Kwani ujinga ni nini?

Kwani ujinga ni nini?

NAMDORY

Member
Joined
Feb 21, 2017
Posts
35
Reaction score
23
Kwani ujinga ni nini?

Denis Mpagaze
________________

1. Ujinga ni mtu bila akili. Mtu bila akili ni mwenda wazimu.

2. Taifa lenye wajinga wengi ni mzigo kwa walipa kodi.

3. Ujinga unafanya watu wasiwe watu wa maana. Wanakuwa watu wa hovyo.

4. Mtu ni akili. Mtu bila akili ni mwehu. Mtu bila akili ni mkurupukaji! Hana mipango! Yeye ana matukio! Tena ya ghafla!

5. Ujinga uchi kuwa uchi akilini. Huu uchi mbaya kuliko uchi wa kawaida.

6. Ujinga ni kufanya jambo lilelile kwa kutumia njia zile zile ukitegemea matokeo tofauti.

7. Unaogopa kuonekana wa tofauti, unafurahi kuonekana wa kawaida.Huo ni ujinga sugu

8. Ukiona mtu kafanikiwa jua kuna jambo la tofauti kafanya! Be different bro if you want kutoboa!

9. Ujinga ni kulazimisha kufanana na wenzako na wakati Mungu kakuumba tofauti.

10. Duniani tuko watu bilioni saba na ushehe lakini madole gumba yetu yanatofautiana. Hii maana yake ni nini?

11. Maana yake ni kwamba kutaka kufanana na mwenzako ni kumdharau aliyekuumba tofauti!

12. Ujinga ni kujifanya unazo kwenye hamna! Unaishi maisha ya mboga saba kwenye nyumba ya kupanga.

13. Unalazimisha kuzaa mapacha na wakati mimba ni moja.

14. Sikiliza! *Ukiiga kunya kwa tembo utachanika huko nyuma🫢🫢

15. Ujinga ni kununa kwa sababu hajakupost kwenye ukurasa wake wa instagranu.

16. Si kila anayepostiwa anapendwa ndiyo maana hata kwenye kopo la sumu ya panya kuna picha ya panya.

17. Sasa unataka kuniambia hapo panya anapendwa? Wakati mwingine tunapost panya dada!

18. Ujinga ni sehemu ya unafiki na ushenzi. Unasema unampenda halafu akiondoka unamponda.

19. Baada ya mke na watoto wake kwenda kusalimia wazazi wake kijijini akamuandika meseji mchepuko wake, Njoo mpenzi leo kiwingu hakipo meseji ikaenda kwa mama mkwe!

20. Hapo ndo utajua kwa nini jogoo anabaka hadharani na hachukuliwa hatua.

21. Ujinga ni kutaka watu wapost kile unachotaka kuona, wakipost tofauti unaleft group! Jifunze kukubali kutokubaliana! Acha ujinga.

22. Ujinga ni kuutesa moyo kwa kusubiri vya kupewa na wakati maisha ni kutafuta cha kupewa ni kaburi.

23. Ujinga ni kutamani kwenda mbinguni na wakati unaogopa kufa.

24. Ni sawa na kuomba Mungu akupe miaka mingi na heri duniani na wakati unaukataa uzee! Unapaka black.

25. Sikiliza, uzee haundoki kwa kupaka piko! Uzee haundoki kwa kuvaa wigi. Uzee unaondoka kwa kubadili hisia.

26. Ujinga ni kumwamsha mgonjwa umpe dawa ya usingizi.

27. Yaani ni sawa na kusema kazi iendelee na wakati huna kazi. Hii inachekesha kweli!

28. Ujinga ni kutangaza fulani ana ngoma na wakati wewe umekimbia majibu! Unaogopa kupima! Ujinga ni nusu kaputi.

29. Yaani hii ni sawa na kuchukia kwa nini ulizaliwa lakini unampenda aliyekuzaa, mama yako. Ajabu!

30. Ujinga ni kutojielewa kama wewe ni mjinga ukatibiwe. Uzuri ujinga unapona kwa sababu ni ugonjwa alisema Nyerere.

31. Ugonjwa ukitibiwa unapona, mjinga akielimishwa ujinga wake humtoka.

32. Upumbafu ndio hautibiki. Huo ni kama kipaji hautoki alisema Nyerere.
 
Back
Top Bottom