadamu hawezi kuumba binadamu mwenzake, kwa kuwa naye aliumbwa na Mungu.

Kwa hiyo ni Mungu pekee mwenye uwezo wa uumbaji, ambaye ndiye aliyeumba dunia na vyote vilivyomo duniani na akaumba pia viumbe vyote vilivyomo humu duniani, tukiwemo sisi binadamu, ikiwa ni pamoja na wewe na mimi.

Pia Mwenyezi Mungu kwa uwezo wake mkubwa sana, aliumba pia sayari zote zinazoizunguuka dunia.

Kwa hiyo Mwenyezi Mungu, ambaye ni alpha na omega, uwezo wake ni mkubwa sana tena sana, ambao hauwezi kufananishwa hata kidogo na uwezo wa binadamu.

Ndiyo maana ukitaka kutafakari na kuchunguza uwezo alio nao Mungu, utaishia kuumiza kichwa chako, kwa kuwa Mwenyezi Mungu ametuwekea 'speed governor' kwenye bongo zetu, pale tunapoanza kuupeleleza na kutaka kuujua kwa undani ukuu na uwezo wake.
 
Back
Top Bottom