Hili jibu bado haliridhishi, narudia swali la mleta mada, kwanini isiwe waziri anayehusika na mazingira badala yake akapelekwa waziri anayehusika na gesi?
Habari ya kusema kwa hapa ndani, hapo sikuelewi zaidi, ina maana ndani Rais ndio anafuata taratibu, lakini nje anavuruga atakavyo?
Tusikwepe ukweli hapa, Rais hamuamini Jaffo, kama anamuamini angemtuma yeye, na hiki alichofanya amekosea, ndio anazidi kuwafanya hawa jamaa wengine wazidi kujiona wajuaji, anatengeneza makundi kwenye baraza lake la mawaziri bila kujua.