Kwani Kikwete ana tatizo gani? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwani Kikwete ana tatizo gani?

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by payuka, Sep 6, 2010.

 1. payuka

  payuka JF-Expert Member

  #1
  Sep 6, 2010
  Joined: Jun 17, 2010
  Messages: 832
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Kwani Kikwete ana tatizo gani?

  clip_image001.jpg

  Hiyo dummy cheki imeandikwa dola laki mbili kwa maneno na dola 300,000 kwa namba. Je hapa Kikwete alipewa cheki ya dola ngapi? Mbili au tatu? God know how bogus this guy is.
  Kwa wanaofuatilia utendaji mbovu wa rais Jakaya Kikwete, watakubaliana nami kuwa si mtu makini wala hajifunzi. Kama anajifunza basi ni mzito na mgumu wa kufanya hivyo na saa nyingine anajifunza kutojifunza kabisa. Hebu angalia hiyo picha hapo juu. Je unajifunza nini toka kwa rais wako anayemaliza muda wake akiwa amezungukwa na kila aina ya tuhuma kuanzia ufisadi hadi kutokuwa muaminifu katika ndoa?

  Arusha alifungua hoteli iliyokuwa imevunja sheria. Mbeya amepewa kadi feki za CHADEMA. Hapa bado hatujagusia mama wa kashfa-kusaini mswaada uliokuwa doctored. Bado hatujagusia uchakachuaji wa mafuta na uraia wa Hussein Bashe ambao inasemekana Kikwete katumiwa na mwanae kumkomoa adui yake. Hapa bado hatujagusia suala la umri wa aliyekuwa mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM, Hamad Yusuf Masauni aliyepitishwa na Kikwete kwa kuingilia uchaguzi wa jumuia hiyo.

  Hapa bado hatujagusia uteuzi wa mkuu wa wilaya mkoani Shinyanga na kumbatilisha siku iliyofuata. Hapa ikumbukwe. Bado hatujagusia upayukaji wake aliposema hivi karibuni kuwa ukiona misongamano ya magari barabarani ujue ni dalili za maisha bora.
  Huyu ndiye Kikwete anayetaka kuwaingia watanzania mkenge kwa mara nyingine tena bila aibu.

  Angalia mafisadi wakubwa ambao ni marafiki na washirika zake kama Rostam Azim, Edward Lowassa, Andrew Chenge, Jaffer Sabodo, Andy Chande, Benjamin Mkapa na wengine wanavyozidi kutesa huku umma ukiteseka. Angalia mwanae na mkewe wanavyomtumia kuichafua ikulu kwa kuifanya nyumba ya biashara tena ya aibu. Angalia uteuzi wake wenye utata wa kujaza nafasi mbali mbali.
  Uliyachunguza na kuyajua yote ya Kikwete unapata kinyaa. Hakika Kikwete si kingine unachoweza kuelezea bali ajali ya kisiasa. Hivi unategemea mtu anayeshauriwa na mkewe, mwanae, waramba viatu kama Salva Rweyemamu, Yusuf Makamba na makapi kama Tamwe Hiza kweli awe na bao?
  Hatumchulii. Yatafichuka mengi hasa pale watanzania watakapofanya kosa wakaridhia arejee madarakani iwe kwa kumchagua au kukubali kuibiwa kura.

  Chanzo: Freethinking Unabii.

   
 2. Kiranja Mkuu

  Kiranja Mkuu JF-Expert Member

  #2
  Sep 6, 2010
  Joined: Feb 18, 2010
  Messages: 2,100
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  [​IMG] Kwani Kikwete ana tatizo gani?
  ana matatizo ya kifafa na ufinyu wa fikra.
  Nlicheka sana siku alipohojiwa na wale waandishi wa Kifaransa, akaulizwa kwa nini nchi yako ni masikini sana licha ya kuwa ina rasilimali nyingi?
  Akajibu "Sijui"
  Kweli huyu mtu hawezi kutukomboa kwenye ufukara tulionao, kwa kuwa macho yake yote yako kwenye kuwalinda mafisadi.
   
 3. Lukolo

  Lukolo JF-Expert Member

  #3
  Sep 6, 2010
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 5,137
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Hapa umejibu nini kulingana na post iliyopo hapo juu? Kweli wewe ni kama makamba tu, uwezo wa viongozi na mashabiki wa CCM ndiyo unaishia hapa. Umewekewa evidence kibao hapo juu, zinazoonyesha kwamba Kikwete hana umakini katika utendaji wake, badala ya kujibu hizo unaanza kufanya ulinganisho ambao haupo kabisa kwenye hiyo post. Si ujibu kama hayo yaliyosemwa hapo kwenye hiyo post yalitokea kwa Kikwete au hayakutokea? Hapa habari za Slaa zimeingiaje? Mbona usimseme Lipumba, Rugwe au Mtahwa?

  Tunajua hicho chote ni kiwewe cha CCM dhidi ya Slaa, nafikiri amewashika pabaya mwaka huu. Hata mkishituka tu usingizini cha kwanza kutamka ni Slaa, hakuna lingine. Fedha zote mlizowaibia wananchi maskini mwaka huu zitawatokea puani. Slaa anawashitaki nyie wote na ufisadi wenu huo.
   
 4. Raia Mwema

  Raia Mwema JF-Expert Member

  #4
  Sep 6, 2010
  Joined: Jun 30, 2008
  Messages: 535
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  .

  Chadema ikiwakilishwa na Mbowe na Dr Slaa walipokea mchango wa kampeni wa sh. milioni 100 kutoka kwa Sabodo kumbe nao wanakula fedha za mafisadi. Hawa kweli ni wapambanaji wa kweli au kiinimacho tu?
   
 5. Lukolo

  Lukolo JF-Expert Member

  #5
  Sep 6, 2010
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 5,137
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Unajua ninachoshangaa mimi ni kuingia kwa mjadala wa Slaa kwenye post inayouliza kama Kikwete ana matatizo gani? Na katika hiyo post hakuna panapomtaja Slaa, sasa wewe umetoa wapi habari za Slaa kwenye post hii?

  Ndiyo maana nasema CCM hamna jipya zaidi ya siasa zenu za fitina na kuchafuana. Kwani ni nani asiyejua namna ambavyo mgombea wenu alitumia magazeti na vyombo vya habari kuwachafua akina Sumaye, Mwandosya na Salim mwaka 2005? Tumeshamzoe huyo mgombea wenu, anajijua hana uwezo, na anajua kwamba watanzania hawana imani naye tena.

  Ndiyo maana ameyanunua magazeti ili yaandike hizo pumba zake. Huwezi kufikiria ni kwa vipi gazeti la serikali linashindwa kuandika sera za Slaa badala yake linaandika habari za udaku? Sasa magazeti ya Shigongo yataandika nini? Mmepoteza dira ndugu zangu.
   
 6. Sokomoko

  Sokomoko JF-Expert Member

  #6
  Sep 6, 2010
  Joined: Mar 29, 2008
  Messages: 1,918
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Mimi simlaumu mzee kwa hiyo cheki hapo vijana ndio wamemwingiza chaka...
   
 7. Lukolo

  Lukolo JF-Expert Member

  #7
  Sep 6, 2010
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 5,137
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Tupe ushahidi kwamba Sabodo ni fisadi. Najua huna huo ushahidi, wewe kwako kila mwenye hela basi ni fisadi. kwahiyo kama wewe umeweza kujenga nyumba ya kuishi na wengine hawajajenga basi wewe ni fisadi? Kama Sabodo ana fedha ya kuweza kutoa mchango kwa CHADEMA na wewe huna, basi Sabodo ni fisadi?

  Lakini sisi tutakupa ushahidi kwamba Kikwete ni fisadi namba moja nchini. Ndiyo maana kajaze kesi hewa mahakamani kuhusiana na ufisadi. Siku zake zinahesabika tutamlipua mambo yake hadi atakiwe kujiuzulu urais ili akajibu hizo tuhuma alizonazo.
   
 8. JOYCE PAUL

  JOYCE PAUL JF-Expert Member

  #8
  Sep 6, 2010
  Joined: Jan 8, 2010
  Messages: 1,007
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  nimeamini kweli jina analolichagua mtu linaendana na tabia.wewe PAYUKA jina lako kweli ni la mpayukaji,kwani mtu anayepayuka always anaongea vitu bila kuchuja wala kufikiri.ama kweli nyani haoni kundule.hata kama ndio mzalendo na nchi ya tanzania kweli sio jambo la busara kutoa lugha chafu kumdharau KIONGOZI WA NCHI YAKO LOH,ebu jaribu kujirekebisha ikiwezekana uombe RADHI kwa wanajamii forum KWA KUMNENEA KIONGOZI WAKO WA NCHII maneno yasiyo na heshima.pili huyu ni kama baba yako huwezi kumpayukia tu kama jina lako linavyoonyesha kuwa ni mpayukaji.ubarikiwe katika kipindi hiki cha ramadan tena ongea maneno mazuri yenye kutoa ujumbe mkali wa kuinyooshaa serikali yetu iliyoonyesha kulega lega kwa kutumia lugha nzuri.
   
 9. Mr. Zero

  Mr. Zero JF-Expert Member

  #9
  Sep 6, 2010
  Joined: Jun 5, 2007
  Messages: 9,503
  Likes Received: 2,744
  Trophy Points: 280
  Lazima wewe ni mtoto wa kigogo!! Otherwise, akili yako haina ak....!!!!! Propaganda zisha kupumbaza......!!!
   
 10. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #10
  Sep 6, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  kikwete hana tatizo

  tatizo ni sisi
   
 11. Sokomoko

  Sokomoko JF-Expert Member

  #11
  Sep 6, 2010
  Joined: Mar 29, 2008
  Messages: 1,918
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Mkuu hujaweka wazi tatizo sisi tunavyofikiria ama? mie sioni ubaya wowote hapo labda yeye ndio awe ameliandika otherwise wakulaumiwa waandaaji wa hiyo shughuli na kikubwa watu wa usalama wawe wanakagua hivi vitu maana ni kweli sisi tuna matatizo tutaanza ohh huyu vp karogwa kumbe masikini baba wa watu amewaamini watu na wao hawakutimiza wajibu wao.
   
 12. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #12
  Sep 6, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  tatizo sisi...sisi wote hatuko makini na yeye ni kioo cha jamii na jamiii ni sisi

  tunaishi hivyo wote, hatuko makini, nk.

  Unachokiona kwenye hiyo picha ndiyo reflection ya jamii ya watanzania, umakini mdogo na rabsha nyingi
   
 13. m

  mwita ke mwita JF-Expert Member

  #13
  Sep 6, 2010
  Joined: Aug 13, 2010
  Messages: 5,491
  Likes Received: 1,220
  Trophy Points: 280
  kijana zungumzia mendeleo ya watu sio vitu we hujui wananchi wanatozwa kodi ulitaka kodi hizo zinuue ndege ya raisi au kuwapa vimada
   
 14. payuka

  payuka JF-Expert Member

  #14
  Sep 6, 2010
  Joined: Jun 17, 2010
  Messages: 832
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Tumeshazizoea lugha zenu mafisadi....Mkishikwa pabaya mnadai mmetukanwa! ni kipi kisicho na ukweli katika hiyo msg???

  Afu una uhakika gani huyo unayemsema wewe sio mjukuu wangu??? jiangalieni sana ninyi manao dandia magari mbele!!!! mi si sawa na MFUKUNYUZI ulie-mwaribia thread yake!!! alivopost madhara ya dawa ya kichina!!! inavoelekea wewe ni muhanga wa dawa za kichina ...na zimeshakuchanganya kiasi kwamba unashindwa kupambanua mambo pamoja na kujenga hoja za msingi kulingana na wakati halisi!!!!

  Mmegusa pabaya safari hii .....kwani hata mtanzania asiekwenda shule ameanza kujua janja yenu ya KUIMALIZA nchi!!!!
   
 15. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #15
  Sep 6, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,765
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  Nawasiwasi na uwezo wako wakufikili hapa Slaa ametoka wapi ongea kuhusu ya kikwete!!
   
 16. jaxonwaziri

  jaxonwaziri JF-Expert Member

  #16
  Sep 6, 2010
  Joined: Feb 17, 2010
  Messages: 378
  Likes Received: 54
  Trophy Points: 45
  Kitu kimoja ni dhahiri: Pamoja na yooooote yaliyokwisha semwa, kama kuna kosa ambalo nchi hii italijutia mpaka milele ni kumchagua kikwete awe rais wa kwa mara ya pili. Litakuwa ni kosa litakalo igharimu nchi kwa karne nzima! Sisemi kuwa CCM hakuna watu wazuri na viongozi waadilifu, wapo wachache ambao ni waadilifu na wachapa kazi wazuri sana, lakini KIkwete....? Aaaaaah...jamani Kikwete......? Lets be serious!
  Labda mwingine but this guy seems so soft on issues and this time arround this country needs somebody who is stern, has guts to face the issues!
  And if I look arround, sioni mwingine zaidi ya Dk Slaa. Watu wanamsema sana kuhusu mambo yake binafsi, but tujiulize kuna viongozi wangapi duniani hawakuwa wasafi katika maisha yao binafsi na waliongoza nchi zao vizuri? Tizama Ufaransa, Italia, South Africa etc. Kwanini tunazungumzia masuala ya ndoa hapa, kwanini tusizungumzie Ufisadi, mfumuko wa bei, kukosa umakini katika maamuzi mazito ya mustakabali wa taifa, kuimarisha uwajibikaji katika sekta za umma, etc?
  Kunanini baadhi ya wanachama wa CCM hawataki hayo yazungumzwe? Wanataka kuficha nini? Kwanini hawataki Kikwete, Slaa, Lipumba wajitokeze kwenye mjadala wa wazi kuhusu maslahi na mustakabali wa taifa bali wana-mtetea kila siku kuwa eti hawezi kukaa sehemu moja na slaa ili kuzungumzia masuala hayo...! What a shame...! Mbona viongozi wa nchi zinazoongoza dunia hii huwa hawaogopi mijadala, mbona huwa hawatumi makatibu wa chama kuwajibia? Tuamke jamani, hatutaki kubebana kwa namna hii....! kama wapo watu wanaodai kuwa kikwete kuna alichofanya cha manufaa, kwanini wasimruhusu aje kwenye mjadala aseme? Maraisi wenye akili timamu huhitaji sana mijadala wala hawaikimbii....! Ndo maana ninyi CCM mnatulazimisha kufikiri kuwa inawezekana mnafaidika na madudu yanayoendelea katika nchi hii pamoja na uoza wooooote uliopo katika sekta ya umma, mashirika yake na serikali kwa ujumla!
   
 17. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #17
  Sep 6, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,765
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  Nikweli hana tatizo nchi ndo inamatatizo ambayo raisi hayamuhusu
  - Maradhi
  -ujinga
  -Ufisadi
  -n.k
  kama haoni matatizo ya hii nchi atoke!!
   
 18. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #18
  Sep 6, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,765
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  Ni kweli kama yeye uwezo wake ni mkubwa akajibu maswali mdahalo ni muhimu but bcs uwezo wake ni mdogo thus why anaogopa!
   
 19. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #19
  Sep 6, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,765
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  Kwani yeye nani asisemwe kama anakosea!?? unajua kama anaharibu ajirekebishe bila kujali yeye ni nani kwako Bibie!!
   
 20. N-handsome

  N-handsome JF-Expert Member

  #20
  Sep 6, 2010
  Joined: Jan 23, 2008
  Messages: 2,317
  Likes Received: 128
  Trophy Points: 160
  People lets Stop this Kikwete and Slaa personal issues
   
Loading...