Kwani kodi zimebadilishwa?

fakeusername

Member
Jan 12, 2016
7
13
Habari wadau?

Mie ni kijana nnaeanza ujasiliamali na nna fremu ya duka dogo sana ( kigoli) maeneo ya kkoo.
Sasa nimenda kufuatilia tin pale Lumumba leo na kabla ya makadirio naambiwa kodi mil 2 nauliza mbona kwa kuanzia ulikua ni laki 8, nikaulizwa uliambiwa na nani? Nikajibu niliuliza papa hapa tra. Hapo ni mbali na kodi ya pango ile asilimia 10 na ile asilimia 1 sijuhi ya nini kwa mkataba wa pango.

Wadau hii ni sahihi na kama sio sahihi nifanye kipi maana nimeambiwa nilipe hiyo laki 5 kwa miezi mi3 ya kwanza ili nipate tin ambayo inabadilishwa kutoka tin ya leseni kwenda kwenye tin ya biashara na tax clearance ndio niende nikachukue leseni manispaa ya ilala pale mnazi mmoja.

Naombeni msaada wa maelezo kama hizo kodi zimepanda kwa maeneo ya kariakoo kwa maduka madogo mfano wa vigoli
 
Badilisha tin yako iende mkoani then lipia kodi mkoani ! Wakikagua kwenye system yako watakuta umeshalipa tayari ! Kumbuka kuandika kuwa una branch dar then mkoa ambapo lipo file lako ndio watakukadiria kodi ya kishkaji kuwa mjanja mjasiriamali
 
Back
Top Bottom