Kwani ni tatizo la ngozi yangu tu?

kiben10

JF-Expert Member
Apr 28, 2018
616
789
Vijana wenzangu, wazee na watoto ambao mmewahi kuota ndevu za KWAPANI, CHINI, NDEVU & KICHWANI napenda kuwasilisha jambo hili kwenu kama mko na Experience ya ari hii ambayo mimi inanikumba kwa zaidi wa 3weeks sasa.

Nimenununua 1pc ya Nyembe 6 za company ya RUNGU, ila tangu nimeanza kujinyoa maeneo mbalimbali ile siku hadi leo ni 3weeks bado nawashwa maeneo yote tena kwa kujikuna balaa na hata kuwa na vipele vinavyopelekea vidonda. Sasa naomba kuwauliza pia nanyi wenzangu Je?

Mko na experince ya ari hii manvyotumia RUNGU wembe or ni mimi tu na Ngozi yangu?

Cc Mshana Jr
 
Watu tunatofautiana kwenye masuala ya ngozi kinachofaa kwa mwingine huwenda kikawa tatizo kwako.

Lakini Kama ulikuwa unatumia nyembe siku zote ila za Sasa ndiyo zimekuwa tatizo huwenda hazina ubora/makali ya kutosha.

Katika kukata nywele haitakiwi ku disturb ngozi kikatio kiikosa makali Ni lazima uumize ngozi na matokeo ndiyo hayo ya kutoka mapele
 
Seli za ngozi yako zimechoka maeneo zinazoota nywele kwa kukwanguliwa Mara kwa Mara. Unaweza tumia dawa ya kuripea. Ukikosa utanicheki kwa 0713039875
 
Mkuu kuna mashine za kisasa za kunyolea ndevu na vinyweleo, achana na hizo nyembe, sijui rungu labda kama huna uwezo wa kuzinunua, bei ni kati ya laki 2 na laki 3.
 
Utakuwa na mzio na hizo bati zilizochongwa lakini pia hiyo kampuni bidhaa zake nyingi sio best quality...nakushauri tumia bic au gilet
Kwa tatizo la sasa ukienda kuoga sugua hivyo vipele na mswaki baada ya hapo paka limau au ndimu vitakauka vyote
 
Usikwangue na wembe kwa kutumia nguvu nyingi, bali kwangua kama unapangusa vile. Zipo sababu za kisayansi.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom