MAHENDEKA
JF-Expert Member
- Jul 9, 2010
- 337
- 179
Habari za mwaka mpya wanajamii wenzangu ,natumai mu wazima mwaka huu tumevuka salama
Ni mara ya kwanza najitokeza jukwaa hili kuomba ushauri au msaada wa matatizo yanayonisibu mwenzenu
Umri wangu ni takribani miaka 29,nilizaliwa tarehe 22 septemba 1986, toka nizaliwe nimekua nakabiliwa na matatizo mawili sugu ambayo ni kama yanakwenda sambamba hivi
Tatizo la kwanza ni ugonjwa wa ngozi na tatizo la pili ni ugonjwa wa kifua asthma,matatizo haya kwa mujibu wa wazazi wangu yalianza nilipokua na wiki 2 tu tangu nizaliwe.
Mama ananiambia wiki chache tu baada ya kunizaa nilianza kutokwa na vipele vidogo-vidogo vingi mwili mzima nikawa najikuna sana kiasi kwamba siwezi hata kulala,nikawa najikuna na ngozi yangu kubadilika na kua kama tofali la simenti na mara ghafla nikaanza kubanwa na kifua asthma
Kwa matatizo haya mawili wazazi wangu wamejaribu kila namna wanayoweza bila mafanikio yeyote,au kwa.kifupi naweza sema matatizo yangu yamewafilisi.,wamepoteza fedha nyingi sana mpaka uzee wao huu hawajafanikiwa kupata tiba ya tatizo langu japo mmoja kashatangulia mbele ya haki R.I.P,hospitali zote za rufaa hapa nchini nimeshapelekwa bila.mafanikio
Kwa kifua nimeshachomwa sindano nadhani nmemaliza zote, cristapen,sijui hydrocotizone zile.sindano zinazovuta dawa zenyewe kulingana na mapigo ya moyo zote nmechoma,dawa za kumeza nmekunywa sana aminophiline,ephedrine,predinisalone na franol zipo nyingi nyingine nimezisahau majina,nmeshatumia dawa za kupuliza kinywani pindi napohisi kifua kama kinataka kubana(obvious ni wakati wa mawingu mawingu kama mvua inataka kunyesha kuna feelings fulani nazipata na kujua kabisa kifua changu hakiko vizuri)..Lakini pamoja na hayo naumwa kifua ambacho kina maajabu kidogo nikibanwa kifua nikikaa kwenye baridi au upepo ndo napata nafuu,sijawahi sikia hii lakini kwangu ndivyo ilivyo!!
Pili naumwa kifua lakini naweza kimbia riadha hata kilometa saba kwenda na kurudi na.nikawa vizuri tu,lakini siku kikiamua kubana kimeamuana,na kinabana.hasa mtu akibahatika kuniona anajua nakufa,kifua kikinibana siwezi kukaaa wima inanibidi nijikunje kidogo ili niweze kupumua na.sivyo hewa inakua kama.inakata,na kikipona nakua naumwa sana mgongo na mbavu( sababu ya kupumua kwa shida )
Watu wanasema na aleji lakini nmejaribu kutafuta na aleji na kitu gani miaka takribani 10 ya kujielewa kwangu laini sijafanikiwa kujua na aleji na.kitu gani ?
Ugonjwa wa pili ni ngozi,hii inanisumbua sana najikuna kila mara,mpaka mbele za watu,na nikikuna mahala panapowasha kunatokea vipele baadae vipele vinatengeneza kibalango ambacho kinatoa majimaji na kuwasha zaidi na kusambaa kwa kadri navyozidi kujikuna ndivyo ugonjwa unavyozidi kusambaaa kwa kasi nikizidi jikuna ndivyo panavyozidi kua sugu na kutengeneza kama alama nyeusi yenye mapele makubwa zaidi yenye majimaji yaani hali ni mbaya
Nmeshaenda hospitali maana huu ni ugonjwa wangu wa muda mrefu sana,zamani ulikua mwili mzima,lakini ukapungua wenyewe na.kubaki sehemu sehemu za maungio ya mwili lakini sasa unarudi tena,nawashwa mpaka usoni nikijikuna mabalango yananitokea,najaribu kufikiria ntakua mtu wa aina gani sasa?
Nmeenda hospitali nmepewa dawa za aina mbalimbali kuna mafuta ya kupaka lakini hola,nmepewa dawa za tube za kupaka kama safi cream lakini wapi
Mwisho.wa siku nmejaribu kutumia dawa inaitwa gentriderm cream,hii dawa kwa mujibu wa maelezo ya dakitari ni jamii moja na hio hapo juu safi cream ila imenipa unafuu ila hio safi cream.imeshindwa !!!...,lakini changamoto yake ni kwamba nikiacha kupaka tu,ugojwa wa ngozi unarudi vile vile tena kwa kasi,nmelazimika kuandika.uzi huu nione kama.naweza.pata njia.mbadala maana nawasiwasi nikiendelea na dawa.hizi huko mbeleni naweza kuja pata hata kansa ya ngozi,
Changamoto nyingine nayokutana nayo ni hizi gentriderm ni krimu kama jina lake lilivyo napopaka usoni nakua mweupe,sasa mimi ni.mtoto.wa kiume japokua naumwa ndio lakini naona kama reputation yangu inaharibika,watu wanaponiambia kua siku hizi unakua mweupe!!,najiskia vibaya sana lakini sina jinsi ndo maana.nmeona.nijitokeze hapa mbele yenu wadau kama kuna mtu anaweza nipa ushauri nifanyeje
Jambo lingine ni kuwa mimi siwezi kabisa kula karanga hasa mbichi,na kama nikila nawashwa sana koo,na.kuvimba mwili na kutema.mate yanayovutika kama mlenda
*Lakini kama.karanga zitapikwa nakula vizuri tu bila shida yeyote!! Sasa wataalamu mnisaidie sijui hii ni.aleji gani ?
Kwa wataalamu wajuzi wa afya na tiba naomba mnisaidie mwenzenu