Kwanini alimchagua yeye na si wengine?

EINSTEIN112

JF-Expert Member
Oct 26, 2018
21,713
35,525
DAVID: Beni Mshikaji wangu, mwezi wa nane nitafungua Ndoa. Me Ninaoa sasa.

BENI: Haa David, wewe na Monica Mnafunga Ndoa?

DAVID: Ndio Man, nimeamua nioe. Niko tayari sasa.

BENI: Mbona fasta hvyo Mwanangu. Si mwaka mmoja tu tokea mjuane na kuwa kwenye Mahusiano.

DAVID: Kwani Beni, Huchukua muda gani kumsoma Mwanamke?

BENI: Me sijui Man, ila kama naona mapema sana Kaka. Kwaio umeamua kabisa kulihama Chama la ma-seniour bachela. Unaanza maisha ya kurudi nyumbani mapema kuonana na mwanamke huyo huyo kila siku. Kusumbuliwa na maswali ya uko wapi, ulikuwa wapi!? Man, mapema mno aisee!

DAVID: Mshikaji wangu Beni. Mimi sio Mvulana tena bali ni Mwanaume sasa. Simaanishi ninyi sio Marafiki zangu tena, lakini Bro, maisha lazima yaendelee. Katika maisha yangu, Marafiki wamekuja na kuondoka, marafiki wamekuwa wa Msimu lakini familia siku zote hua inakuwa ni ya kudumu.

Nimefika katika point ya maisha ambayo nahitaji nitulie Beni, niwe na familia, niwajibike kwa watoto wangu na niwe na mtu wa ku-share nae mambo yangu ya ndani.

BENI: Dah. Sasa kwanini Umuoe Monica? Kwanini yeye na sio wale wengine uliokuwa nao? Angalia kwa mfano, Umekuwa katika mahusiano kwa miaka mitano na Doreen mkaachana. Lakini ku-date na Monica Mwaka mmoja tu tayari unataka kumuoa.

DAVID: Niliachana na Doreen kwa sababu ya wivu wake. Alikuwa akipenda kuwasikiliza marafiki zake kuliko mimi. Alikuwa ni mtu wa kubadilika mood, mara anune tu bila sababu za msingi, yani alikuwa hatabiriki. Kwakweli mimi nilishindwa. Sikuwa nahitaji kuja kuwa na familia na mtu wa aina hiyo. Sikuwa nahitaji Girlfriend, nlikuwa nahitaji Mke. Monica anatabirika, akikairika ujue kweli ulimuudhi au kuna mtu amemuudhi, ni rahisi mno kupendeka sio kama Doreen.

BENI: Vipi kuhusu Anna. Yule msichana Mrembo uliejuana nae kupitia Facebook?

DAVID: Aah mimi na yule hatukufika mbali sana. Alikuwa ni mwanamke anayependa mambo mazuri pekee. Nilikuja nikatafakari, nikagundua kuwa ni mtu anayependa vitu na sio mtu. Alivutiwa na mimi kwa sababu ya fedha, Mara kwa mara alikuwa akipenda nimpeleke dinner kwenye Migahawa mikubwa mikubwa. Kuomba omba hela ndio usiseme, karibia kila wiki lazima hela ya saloon initoke. Alikuwa ni wa gharama mno, kila kitu ilikuwa ni kuhusu yeye tu, hakuna alichojali kuhusu mimi. Kwakweli pale nilifeli Bro.

Na sio kwamba siwezi kumhudumia mwanamke, ama mimi ni Mbahili, hapana mzee, kuna muda unatakiwa uwe na mwanamke ambaye atakuelewa pale unapomwambia hali si nzuri avumilie basi awe tayari kujifunga mkanda.

Mwanamke kama monica, mpaka akuombe Hela ujue kweli anayo shida. Mara nyingi mimi mwenyewe huwa najistukia na kumwambia Mama hela hii hapa nenda saloon, au nenda kafanye shopping hata kama ana hela zake.

BENI: Aisee. Na je, vipi kuhusu Beatrice, Mamaa Bite. Mama mwenye Mzigo wake nyuma na Hips kama amechongwa. Yule aliyekuwa jirani yako.

DAVID: Aah yule alikuwa ni mwanamke asiye na shida na Mwanaume. Sijui kwa sababu ya kuwa na fedha sana Kwamba yeye anaona anajiweza kwa kila kitu. Kwaio ukiwa na mwanamke wa aina hiyo wewe kama Mwanaume hauongezi thamani yoyote kwake. Alikuwa ni mwanamke ambaye ni Feminism haswa, alikuwa akinipa order utafikiri nimekuwa kuruta wa Jeshi. Mara niletee hiki, mara fanya kile. Na siku nilipokaa nae chini na kumueleza hiyo tabia yake ndio ukawa mwisho wetu. Sihitaji mwanamke ambaye anajifanya kuwa Bosi wangu.

(Wote wakacheka)

BENI: Okey, Ok. Sawa mzee. Na Je, Christina, yule dada Mpole ambaye mara kwa Mara mlikuwa mnaenda kutembelea vituo vya watoto yatima pamoja.

DAVID: Bro, Christina alikuwa ni mdada mpole sana. Mimi na yeye nusura tuwe wachumba rasmi. Lakini kwake maana ya utii kwa mume ni kusema Ndio kwa kila kitu ntakachomwambia. Ni kama alikuwa akinisindikiza tu katika maisha yangu. Yaani aliifunga na kuificha sauti yake kabisaaa.

Tofauti na Monica, Huyu ukikosea jambo anakukosoa kwa heshima na adabu, anakueleza wazi hapa Bwana Mkubwa umekosea jirekebishe. Mzee unahitaji Mke ambaye atakuwa anaku-challenge kiungwana, sio Mke wa ndio mzee. Unahitaji kuwa na Life Partner, sio Mtumwa Mtiifu.

BENI: Basi kaka, Kati ya wote hao, Imani yangu na siku zote nilijua utakuja kufunga Ndoa na Marry. Yule dada ambaye anaimba kwaya Pale kanisani.

DAVID: (huku akicheka) Marry ni mwanamke mzuri, lakini kwa Ndoa hapana. Yule naona niseme kwamba Kanisa wala sio Mungu ndio viko Ndani yake. Yaani kwake Mchungaji wa Kanisani kwao ndio alikuwa kila kitu kwake.

Kila siku yupo Kanisani, kama sio Kanisani basi nyumbani kwa Mchungaji. Ukimueleza kitu hafikirii yeye kwanza, lazima aende kwanza kwa Papaa akaombe ushauri.

Ukimpigia simu Usiku unakuta yuko bize, ukimuuliza alikuwa anaongea na nani utasikia nlikua nafanya Maombi na Mchungaji. Kwenye mitandao yake ya kijamii yote picha ni za mchungaji wake tu, kimsingi mimi nisingeweza kuwa na mke ambaye anamsikiliza zaidi mchungaji wake kuliko Mume.

Lakini Kwa Monica ndio, ni Mtu wa Kanisani sana, lakini ratiba zake ziko vizuri tu, tunakutana tunajadiliana, anatoa mawazo yake, ananisikiliza, ananikosoa. Kimsingi napenda namna anavyoziendesha ratiba zake.

BENI: Bro, Naona kwa kweli umeshampata Mrs. Perfect wako. Yaani hauoni uzuri wowote kwa wanawake wengine.

DAVID: Nisikilize Beni, katika ishu za Life partner, unapopata mtu sahihi kwako siku zote anakuwa kama Jua, anaangaza kote kiasi kwamba huwezi kuiona hata nyota moja angani. Yani anakuwa ni kama SI unit ya kupima wanawake wote. Sio kwamba yeye ndio perfect kuliko wanawake wote! Hapana, ila ameutuliza moyo wangu.

(Wote wakacheka)
FB_IMG_1559227687972.jpeg
 
kwannn mkuu
Dah! Nimesoma story yote kwa ufasaha.

Linapokuja suala la kuoa, mwanaume muelewa hutuliza akili ili apate chaguzi sahihi litakalomfaa.

Kama ningekuwa mimi, ningemuoa Christina hapo.
 
Back
Top Bottom