Kwanini ajira hakuna?

Kwani ukiwa na degree lazima upewe ajira? Acheni ujinga ninyi wasomi, ajira za kupewa hakuna duniani kote. Nendeni mashambani mkajiajiri kwa kulima.
Hizi akili hizi!
Nchi kama Japan,Korea,USA,na UK wana uchumi mkubwa mala 1000,ya wakwetu,lakini wanazungumzia ajira za wasomi wao wakitoka vyuoni! Sasa TZ ambayo bado hata kujitoshereza kwa bajeti yake haiwezi,unashangaa vijana kutaka wapewe ajira!
Kama hao wakubwa na elimu yao nzuri,wanayotoa bado wasomi wao wanatafuta ajira za umma,sembuse sie! Acha kuwa mchawi!
Unafikiri kusomea shahada ya kwanza ni sawa na kuendesha boda bora au kutumia simu janja!
Wewe kama ulisoma hesabu za aljebra darasa LA saba,ukafikiri ndio mwisho wa hesabu,kuna kitu kinaitwa Engineering mathematics!
 
Kwani ukiwa na degree lazima upewe ajira? Acheni ujinga ninyi wasomi, ajira za kupewa hakuna duniani kote. Nendeni mashambani mkajiajiri kwa kulima.
Mbaya zaidi waonaosema haya maneno na wenyewe hua wameajiriwa , hawajawahi kuwaza au kujiajiri hata siku moja
 
Fafanua hiyo green house ya mtaji wa laki moja!! Kweli masikini akipata mata.ko ulia mbwata
 
Unafikiri kusomea shahada ya kwanza ni sawa na kuendesha boda bora au kutumia simu janja!
Wewe kama ulisoma hesabu za aljebra darasa LA saba,ukafikiri ndio mwisho wa hesabu,kuna kitu kinaitwa Engineering mathematics!
Pumbavu! Sasa kama wewe ulisoma zaidi ya aljebra umeshindwa vipi kujitegemea? Mbona sisi wa aljebra tunaishi maisha yeti hatulii kama wewe?

Halafu we mjinga hebu tega sikio nikwamboe kitu. Huko kwenye mataifa uliyoyataja hakuna ardhi kubwa yenye rutuba kama iliyopo Tanzania.

Kwahiyo kwa msomi aliyeelimika hapa Tanzania anapomaliza chuo tayari anakuwa na mitaji 3 ya kujiqjiri:- nguvu zake, elimu yake, na ardhi tele yenye rutuba inayopatikaa bure ktk mikoa ya Tanga, Katavi, na Tabora.

Ukiendelea na mawazo haya utadeki choo na kufua nguo za shemeji yako mpk uzeeke
 
Akili nyingi🕴️
 
Ajira nyingi zingetokana na wingi wa wajasili mali wadogo wadogo.
Tungetegemea benki zetu kwa kushirikiana na serikali iache kupuuzia entrepreneur hao.

Kwa mfano katika mega projects za Raisi Magufuli kama angekuna kichwa na wabobezi wa uchumi akatenga Trillion 6 kwa miradi ya wajasili kwa wastani wa sh milioni 1 kila mradi, ni wastani wa miradi milioni 6 siyo haba.

Hao wajasili mali wakiweza kurudisha mkopo huo na riba ndogo baada ya miaka mitatu tunaweza kutengeneza miradi mingine midogo midogo milioni 6.hivyo kwa kipindi kidogo cha miaka 6 tutakuwa na miradi midogo midogo milioni 12.

Watu ndio uchumi, ukiwezesha watu,hao watu ndio wanatengeneza uchumi.
Hata hiyo mega projects za Raisi Magufuli itakuwa rahisi sana kuijenga kutokana na wingi wa walipa kodi.
 

Herla zote zinaelkezwa kwneey SGR, Nyerere DAM, Ndege.
 
Ajira zote zilizopo huzioni?
 
Toka Sumaye akiwa PM mikopo midogo midogo imekuwa ikitolewa kwa vijana na akina mama, na baadae walemavu nao wameongezwa ukiangalia impact kwa ni ndogo sana.

Mfumo wa ajira ambao haupo kwenye organized sector ambayo watu wanazalisha, wanatengeneza faida, wanalipana mishahara, wanachangia mifuko ya pensheni kwa mishahara yao na kukua kwenye profession hadi kufikia apex ya fani/kada aliyopo. Ni muujiza mkubwa kwa mmachinga, bodododa kuweza kukua hadi kufikia apex ya maisha bora na anapostaafu at 60 years akapata pensheni.

Waajiriwa kwenye organized sector ndiyo wame-breed NSSF,NHIF, PPF, PSPF, LAPF na GEPF (ambazo sasa zimezaa PSSSF).
Wamachinga na bodaboda ni wengi sana kuliko wachangiaji wa iliyokuwa PPF; ila kwa kuwa ni unorganized society sio rahisi tukajenge uchumi endelevu kupitia watu kama hawa.

Moja ya namna ya kutengeneza ajira, jibu alitoa JPM wakati wa mkutano wa SADC 2019.

Kuna sehemu ya ajira tunazipeleka Ulaya kwa kuuza raw materials; wakati tungetengeneza consumable goods, tungetengeza ajira za kutosha
Your browser is not able to display this video.
 
Mkuu wewe mwenyewe unakili hiyo misaada haijaleta impact kwa sababu haikufanyiwa upembuzi yakinifu.
Lakini mkuu kama nguvu kazi tugeitumia kwa mfano ukulima wa tractor na pembejeo kama ulimaji wa miwa na utengenezaji wa sukari ya viwanda vidogo ingeleta impact na zaidi ya hapo tusingekuwa na tatizo la sukari.
Au kama wangepewa mikopo ya kununua ngombe wa maziwa,wakafuga tukapata maziwa ya kutosha.Sio siri ni watanzania wachache wanakunywa maziwa au hata chai ya maziwa ukilinganisha na Kenya.
Kwa kilimo tuna fursa nyingi hadi samaki wa kufugwa kama prawns n.k
Hiyo miradi haikupewa kipaumbele, laiti ingepewa kipaumbele vijana wasio na kipato waliokuwa vijiji wangekaa huko huko wala usingekuwa na lundo la machinga mjini.
Nina imani ingeleta impact.
Kwa sasa machinga ni mtaji wa kisiasa kwa wanasiasa tu wanaowatumia kwa maslahi yao tu.
Hizo habari za kwamba tunapeleka Ulaya raw material ndio tatizo is too theoretical kama tunajua hilo mbona hatujachukuwa hatua za msingi?
Mfano hai ni Tanganyika Packers ikizalisha nyama ya makopo kupeleka nchi za nje leo imegeuka kanisa la Mwaiposa!!
Mifano ni mingi.
 
Wasomi wengi wanategemea kazi za shati nyeupe, swali ni je mfumo uliopo unazalisha hizo kazi kwa kasi ya kuendana na kuzalisha wahitimu wa vyuo ama tumekalia kuimba “tuko pazuri, tutembee kifua mbele????


Sent using Jamii Forums mobile app
 

Wao si wakalime tuone au wanasema vijana mjiajiri wakati pesa zao wameweka overseas kwenye fixed desposit.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mbona kazi zipo tu kibao? Degree yako inatakiwa ikusaidie kuona fursa zilizopo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…