Kwani kuolewa ni jambo kubwa sana?

MWANAMKE YEYOTE AKITAKA AOLEWE MAPEMA KABLA HATA YA 30 AGE ANATAKIWA AFANYE VITU VIFUATAVYO;
1. Awe anajistiri
2.Awe anajishughulisha na biashara maana wadada wengi hupenda hela ambazo si za jasho Lao hivyo wengi huishia kulambwa tu. Kwa hiyo kupitia pesa ataweza jikimu Mwenyewe bila ya kutegemea mwanaume.
3. Awe mchamungu na awe anamuomba muumba wake ampatie mume aliebora.
4.Awe mpole, mkarimu na Mwenye haya sio kila kukicha na kigulu na njia kujipitisha kwa wanaume ili uolewe.
5. Asijirahisishe na ngono.
6.wala asipende asiekua wa level yake au mfanano wake.


NB: Natumaini nimeeleweka ahsanteni niwatakie weekend njema.
 

hahahaaaaaaaaaaaaaaa kama nakuona ulivyo boreka ulivyoenda kwenye hio seminar... 😁 😁 😁 😁 😁 😁
 

tumekuelewa ndugu mjumbe, hivi kinyume cha mabaharia ni nini?LOL
 

Siongezi neno,wakati ukiendelea kujifariji soma na hapa but ninachoamini mimi 99.01% ya wanawake wanaojitambua sawasawa vichwani mwao wanatamani na wanaamini kuwa na familia stable,ile mtoto anaamka asubuhi anamwamkia baba na mama,akiaga kwenda shule anawaaga baba na mama usiku akienda kulala anawaaga tena baba na mama siyo mtoto aamke asubuhi mama alirudi usiku kutoka alikotoka macho yamemjaa usingizi na pombe haelewi hata aliyesimama mbele yake ni mwanae au siku akiulizwa mama baba yuko wapi amdanganye alikufa kumbe yupo hai.

Upo wakati utafika na kama utakuwa bado hai lazima utafika hapo ndipo utakapoelewa kwanini huyo rafiki yako anaweweseka.
 
You have said it all. Mtu analala hovyo na wanaume,analala mpaka na mabosi wake ,na watu ofisini na mtaani wanajua halafu eti anasubiri kuolewa. Wakishalala na wewe, men talk,waoaji wanaogopa!
 
Ukiwa una mtu unafanyanae sex, hakuna haja yakusema hujaolewa,,
Within 3months tu serikali inahesabu tayari hiyo ni ndoa.
Mkuu acha kumlisha matango pori mwenzio
Kasome vema sheria ya ndoa ya mwaka 1971
 
ati kuolewa ni jambo la kawaida hahahahahah wewe itakuwa ule upepo wa kisuli suli ulikupita kwa juu.mtoa mada anataka kuolewa ila kaja na gia nyingine
 
Usipoolewa Maana Yake Hutazaa ?

Ukizaa Maana Yake Utazaa Shaghalabagala Mpaka Na Waume Za Watu Au Vibaka Tu.

Hakuna Mtu Asiyependa Kuwa Na Familia Bora, Yenye Nguvu Na Heshima. Zingine Mbwembwe Tu.

Maisha Bila Familia Ni Ya Upweke Sana And So Boring Na Kila Utakachokipigania, Hutakiona Kama Kina Thamani Yoyote
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…