Kwani ni lazima tupate msaada wa fedha katika budget?

KunjyGroup

JF-Expert Member
Dec 7, 2009
352
26
  1. Naona tuko kama mtoto asiekuwa. Kila siku unamsindikiza shule hadi anamaliza primary, secondary, chuo, anaanza kazi hajajua tu kuvuka bara bara na anakunywa maziwa kwenye feeding bottle. Kwanini wazungu watufadhili? Hadi lini? Kwanini tusijifandhili wenyewe? Si rasirimali tunazo?
  2. 30 to 33% ya budget ya Tanzania inaibiwa na “Wajanja wachae” kama raisi alivyokiri na Mkaguzi wa mahesabu ya serikali nathibithibisha hilo. Hizi ni hela nyingi sana; karibu 4 trillion shillings zinapotea. Wote tunajua hilo. Ni hela za EPA, Deep Green, Meremeta, IPTL, Richmond, Dowans,kwenye bara bara, etc. tukiwa na serikali madhubuti, though nachelea kusema hatuma kwa sasa, hizi hela haziwezi kuziba msaada wa nchi zinazotufadhili?
  3. Tukiwezesha uchumi wetu wa ndani; kufufua viwanda vyetu and we consume products from our own industries hatutoweza? Mfano:
    i. Migodi tuwape wa Tanzania wenzetu mikopo yakuwekeza katika madini
    ii. Tuweke quarters katika imports kama nguo, viberiti, mchele, sukari, cement etc na tufufue viwanda vetu, tuzalishe kwa wingi ili surplus tu export, kweli tutashindwa kufadhili budget yetu wenyewe, kukuza thamnani ya shilling na hatimaye uchumi?
    Naona ni ujinga uliokithiri kukazana kujenga airport Mbeya badala ya kuweka zile hela kwenye kiwanda cha Mbeya textile (next door to the new airport) ili tuajiri watu wengi na tuzalishe nguo zetu wenyewe. “Eti mtauza mauwa nchi za nje” kwani wale watu wambeya wanajua hata kilimo cha mauwa? Watatoa wapi nauli yakupanda ndege waende wakatafute soko uko ulaya kama mahindi yenyewe mnawaliya bei? Umejuaje kama kulimo cha maua kitawezekana Mbeya? Duh!
Mi naona hatuna vingozi wazalendo. Wanachojali wao nimatumbo yao, kutembeza mabakuri kama omba omba na kufisadi mali ya umma pamoja na watoto na washikaji wao.
Zambia naona mabadiliko. Kuna rais mwenye dhamira ya kweli. Ndani ya miaka mi 5, tutahaibika. Watakuwa juu na sisi ktukibaki na sifa zakijinga “Eti raisi wetu alikuwa wa kwanza kuonana na Obama kati ya marais wa Africa…”
 
Back
Top Bottom