Kwangu, huyu ndiye spiderman mkali

Kwangu, huyu ndiye spiderman mkali

Chilojnr

JF-Expert Member
Joined
Jul 5, 2012
Posts
308
Reaction score
1,354
Nimekaa nikisubiri trela la pili la Spiderman: No Way Home kuletwa kwa Youtube leo hii. Wakati huohuo nikawa najiuliza kwa sababu gani watu wanasumbua sana vichwa vyao kujua ni Spiderman gani mkali zaidi ya wenzake. Namshukuru sana Mungu nimefanikiwa kuwaona wote hao, tena siku ambazo muvi zao zikiwa zimezinduliwa kwa siku ya kwanza kwenye majumba ya sinema. Nadhani kwenye hili na mimi nitachangia ninachokijua.

Tobey Maguire: Siku zote mtu wa kwanza hupata umaarufu na kuonekana kuwa bora sana, ni kwa sababu tu yeye ndiye alikuwa wa kwanza kuonekana kideoni akiwa na character hiyo hapo.

Ni sawa na leo hii ukiuliza James Bond gani mkali, mimi nitasema Craig Daniel ni hatari sana huku akifuatiwa na Pierce Brosnan lakini duniani wanasema James Bond bora kutokea ni Sean Connery, ni kwa sababu tu ndiye alikuwa mtu wa kwanza kuigiza huo uhusika.

Tobey ni mzuri sana, ila hakuwa amechangamka kama inavyotakiwa, na hata script zake zilikuwa ni serious sana kuliko za wengine waliofuatia.

Huyu jamaa, Spiderman wake alikuwa fasta sana kuliko wengine, alikuwa akisense sana hatari kuliko hata hao wengine.

Muvi yake ya kwanza, niliona ikiwa kali sana, ni mtu ambaye unajua kabisa anataka kufika mbali zaidi, kwenye muvi yake ya pili pia alikuwa makini mno ila ile ya tatu, ilionyesha kabisa Tobey amechoka na alihitaji replacement.

Kwenye muvi, hakuna kitu kinachochosha kama kuigiza character moja kwa muda mrefu. Tobey alionekana kuchoka sana, na pia umri wake haukumruhusu kuendelea kuwa Spiderman.

Unajua wanachokifanya Marvel, Spiderman imechukuliwa ni character ya watoto, hivyo anayetakiwa kuigiza, inampasa kuwa na umri chini ya miaka 30 ama 25. Hivyo wakaamua kumtoa na kumleta Andrew.

Andrew Garfield: Kwangu naweza kusema huyu ndiye Spiderman ninayevutiwa naye zaidi. Kwanza amechangamka sana, nadhani kilichomfanya kupendeza zaidi kwangu ni kwa sababu alianza kuaminika kwenye muvi nyingi za nyuma yake.

Jamaa aliipata ile character akiwa na jina kubwa, hivyo aliweza kuisimamia vilivyo, ila aliangushwa na script tu, hazikuwa zile zenye ubora mkubwa, na zilikuwa na mapungufu kadhaa.

Ukiangalia action zake za kwenye Amazing Spiderman, utakubaliana na hili ninalosema, na alikuwa na comedy fulani hivi tofauti na Tobey.

Huyu mwamba aliigiza mbili tu, Amazing Spiderman na Amazing Spiderman 2, wakaachana naye kwa sababu ya umri na ndipo alipochukuliwa Tom Holland.

Tom Holland: Niseme tu kwamba huyu dogo ndiye atakuja kuwa Spiderman maarufu kuliko wote waliowahi ama watakaowahi kuigiza character hiyo.

Dogo ana mvuto mbele ya kamera, na kwa kipindi hiki, huyu ndiye muigizaji ninayevutiwa naye kuangalia muvi zake, na niseme tu naisubiri kwa hamu Uncharted ya mwaka kesho nione makamuzi yake.

Dogo alipata mashavu kadhaa kabla ya kuwa Spiderman ila baada ya kupata shavu hilo, amekuwa akipata mashavu kila kukicha. Hili liweke akilini, kuna siku utakubaliana nami...

Huyu dogo atakuwa maarufu zaidi ya Spiderman yeyote. Huyu dogo atakuja kuwa muigizaji anayelipwa pesa nyingi kuliko wote. Na huyu dogo kuna mwaka atakuja kuwa James Bond huko mbeleni kwa kuwa sifa moja kubwa ya kuwa Muingereza anayo.

Tom amepata nguvu sana ya kuwa Spiderman kwenye muvi kwa kuwa alibebwa sana, hakuwa amejibeba yeye mwenyewe, na Marvel walifanya hivi kwa kuwa baada ya kuondoka kwa Tobey na kuja Andrew, character ikaanza kupoteza nguvu, hivyo walichokifanya majamaa ni kuiboost hiyo character kwa kumuingiza kwenye kundi la Avengers.

Lengo kubwa ili utakapokuwa unampenda Ironman, Captain American wengineo na kuangalia muvi zake, humo umkute dogo.

Character hiyo ilipata nguvu, watu wakaanza kutamani kuona muvi yake akiwa peke yake, hapo ndipo wakaachia Spiderman: Homecoming, bila kufanya boosting ndani ya Avengers: Civil War, hii character ilikuwa inakwenda kupotea kwa kuwa ilianza kuyumba.

Holland amefanikiwa sana. Amevunja rekodi ya trela lake kuangaliwa mara nyingi Youtube kuliko trela lolote lile tangu kuumbwa kwa dunia hii, aliivunja rekodi ya Avenger Endgame ambayo iliweka rekodi ya kuangaliwa mara milioni 24 ndani ya saa 24 tu.

Na kwa jinsi Marvel wanavyoleta ujanja ujanja wa kupiga pesa, tetesi zimeanza kuenea kwamba hii Spiderma mpya itakayotoka mwezi ujao itakuwa na Spiderman wote, yaani Tobey, Andrew na Tom.

Hii imeongeza msisimko mkubwa wa watu kutaka kuitazama muvi hiyo kwa hamu kubwa. Sijajua kama kwenye trela la leo wataonekana wote ama mpaka trela la tatu mwezi ujao. Ila nahisi itakwenda kufanya vizuri sana sokoni.

Kwa tetesi ambazo nimezinyaka ni kwamba Tom Holland hii inaweza kuwa muvi yake ya mwisho kuigiza kama Spiderman, Marvel wameanza kufanya mchakato wa kumtafuta mtu mwingine ambaye atakuwa na umri mdogo, ningependa tu character hiyo apewe mdogo wake, Harry Holland kwani naye naona anakuja vizuri kwenye muvi.

Kwa kuwa Marvel wanaijua biashara kama Wachaga, usishangae kuona Spiderman anayefuata kuwa mtu mweusi. Manake washafanyahivyo kwenye Animation, bado kwenye muvi halisi.

IMG-20211116-WA0002.jpg

Tobey Maguire atabaki kuwa Spiderman bora kuliko wote daima kwa upande wangu maana yeye ndio kanikuza enzi hizo za spiderman.. mpaka tunapanda juu tunaruka tunakosekana kidogo kuumia ni yeye ndio aliyejaaa memories na nostalgia...nenda east, west atabaki kuwa Maguire ndio Spiderman kama ulivyosema so hell yeah.

Kuhusu Andrew Gafield yeye sio Spiderman bora kabisa kwa mtu yeyote anaemfaham character Spiderman vizuri hatokubaliana na wewe kabisaa..bora ungesema Tom Holland, hapo umekosea sana maana Andrew ni mtu fulani yuko cool hivi Confident character.. ambavyo ni opposite kabisa na personality ya spidey as nerdy teenager

Tom walipatia sana maana kajamaa kana vipaji vingi besides acting anaweza vitu vingine kama dancing, acrobats n.k, kuhusu Avengers kumboost spiderman hapana maana Spiderman kwa Marvel ndio Character ambae alikuwa Stand-alone na ana mashabiki wengi sana, walikuwa wanashindwa kumleta kwenye Avengers sababu hakuwa wakwao alikuwa wa Sony enzi hizo
 
Tom hiyo uncharted kwakua game lake nimelicheza sana nasubil nilione hilo movie lake
 
Back
Top Bottom