GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 56,548
- 108,882
Siku zingine Watu wenye umakini na jambo fulani wakiwa wanaandika na kushauri hapa msiwe wepesi sana wa Kutukana au Kudhihaki na badala yake muwe mnayasoma vizuri, kuyatafakari na hasa muyafanyie Kazi kwani kuna Binadamu wengine tumenyimwa tu Pesa na Mali ila Maono na Upeo wa hali ya juu Mwenyezi Mungu alitutunuku kama siyo kutubariki nao.
Wiki kama mbili zimeshapita sasa hapa hapa Jamvini nilikuja na Uchambuzi wangu wa Kiangalizo / Kiushauri kabisa kuihusu Klabu yangu ' pendwa ' kabisa ya Simba na hasa katika mechi zake hizi za Makundi ambazo imepangwa na Timu ngumu ila nilichoambulia ni dhihaka, matusi, kejeli huku nikibatizwa kwa lazima kuwa Mimi GENTAMYCINE ANTIBIOUTIQUE ni Yanga dam dam / kindakindaki.
Narudia tena leo japo najua wote tunaumia kwa Kipigo cha Kishalubela / Kikatili cha Kufungwa Goli 5 kwa Sifuri na AS Vita Club japo bado Watani zetu Yanga SC wanashikilia rekodi yao ya Kubugizwa / Kufungwa Goli 6 kwa Sifuri mwaka 1998 pale walipocheza na Klabu ya Raja Casablanca ya Morocco japo hata leo ilikuwa kidogo tu na Sisi Simba SC tuivunje hiyo rekodi kama si papara za Mafowadi wa AS Vita Club. Shukran kwake Maulana / Mola kwa hizo Goli Gwala / Tano.
Tuacheni Unafiki wala Kuficha ukweli hapa kwamba kwa Kikosi hiki cha Simba SC tusitegemee makubwa yoyote bali tuzitumie hizi mechi zetu Sita katika kujipatia tu uzoefu na pia Kujitangaza hasa kwa Wachezaji wetu baadhi wenye uwezo ili tuwauze, Timu ipate Pesa na tukijenge zaidi Kikosi chetu kwa Mashindano yajayo kama kwa Msimu huu tutachukua tena Ubingwa wa TPL japo dalili hizo sizioni kwakuwa hata Yanga SC na Azam nao bila kumsahau KMC Kimahesabu wana uwezo wa kuwa Mabingwa vile vile.
Kiufundi na najua kwa hili Wanasimba wengi mtanishangaa ila najua wale Wenzangu tuliocheza mpira hata kidogo au Wachambuzi na Wafuatiliaji wazuri watakubaliana nami kuwa kama kuna Mchezaji ambaye kwa leo pale Kinshasa ameigharimu Timu ' Dearly ' kabisa ni ' Kipenzi ' cha wengi kwa sasa Mchezaji Clatous Chota Chama.
Niliwahi kusema hapa hapa kwamba Chama ni Mchezaji mzuri ila Kiuzoefu zaidi Mimi nilikuwa napendelea sana mbele ya Mkude na Kotei awepo ama Haruna Niyonzima au Hassan Dilunga kisha Kipindi cha pili ndipo Chama awe anaingizwa au badi Kocha ' Uchebe ' Patrick Aussems abadili mfumo ili awe anamtumia Chama kama Kiungo wa Pembeni au amuanzishe pamoja na Niyonzima au Dilunga.
Mechi ya leo Chama ameigharimu Timu kabisa na muda mwingi alikuwa anacheza ' Kibishoo ' mno huku mara kwa mara akipoteza umakini wake na alisahau kuwa pale Simba SC tulikuwa ugenini na tulihitaji Ushindi pekee na siyo zile ' Mbwembwe ' zake ambazo amezoea Kuzitoa akiwa ' Kwa Mchina Stadium ' kisha Mashabiki wote ' wanatapika ' Uwanjani na Kumsifu huku akijiona Yeye ni Iniesta au Zidane wakati bado ni wa kawaida sana tu ila ' Kibongobongo ' anaonekana ni Mfalme.
Timu leo imefungwa kwa sababu nyingi sana ila Kubwa ni Saikolojia ya Wachezaji wa Simba SC, Wachezaji Kujisahau, Kulewa Sifa, Uzembe wa Kujirudia kwa Mabeki, Kiungo chote Kufichwa kama siyo Kufunikwa na Viungo wa AS Vita Club na Kujiona sasa kwamba wameshamaliza na wamechukua Ubingwa wa Klabu Bingwa Afrika tayari wakati ukweli ni kwamba hata 25% ya kuyafikia hayo Mafanikio bado.
Nilionya ila sikueleweka vyema kuwa hakuna Beki ambaye Mimi hadi hivi leo sikupendezwa na Usajili wake kama Pascal Serge Wawa na Kuhoji ni kwanini Kocha Aussems alikuwa hapendi Kumtumia Beki mahiri na ninayemkubali kwa 100% Juuko Murshid kiasi kwamba Kukaa Kwake Mkeka / Benchi Kumeathiri mno Kiwango chake japo kidogo sasa kinarejea.
Nakumbuka nilisema kuwa kama Siku Simba SC itacheza na Azam FC na kwa aina ya Mafowadi wa Azam FC akina Chirwa na Ngoma walivyo na kama Simba SC tutampanga Beki Pascal Serge Wawa basi Siku hiyo Chirwa na Ngoma watakuwa wanaingia nyavuni ( wanafunga wanavyotaka ) na tutaaibika na kutafuta wapi tufiche Sura zetu hizi ngumu na zilizokomaa utadhani Kisigino cha Nyati.
Simba SC haiwezi Kushinda na Kufika mbali na Kikosi cha Wachezaji kama Wawa ambaye ni mzito, Mohammed Hussein Zimbwe Jr ambaye hana ubavu / nguvu za kuweza Kupambana na Mawinga machachari wa Timu pinzani na ndiyo maana kama umegundua Mechi nyingi Simba ilizofungwa Magoli mengi yalipitia Kwake.
Simba SC ya Fowadi kama John Boko ambaye ameshapoteza ule uwezo wake bora pamoja na akina Salamba huku ikiwa imesajili ' Kishamba ' kabisa Beki mzigo Zana Coulibaly kutoka Burkina Faso na hadi hivi leo haina Kocha Msaidizi ni dhahiri shahiri kwamba tusijidanganye tutafanikiwa bali tuendelee tu Kujiandaa Kisaikolojia kwa lolote litakalotutokea huko mbeleni. Kama leo AS Vita Club ametufunga Goli 5 vipi Siku tukikutana na wale wanaojua hata kuliko AS Vita Club hawa akina Al Ahly ya Misri? Kwa mpira huu wa Kipuuzi na Kitoto Simba SC tuliocheza leo kama tukicheza hivi hivi pia na Al Ahly kuna hatari ya Kufungwa kati ya Goli 13 hadi 17.
Ili Simba SC ifanye vizuri basi ivunje Benki yake na isajili Wachezaji wakubwa, wazuri na mahiri mno ambao wataweza Kushindana na Wenzao wanaofanana nao Kiuwezo na siyo hawa ' School Boys ' waliopo sasa. Timu isajili Wachezaji wenye Uwezo wa kama akina Okwi, Kagere, Chama, Murshid, Makambo, Walter Bwalya, Ronald Kampamba na wengineo ili iweze Kushiriki vyema Kimataifa tofauti na hapo tutaendelea tu Kujidanganya na Ubingwa Wetu wa Kuwafunga akina Ndanda FC, Stand United na Mbeya City au Lipuli FC.
Poleni sana Wana Simba SC wenzangu ila kwakweli leo akina Bandeko Nangai ( Wakongo ) wametuaibisha mno huku wakituchezea Mpira mwingi na pia hapo hapo Wakitufundisha Kucheza Mpira ili tukirejea Dar es Salaam Tanzania tuweze Kuwafuna akina Coastal Union na KMC. Namuonea huruma mno Msemaji wa Simba SC Haji Manara kwani kiukweli Simba tumeshafungwa sana tu hadi Kuzoea ila hii ya Kupigwa ' Hamsa / Tano ' tena kwa Sifuri limetuaibisha na kutudhalilisha kabisa.
Nawasilisha.