kwani mi nafanana na fundi

kwani mi nafanana na fundi

oduko

Senior Member
Joined
Dec 16, 2012
Posts
169
Reaction score
56
Jamaa yuko home kwake
anaangalia mpira, mke wake
akamfuata sebuleni: Mume wangu
hiyo taa hapo mlangoni haiwaki
vizuri, itengeneze basi. Jamaa
akajibu: Nitengeneza taa wakati
naangalia mpira? Hivi unaniona
nafanana na mafundi umeme? Mke
akanyamaza. Baada ya dakika
chache akamfuata tena: Mume
wangu hivi umeona meza
imevunjika mguu mmoja kule
jikoni? Jaribu basi kuitengeneza.
Jamaa akamcheki halafu akajibu:
Hivi we mwanamke una nini?
Ukiniangalia nafanana na mafundi
seremala? Mke akaguna halafu
akaondoka. Baada ya muda akarudi
tena: Baba watoto, hapo kwenye
ngazi mlangoni umeona tofali moja
limetoka? Jaribu basi kulirudishia.
Jamaa kwa hasira akajibu: Hivi
hupendi kuona mtu amekaa kwa
starehe? Mimi nafanana na
mafundi ujenzi?
Baada ya kuona anasumbuliwa
jamaa akaamua aende zake
kuangalia mpira baa. Akiwa
anacheki mpira nafsi ikamsuta
kwamba alichomfanyia mkewe si
kizuri akaamua kurudi home
kumuomba msamaha. Alipofika
akukuta tofali mlangoni
limetengenezwa, meza jikoni nayo
imetengenezwa na hata taa
mlangoni nayo imeshatengenezwa,
akashangaa akamuuliza mkewe
vipi? Mkewe akajibu: Alikuja
Kiwango Dungadunga yule kaka wa
nyumba ya jirani akanisaidia ila
kwa masharti kwamba,
nimtengenezee ice cream au
nikalale kwake lisaa limoja. Jamaa
akajibu: Dungadunga mjinga kweli,
kwa hiyo ukamtengenezea hiyo ice
cream. Mke ajibu: Kwani mimi
nafanana na kiwanda cha bakhresa?
 
Kama hafanani na kiwanda cha bakhresa means,,,,, b'dada alitimiza lile shart lingine...
Jamaa lazma akasomee ufund....
 
kumbe jamaa anakaa na malaya:smile-big:
Nalog off
 
Toba weeeeeeee presha juuuuuuuu

Sent from my BlackBerry 9900 using JamiiForums
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom