uncle J4
Member
- Jan 2, 2018
- 25
- 28
Usishangae kwanini amekuacha na kwenda ila jiulize ujasiri kaupata wapi?
Ukishalijua hilo jichunguze kuona ulikosea wapi ama yeye alikosea wapi na ukishaligundua hilo basi usisononeke bali jipongeze kwani huenda ungebaki nae ungeumia..
Kwani ni kheri aombae msamaha mara kwa mara kwa kosa jipya kuliko aombae msamaha kila kukicha kwa kosa moja.
Ni sawa tumeumbwa kusamehe lakini maumivu ya moyo hayasahauliki hivyo ni vizuri kujifunza kutokana na makosa pasi na chuki ya kulipa kosa kwa kosa.
Kwani kushindwa si kupoteza bali ni hatua ya kuvifahamu vitu vipya na vizuri.
Jifunze:
Unaweza ukatumia MKONGO,
Kurejesha heshima iliyopotea kitandani..
Lakini ukashindwa kuutumia UBONGO,
Kila kukicha ukitafuta mchawi nani.
"KIFO huwa tayari kwa maradhi yasiyo na tiba"
@Uncle_J4