Kwanini baadhi ya watanzania wanamuhukumu Lowassa?

Kwanini baadhi ya watanzania wanamuhukumu Lowassa?

weraufo

Member
Joined
Jun 12, 2015
Posts
20
Reaction score
5
Hivi baadhi ya watanzania ni kwamba wanamchukia tu Mh. Lowasa kwa sababu zao au wanaogopa utendandaji kazi wake?

Mh Lowasa ni mtanzania na binaadamu kama mtu mwingine yeyote yule ambaye ni mtanzania na binaadamu, watanzania wamekuwa wakimuhukumu huyu mzee na kujisahahu kama wao pia ni binaadamu na wanakosea, na kwakufanya hivyo watanzania hao, wamechukua nafasi ya Mungu, na kujiona wao ndio wanaweza kuhukumu na sio Mungu, kama nikikumbuka vizuri Lowasa alishatubu tena na akaenda mbele zaidi kwa kuchukua maamuzi magumu na kuamua kujiuzuru wadhifa wake wa uwaziri mkuu.

Na Mungu alishatuambia hata kama dhambi zenu zilikuwa nyekundu kama bendera, zitakuwa nyeupe kama sufi, kwa maana hiyo Yeye ndiye anaye samehe na Yeye ndiye anaye hukumu, na msamaha wa Mungu unatatokana na pale tu, mtu anapotubu, na tukishatubu huwa tunaamini ya kwamba tumesamehewa, kwahiyo Mh Lowasa alishatubu na akaamini ya kwamba amesamehewa, sasa ni kwanini baadhi ya watanzania wanahukumu kitu ambacho kilishafanyiwa toba?

Watanzania wengi huwa hawajiamini, na kutokujiamini huwa inaleta woga, na woga ukikoma huleta chuki na wivu, tusipokuwa makini chuki na wivu ambao upo kwenye jamii leo hii, zitatuingiza kwenye migogoro isiyofaa, watanzania tubadilike, tuombee nchi yetu na tuombee viongozi wote pasipo kubagua, na mengine tumwachie Mungu.
 
Hakuna anayemchukia Walla kumuogopa. Bali wanamhamu kuwa hafai kuwaongoza wa Tanzania ktk kukabiliana na changamoto zinazowakabili kwa kuwa hana uwezo.
 
Mungu Anayeipenda Na Kuibariki Tanzania Kaamua kuhukumu UFISADI Kwenye Taifa lake Teule kwani huu ndio wakati muafaka. Pima mwenyewe mchakato wa hilo zoezi. Linapokuwa limemalizika na kukamilika kwa ufanisi ... Lituacheje. ?
 
NAMI NASHANGAA INAKUWAJE WATU WANAMTETEA LOWASA NAMNAHII,NDUGU ZAKE WAKO KIMYA,YAANI HAWAONI ALICHOFANYA WANAULIZA KOSA LAKE.KATUBU WAPI YEYE ANALALAMIKA TUU! WEWE MBONA UNAM2BIA..WACHA ASEME MWENYEWE. WEWE NDO HUJIAMINI. LZM TUMJUE ANAETAKA KUTUONGOZA YUKOJE,KIONGOZI MZURI ANAJULIKANA.kakaa bungeni miaka3 kama mbunge wa kawaida..hajachangia wala kukemea chochote..bunge la katiba nalo kimya.hawezi kufananishwa na kafulila huyo.
 
hakuna anayemhukumu lowassa ila anajihukumu mwenyewe kwa ufisadi wake mpaka sasa anatumia pesa alizoiba kuingia ikulu halafu unasema ametubu tumemsamehe umemsamehe wewe na nani njaa zenu ndio zinaleta viongozi wabovu
 
Hivi baadhi ya watanzania ni kwamba wanamchukia tu Mh. Lowasa kwa sababu zao au wanaogopa utendandaji kazi wake?
Mh Lowasa ni mtanzania na binaadamu kama mtu mwingine yeyote yule ambaye ni mtanzania na binaadamu, watanzania wamekuwa wakimuhukumu huyu mzee na kujisahahu kama wao pia ni binaadamu na wanakosea, na kwakufanya hivyo watanzania hao, wamechukua nafasi ya Mungu, na kujiona wao ndio wanaweza kuhukumu na sio Mungu, kama nikikumbuka vizuri Lowasa alishatubu tena na akaenda mbele zaidi kwa kuchukua maamuzi magumu na kuamua kujiuzuru wadhifa wake wa uwaziri mkuu.
Na Mungu alishatuambia hata kama dhambi zenu zilikuwa nyekundu kama bendera, zitakuwa nyeupe kama sufi, kwa maana hiyo Yeye ndiye anaye samehe na Yeye ndiye anaye hukumu, na msamaha wa Mungu unatatokana na pale tu, mtu anapotubu, na tukishatubu huwa tunaamini ya kwamba tumesamehewa, kwahiyo Mh Lowasa alishatubu na akaamini ya kwamba amesamehewa, sasa ni kwanini baadhi ya watanzania wanahukumu kitu ambacho kilishafanyiwa toba?
Watanzania wengi huwa hawajiamini, na kutokujiamini huwa inaleta woga, na woga ukikoma huleta chuki na wivu, tusipokuwa makini chuki na wivu ambao upo kwenye jamii leo hii, zitatuingiza kwenye migogoro isiyofaa, watanzania tubadilike, tuombee nchi yetu na tuombee viongozi wote pasipo kubagua, na mengine tumwachie Mungu.
Unaposema kwamba Lowassa alitubu ujumbe unaotoa ni kwamba kweli Lowassa alifanya makosa anayotuhumiwa kwa namna moja au nyingine. Unapotaka kuingiza suala la ubinadami na kudai eti Lowassa nae ni mwanadamu kama mwanadamu mwingine unatakiwa kwanza kufahamu ikiwa makosa anayotuhumiwa nayo ni makosa yanayotokana na upungufu wa kibinadamu au vinginevyo. Ikiwa kweli Lowassa alitubu kutokana na makosa ya ufisadi ambayo amekuwa akituhumiwa; ufisadi si moja ya makosa yanayotokana na mapungufu ya kibinadamu. Wewe huwezi kuwa muuaji halafu ukataka usamehewe kwa kuwa nawe ni mwanadamu kama mwanadamu mwingine wakati uuaji hautokani na mapungufu ya kibinadamu hususani kama uuaji wako haukusababishwa na mapungufu ya kibinadamu kama vile hasira ulipomkuta dume juu ya kifua cha mke wako na ukashindwa kuji-control na kufanya mauaji! Hasira ni makosa ya kibinadamu kwa maana hata kwenye elimu ya viumbe, tunaambiwa mwanadamu ana hormone zinazoitwa adrenaline hormones na hizi hormones zinapokuwa secreted/produces, automatically mwanadamu atajikuta anapandwa hasira! So, the more your body produces these hormones the more you become less control na hasira! You've no control on your hormones na ndio maana kosa litakalotokea hapo litahesabiwa ni la kibinadamu though it's not an excuse either!

And in addition, anapoamua kujiuzulu amefanya hivyo kuitikia utawala wake wa kiserikali na sio utawala wa wananchi ambao nasi tuna namna ya yetu ya kutoa hukumu tofauti na vile serikali inatekeleza hukumu zake! Vile vile, hata kama kweli alitubu na kusamehewa na Mungu, bado pia miliki ya Mungu ni tofauti na ile ya mwanadamu. Yeye ana namna yake ya kushughulikia wakosaji wake na sisi tuna namna yetu! Kwanini nimsamehe mtu kwa kigezo tu huenda amesamehewa na Mungu na what if I don't believe in God?
 
Siyo kwamba tunamchukia kama Lowassa, au kwa kuwa ana mvi, au kwa kuogopa uwezo wake wa uongozi; tunamchukia kwa sababu ya mawazo yake. Au tunaweza kusema, tunamchukia wizi, na kwa kuwa Lowassa ni mwizi, basi tunamchukia yeye na wizi wake.
 
... Anataka Kutuweka Mikononi Kwa Kutumia Hela Zake Za Wizi
 
sina wasiwasi kabisa na uchapakazi wa lowasa. tatizo lake moja tu, MWIZI.
Between hizo hela anazogawa kama njugu kazitoa wapi na zitarudije? Tafakari, chukua hatua.
weraufo
 
Last edited by a moderator:
wengine wafuata upepo,in short Lowassa ni mvumilivu sana,kapitia mengi na haya pia yatapita,tuhuma za kipuuzi zisijekutukosesha raisi tumtakae
TEAM lowassa
 
Last edited by a moderator:
Watu wengi humu wanaendeshwa na MIHEMUKO YAMKUMBO WA KISIASA na wanakundi yao, CHUKI ZAO SI KWA KUTOKUJUA SIFA ZA MGOMBEA A? BALI NI KUMCHAFUA A ILI WAMPAISHE WAO
 
Inaonekana huamini kuwa kila mtu ana utashi, hata Mungu anatawala kila kitu isipokuwa dhamira ya mwanadamu. Waache watu wachague cha kupenda na kuchukua si wamepewa watu 37 wa kuchagua mbona nachagua yule mkulima wa Kigoma japo sina hakika kama kamati kuu itanipa
 
Inasikitisha kuona kuna watanzania wenzetu wanalifanyia mzaha suala la urais. Wanaangalia ni nani ana hela nyingi ndio huyo wanaona anafaa kuwa rais. Hawajali kazipataje. Hawajali ana historia gani na mali za uma - kama ni mkwapuaji au la. Huwaoni humu wakiongea lolote jinsi ubunifu wake au biashara zake au jitihada zake zingine zilivyo muwezesha kuwa tajir. Hilo kwao mwiko. Hii hatari. Ndugu watanzania, adui wetu namba moja kwasasa ni uwizi. Kila zama na changamoto zake. Kwasasa changamoto namba moja ni hiyo - ufisadi. Tupigane kufa na kupona bosi wa sifa hizo asiende ikulu yetu. Haimaanishi wengine ni malaika - lahasha. Lakin watu hawafanani - people are never the same. Viwango vinatofautiana. Hata walokole kuna walokole wa zaid. Hata majambaz kuna yaliyopitiliza. Wengine ni mkumbo tu. Lakin wenyewe kama wenyewe wakipewa ukuu wa nchi nchi yetu itakaa sawa
 
Mtu akitubu anaacha kufanya dhambi. Kibaya zaidi ni kwamba Lowassa bado anaendelea na dhambi zake. Hizi pesa anazogawa kama njugu ili apitishwe kugombea anazitoa wapi? Je atazidudisha vip? Kwa mtu yeyote mwenye kufikiri ataona Lowasa ana agenda ya siri inayoweza kuligharimu taifa! ni hilo tu mkuu.
 
Lowassa asipopelekwa Mahakamani ili akahukumiwe kihalali ataendelea kuhukumiwa kavukavu mpaka atakapokuja kuhukumiwa na Mungu.
 
Wanaomtuhumu Lowasa kisa kachukua form ni vilaza tu na hata wachangiaji wengi wa JF wanaosapoti hilo ni vilaza tu coz kuna watia nia 40 ndani ya ccm na kati yao atapitishwa mmoja na wenye mamlaka ya kupitisha wagombea 5 ni cc yenye wajumbe 28 tu hivyo ni ujinga kuanza kumshambulia mtu mmoja as if ni yy tu asiefaa kati ya wagombea wote 40 kitu ambacho sio kweli.
Suala la kugawa pesa ni la kawaida kbs kwa uchaguzi hasa ndani ya ccm miaka yote ndio maana hata wabunge wa ccm ni wale wenye pesa tu ndo wanashindaga kwenye kura za maoni hivyhivyo kwa rais pia hilo loko wazi.
Kwa hiyo sioni busara kumshambulia Lowasa kisa alishawishi serikali iingie mkataba na richmond ambayo haikuwa na usajiri nchini marekani. Hilo ni kosa la kiuongozi ambalo linafanywa na viongozi kibao wa serikalini na wengine wapo bado serikalini na wengine wanatangaza nia lkn hakuna anaewaongolea kila mtu ni lowasa acheni cc ifanye kazi yake kelele za watu wa IQ ndogo km watangaza nia wanaoacha kuuza sera zao na kuanza kushambulia mtu haziwezi kubadili chochote kwenye cc ya ccm
 
Sijaelewa amehukumiwa vipi?
kwani ukiwa na makandokando watu wema wakakusema ndio hukumu?
badilika kaka, call a spade a spade!
 
Wanaomtuhumu Lowasa kisa kachukua form ni vilaza tu na hata wachangiaji wengi wa JF wanaosapoti hilo ni vilaza tu coz kuna watia nia 40 ndani ya ccm na kati yao atapitishwa mmoja na wenye mamlaka ya kupitisha wagombea 5 ni cc yenye wajumbe 28 tu hivyo ni ujinga kuanza kumshambulia mtu mmoja as if ni yy tu asiefaa kati ya wagombea wote 40 kitu ambacho sio kweli.
Suala la kugawa pesa ni la kawaida kbs kwa uchaguzi hasa ndani ya ccm miaka yote ndio maana hata wabunge wa ccm ni wale wenye pesa tu ndo wanashindaga kwenye kura za maoni hivyhivyo kwa rais pia hilo loko wazi.
Kwa hiyo sioni busara kumshambulia Lowasa kisa alishawishi serikali iingie mkataba na richmond ambayo haikuwa na usajiri nchini marekani. Hilo ni kosa la kiuongozi ambalo linafanywa na viongozi kibao wa serikalini na wengine wapo bado serikalini na wengine wanatangaza nia lkn hakuna anaewaongolea kila mtu ni lowasa acheni cc ifanye kazi yake kelele za watu wa IQ ndogo km watangaza nia wanaoacha kuuza sera zao na kuanza kushambulia mtu haziwezi kubadili chochote kwenye cc ya ccm
Mawazo yako saafi, kama ni kutokuwa na sifa za uongozi tuanze na yule mkulima toka kigoma maana hajawahi kuwa kiongozi.
 
Back
Top Bottom