Ultimately kinachouwa huwa sio ukimwi bali magonjwa ya kawaida. Kwa hiyo mtu mwenye AIDS atakufa kwa kisukari, malaria etc kama wanavyokufa watu wasio na AIDS kutokana na magonjwa hayohayo. So kama mtu ameumwa malaria na kwa bahati mbaya ikamwondoa kutangaza HIV status yake ni irrelevant and i also believe its useless!Si vizuri, lakini si vizuri pia kuficha mfano kama ni taarifa
kwenye Media husikii mtu kafa kwa ukimwi utasikia tu
baada ya kuugua muda mrefu, mi naona ukimwi ni
ugonjwa wa kawaida kama kisukari huku ukiwa chini ya
kansa lakini umefanywa uonekane unatisha kuliko hata
hiyo kansa!
Tatizo ni sisi wabongo tunachukulia kama m2 akifa na ukimwi ndo alikuwa malaya hajatulia
kumbe unaweza ukawa umetulia na ukaded nao
tusinyosheane vidole hata kidogo,cz ukienda ambako zinachukuliwa dawa za kurefusha maisha
mwenyewe akili itakukaa sawa na kujifikria je mm nimepona kweli au k2 bado hakijaanza kjitokeza
sababu inatisha jamani.....tena huyo anaetangaza akae kimya HALI NI MBAYA JAMANI.
Anakufa mtu unayemjua tangu akiwa mzima wa afya hadi alipougua na kufariki. Kabla hujajua amekufa kwa maradhi gani, unaanza kupita ukinong'ona kwamba, amekufa kwa Ukimwi.
Inawezekana ni kweli amekufa kwa ukimwi, lakini hata kama ni hivyo, ni lazima upite ukitangaza kila mahali?
Je itakupa ahueni gani?
Lakini, hivi ikitokea na wewe unafiwa, halafu anatokea mtu au watu wanapita wakitangaza kuwa huyo mtu wako amekufa kwa Ukimwi utajisikiaje? Bila shaka utajisikia vibaya, utaumia na kukereka..... Ni ujinga eh! Ndio ni ujinga kwa sababu umesahau kuwa jana na juzi ulitenda hivyo kwa mwingine.......