Kwani Anne Makinda asikae karibu na waliomchagua huko Iringa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwani Anne Makinda asikae karibu na waliomchagua huko Iringa?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mzalendo80, May 18, 2011.

 1. Mzalendo80

  Mzalendo80 JF-Expert Member

  #1
  May 18, 2011
  Joined: Oct 30, 2010
  Messages: 2,385
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 160
  Watanzania nashindwa kufahamu kwanini wabunge wengi hasa wa Magamba wanapenda sana kuishi Dar na kuwakimbia wananchi wao waliowachagua.

  Hivi kuna haja gani ya kumchagua Mbunge ambaye hakai kwenye Jimbo?
  Mfano Spika Anna Makinda anajenga Dar na waliomchagua wapo Iringa kweli inaingia akilini, kuwakilishwa na Anna yuko takribani ya umbali 500 Mile? Tena anajenga na kuziba barabara wananchi wa Dar wasumbuke kwa ajili ya ujinga wa mtu mmoja tena sio Mbunge wao, Anna Makinda amewakimbia wapiga kura wako na kuja kukaa karibu na waliomuingiza kwenye mtandao wa Kifisadi (Ujambazi wa kuliibia Taifa na watanzania)

  Anna Makinda yupo zaidi kwenye maslai ya Kwake na mafisadi waliomuweka kuliangamiza Taifa letu.

  Hizi Tabia mbovu zinazofanywa na wanasiasa ucharwa kama hawa wa magamba tuzikataeeni Watanzania na kuwaepuka wanasiasa hawa kama Anne Makinda, Lowassa, chenge Mkono, Kikwete, Rostam na Mafisadi wengine ambazo wanapanga kuliangamiza hili taifa tuwaangamizeni kabla ya Taifa letu kuangamizwa na Mafisadi.

  Tunajuwa kuwa kila mtanzania anahaki ya kuishi kokote lakini hizi tabia chafu zinazofabywa na hawa majambazi wa kisiasa kwa maufaa yao sio sahihi, akakae hukuhuko alipochagualiwa ili awekaribu na wananchi waliochamgua sio kuwakimbia na kuwakumbuka kila uchaguzi unapokuja.

  Waliompigia Kura huyu mama poleni huko Iringa kama angekuwa ni mbunge wangu ningehakikisha harusdi tena Iringa kugombea Umbunge tabia Mbovu acheni nyie wabunge Uchwara na waroho wa Madaraka.

  Nenda kakae jimboni kwako wewe Mbunge uwe wa Magamba au Upinzani saidia wananchi wako
   
 2. Ndumbayeye

  Ndumbayeye JF-Expert Member

  #2
  May 18, 2011
  Joined: Jan 31, 2009
  Messages: 4,806
  Likes Received: 1,053
  Trophy Points: 280
  mkuu mbona unamuonea mama wa watu, kwani kuna sheria inayokataza kujenga nje ya jimbo lako!
   
 3. tanga kwetu

  tanga kwetu JF-Expert Member

  #3
  May 18, 2011
  Joined: May 12, 2010
  Messages: 2,165
  Likes Received: 1,124
  Trophy Points: 280
  Zitto ameshawaambia LIVE juzi wapiga kura wake tena jimboni mwake Makinda.
   
 4. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #4
  May 18, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,435
  Likes Received: 19,784
  Trophy Points: 280
  hii ni sera ya ccm kubanana hapa hapa
   
 5. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #5
  May 18, 2011
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Nafikiri hii ni changamoto kwa Watanzania kuliweka wazi ndani ya katiba suala la makazi ya viongozi.

  Na Serikali lazima ijenge makazi ya kudumu kwa viongozi wake wakuu pindi wanapochaguliwa.
   
 6. Mzalendo80

  Mzalendo80 JF-Expert Member

  #6
  May 18, 2011
  Joined: Oct 30, 2010
  Messages: 2,385
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 160
  Mkuu simuandami huyu Mama ila ameniboa sana kufunga mtaa kwa mahitaji yake hawa Magamba wanafikiri hii nchi ni ya kwao wao peke yao. Kuna haja gani ya Kufunga Mtaa kwa ajili ya Ujenzi wa kibanda chake? Je na mimi nikiwa na jenga pia ninaweza kufunga mtaa kwa ajili ya Usalama wangu?

  Kwanini asigombee ubunge Kawe au Ilala kama anataka kukaa Dar?
  Huyu Mama anataka kukaa Dar kwa sababu ya Kupiga madili ya Mikataba feki anataka awe karibu na Mogogoni ili naye afaidi matunda ya Magogoni kabla nchi hawachukuwa wenyewe walalahoi.

  Ila kila kitu kina mwisho wake na mwisho wao hawa Mafisadi ni JELA , siku tutakapo chukuwa nchi Mafisadi wote ni kufunga
   
 7. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #7
  May 18, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  According to Anna Makinda Mwaka 2010 ulikuwa wa mwisho kugombea Ubunge huko Iringa...

  Anategemea CCM itashinda atakuwa Spika bila ya kuwa na Jimbo kama Marehemu Cheif Adam Sapi Mkwawa...
   
Loading...