Kwani mwenye CCM ni nani??

Kwani mwenye CCM ni nani??

CBNJR

Member
Joined
Aug 11, 2013
Posts
95
Reaction score
22
Msimamo wa chama,Serikali 2, Kura ya Wazi:Haya mambo mawili ndio yananifanya kila siku niwaze, CCM mwenyewe nani?

Je,hakuna wanaCCM wa serikali 3? Je,wale wawili wa bungeni ndo hao tu wanataka kura ya siri? Je,CCM ni Nape,Jk na Kinana?

Je,CCM haiheshimu mawazo ya wale waliokuwa wanaheshimu mawazo yao kwa miaka mingi sasa?

Je,pale mjengoni,CCM ni Wasira,Pinda,Mkuchika na Lukuvi?

Bado nawaza,CCM ni ya nani? Mbona hao wakiongea wengine ni kuunga mkono tu?? Naenda tafuta chakula kwanza then nitarudi kama nikishiba,maana mfukoni hali ni tete!
 
we hujui hiki chama kuwa ni cha masultani? masultani ndo mali yao!
 
CCM ni kundi dogo lenye mamlaka ya kuongoza dola.
Hili ni kundi la watu wachache wanaotumia 75% ya bajeti ya nchi katika kutawala.
CCM ni kundi la watu wachache wanaojiona wao ndio wenye akili na kudharau maoni mpaka ya majaji.
Kwa kifupi CCM imetekwa na kikundi kidogo cha watu ambacho kimekuwa hatari kwa wananchi wengi kuliko hata kikundi cha Freemason.
CCM inamilikiwa na watu wachache wenye kutumia ushawishi wa fedha na madaraka kutimiza malengo yake.
 
Kama juzi Rais Zuma aliitwa kuhojiwa kuhusu gharama za kukarabati nyumba yake,sidhani kama hapa kuna mwenye ubavu wa kumuita Kikwete na kumuhoji kuhusu matumizi yake.. Basi tuamue tu,nchi iwe ya kisultan au kidikteta
 
Ni ya familia za Karume Mwinyi Nyerere Kawawa Makamba Kikwete Nnauye wengine wachumia tumbo
 
chama cha jamaa mmoja anaitwa patel. yaani huyo anaweza kugawia wajumbe wote wa katiba brifkes full dollar kila mmoja ukapata katiba ya Kihindi
 
Kabla ujaiuliza hayo jiulize CHADEMA NI YA NAN? JIBU RAHISI MTEI,MBOWE,SLAA NA WACHAGA WOTE NA MAPADRI/WAKRISTO........

CCM YA WANANCHI
 
Wenye CCM ni wale wanaofaidi Fedha za Ruzuku wa wabunge wa Zanzibar na Tanganyika na pesa za misaada toka Kwa wafadhili Pia zile za kumbembeleza' muungano hao ndio CCM Kama ulikuwa haujui .
 
Wenye CCM tupo;
..............
tuachieni chama chetu.
 
Last edited by a moderator:
Msimamo wa chama,Serikali 2, Kura ya Wazi:Haya mambo mawili ndio yananifanya kila siku niwaze, CCM mwenyewe nani?

Je,hakuna wanaCCM wa serikali 3? Je,wale wawili wa bungeni ndo hao tu wanataka kura ya siri? Je,CCM ni Nape,Jk na Kinana?

Je,CCM haiheshimu mawazo ya wale waliokuwa wanaheshimu mawazo yao kwa miaka mingi sasa?

Je,pale mjengoni,CCM ni Wasira,Pinda,Mkuchika na Lukuvi?

Bado nawaza,CCM ni ya nani? Mbona hao wakiongea wengine ni kuunga mkono tu?? Naenda tafuta chakula kwanza then nitarudi kama nikishiba,maana mfukoni hali ni tete!
ccm wapo wengi wanaotaka Serikali 3, lakini hawana uwezo kwani wale wanaofaidi pesa za ccm wamewafunika wenye ccm ni wale wanaofaidi matunda ya ccm kwa namna yeyote ile.
 
Tanzama alisimia ya wabunge, vitogoji ilivyokamata na Halmashauri inazoongoza ndiyo utajua CCM ni nani.
 
Tanzama alisimia ya wabunge, vitogoji ilivyokamata na Halmashauri inazoongoza ndiyo utajua CCM ni nani.

Mkuu,ina maana hao wabunge wote,viongozi wa halmashauri,wenyeviti wa vijiji,na vitongoji,wote wanataka serikali 2 na kura ya wazi?
 
CCM ilikuwa ya wana TANU na ASP ambao kama hawajaitwa na Mungu basi ni vikongwe sana, CCM ya sasa ni ya wajukuu wa Waasisi wa iliyokuwa CCM O.G!
 
Nawashanga sana walala hoi wanajinasibisha na sisiemu.Shame on you!
 
Back
Top Bottom