Kwani Simba kuchukua ubingwa ni mpaka Yanga wawe wabovu (watembeze bakuli)? Ni aibu

Will Jr

JF-Expert Member
Jul 21, 2018
4,661
6,579
Wasalaam!

Yaah! Wote tunaelewa nyakati zinabadilika sana, Yanga inavyobadilika na mpira wa bongo unabadilika, Kutoka kwa Manji to bakuli now kwa GSM, nakumbuka kipindi Yanga wanatembeza bakuli faraja yao kubwa ilikuwa kuwafunga Mikia, lakini Yanga kuwafunga Mikia sio habari, washazoea. Habari huwa ni side B kupindua meza. So ni kama meza imegeuka, uzuri kwa sasa Yanga wanafanya haya huku lile chama likiwa bado chini ya mikono ya tajiri kijana Afrika, so what went wrong?

Ukiuliza mafanikio ya upande wa pili msimu huu utaambiwa ni kuwafunga Wananchi 2-0, kila shabiki anajigamba kwa ushindi wa msimu huu, of course inaleta faraja, inaonesha kuna kitu kilifanyika msimu huu, msimu haukuisha burebure tu.

Lakini kwanini chama kubwa la kidunia lenye maskauti kutoka uholanzi, makocha wa kibrazil waliocheza na Mario zagallo & Pele dos Santos linatapata tabu kuchukua ubingwa mbele Yanga hii?

Ukizingatia chama kubwa lina kila kitu, kuanzia pesa, wachezaji bora wanaoweza kuwaweka benchi kina Sadio Mane, manguli wa masuala ya usajili kumzidi Monchi, benchi bora la ufundi na ufundi wa kijadi pia. Je Mikia tusubiri paka GSM awakache Yanga ndio tuchukue taji?

This is inferiority complex, this is unacceptable, this is not the way, this is embarrassment. Ebu ndugu zangu Mikia na JF tacticos tutililike nini kinazuia ubingwa kwenye mto ule? Wote tupo hapa kujifunza michongo mipya ya kimpira. Asante.
 
Nishasahau ebu nikumbushe Bakuli mmetembeza misimu mingapi?

Kwasababu Simba imechukua 4 times back to back.
 
Back
Top Bottom