Simulizi zinasema kuna watu waliwahi kupachezea na kuzindika mambo yao, hivyo kuna mambo ukiyafanya kinyume.. Yaani ndivyo sivyo inakula kwako mbaya
Usiku kiza kikiingia na watu wakienda kulala, mizimu vinyamkera na yale maroho huingia kazini
Kuna simulizi pia za kupelekewa moto vibaya Sana, na hii ilitokea sana kipindi kile kabla ya yule aliendoka wa mwisho! Wanasema ilikuwa hakuna kulala
Hata hivyo location pia inaweza kuwa ni tatizo kubwa.. Pale ni sawa na madhabahu takatifu pakichezewa kidogo tu pakanajisika, basi midude ikichoka kukaa kwenye maji makuu huenda pale kaka ufukweni pao kubarizi
Hiyo midude wanasema haina show za kitoto hasa kuanzia saasaba mpakasaatisa.. Ni kama vile yanaliteka eneo lote kwa muda hakuna kutoka mtu Ila kuingia ruksa
Nilishawahi kuishi nyumba ya namna hiyo Tanga. Wenyeji wakaniambia hapo pazito usipaone hivyo, hakikisha hupachafui kiroho.. Na siku ukienda kuchafuka nje hakikisha unakuwa msafi kabla hujaingia ndani
Weekend moja nikapita chocho moja lenye mitungi na mikasi.. Nikaifurahisha nafsi mpaka karibia siku kupinduka ndio nikarudi kwangu..Si nikajisahau kujitakasa!
Nikaingia ndani nikatia komeo nikalala fofofoo fool!
Nane usiku nikastuka na kuona chumba chote kina mwanga.. Kucheki taa haiwaki. Nikadhani ni wenge la mitungi tuu. Kabla sijakaa sawa mwanga ule ukapotea na nikahisi kabisa pale chumbani (sio kitandani) siko pekeyangu
Vituko vilivyoendelea baada ya pale mpaka alfajiri kabla ya adhana ya kwanza sitakaa nivisahau
Hapa pa sasa pamechafuliwa na kunajisiwa vibaya Sana! Sio pasafi na hapana utukufu tena
Yale madude yameshapageuza kiwanja chao cha kudumu.. Na mizimu imeruhusu. Hivyo hapakaliki hapalaliki!
Falme mbili hazikai pamoja hasa ufalme wa nuru na ufalme wa giza ni lazima zitasigana! Ukivaa joho jeupe nje lakini ndani umefutika uvundo lazima usande
Wapangaji waliotangulia walitumia damu kubwa kwa uchache na kwa uangalifu mkubwa ndio maana walau walivumiliwa kiasi chake
Washauri wabaya na vipotoshi waliosema itumike damu kubwa halafu nyingi ndio wameharibu kabisa
Mwangi, miito, vilio na taswira za wenye damu zao zinawaandama kila wakitia miguu yao! Panatisha Sana na kuogopesha Sana!
Ukimuona baba kahama kwenye mjumba wake wat maana hata kama ni wa kupanga na kwenda kuishi uswazi kwenye nyumba ndogo sometimes usimkejeli bali muonee huruma! Ana mazito na magumu moyoni
Good morning Tanganyika!
View attachment 3526449