Kwani tume ya uchaguzi wanaweza kumkata tena?

Babu Kijiwe

JF-Expert Member
Joined
Mar 31, 2010
Posts
4,845
Reaction score
4,776
Miongoni mwa mambo aliyo ongea leo jaji Lubuva ni kuhusu ratiba ya kuchukua form za urais na ubunge toka tume ya uchaguzi, ninachotaka kujua ni kwamba tume ya taifa ya uchaguzi inaweza kukata jina la mgombea fulani kwasababu yoyote ile? Kama ndiyo, mkatwa asipo ridhika inakuwaje? Nauliza hivi kwakuwa nauchungu sana maana alikatwa kule akaja huku sasa wasije wakamkata na huku, kama wakimkata tena ctapiga kura ng'oo!
 
Mtu Akatwi Mara Mbili.Kama Akikatwa Ni Mengine Yanatafutwa, Na Watanzania Hawapo Tayari Kuona Haki ya Mtu Inapotea Pasipo Sababu

za Kimsingi. Kilchobaki Hapo ni Kujipanga Kikakati ili Sanduku la Kura Liseme Lenyewe. Kukubali Matokeo Halali Ndio Uungwana na

Ukomavu wa Demokrasia.Lakini Pia Kwa Mgombea yoyote Kukubali Matokeo Yaliyochakachuliwa Ni Ujinga na Kutojitambua.

So Haki Tutaomba Itawale Kila Hatua ya Mchakato Huu Muhimu.
 
Miongoni mwa mambo aliyo ongea leo jaji Lubuva ni kuhusu ratiba ya kuchukua form za urais na ubunge toka tume ya uchaguzi, ninachotaka kujua ni kwamba tume ya taifa ya uchaguzi inaweza kukata jina la mgombea fulani kwasababu yoyote ile? Kama ndiyo, mkatwa asipo ridhika inakuwaje? Nauliza hivi kwakuwa nauchungu sana maana alikatwa kule akaja huku sasa wasije wakamkata na huku, kama wakimkata tena ctapiga kura ng'oo!

Kama hatakidhi vigezo itakuwa ngumu kupitishwa, mfano kama alishawahi kupatikana na jinai mahakamani kama kupigana hadharani. Pia kama hajatimiza vigezo vya katiba ya chama husika, kama mhusika hana akili timamu mfano mtu mwenye kiharusi sijui kama nae anakuwa na akili timamu.
 
Nafikiri UKAWA wanatakiwa wawe na plan B hawa watu wa tume hawaaminiki wanaongozwa kwa remote.
 
kweli! hawawezi kukata kipenzi cha watu.
 
Miongoni mwa mambo aliyo ongea leo jaji Lubuva ni kuhusu ratiba ya kuchukua form za urais na ubunge toka tume ya uchaguzi, ninachotaka kujua ni kwamba tume ya taifa ya uchaguzi inaweza kukata jina la mgombea fulani kwasababu yoyote ile? Kama ndiyo, mkatwa asipo ridhika inakuwaje? Nauliza hivi kwakuwa nauchungu sana maana alikatwa kule akaja huku sasa wasije wakamkata na huku, kama wakimkata tena ctapiga kura ng'oo!

Hawawezi, labda wamkate Mungu kwanza. Mungu ndiye alikusudia kuleta mabadiliko.
 
Wee binadamu gani usie muogopa MUNGU?Uunapata wapi ujasili huo "eti wamkate Mungu kwanza ....utubu haraka vinginevyo MUNGU wa mbingu na dunia hii anakutizama kwa karibu...naomba usicheze na MUNGU wetu aliye hai...chunga sana ulimi wako na kamwe usichanganye mambo
 
Back
Top Bottom