Kwamba raia ni kigeugeu?

Sijali

JF-Expert Member
Sep 30, 2010
2,586
1,678
Kwamba raia ni kigeugeu, na kwamba pamoja na udidimiaji wa wazi wa haki za binadamu katika awamu hii, isipokuwa ikiwa Rais ataleta maendeleo makubwa katika kipindi chake, watu watasahau maovu yote na kumsifu hata pengine kum miss ajapo mwengine 'mpole'?

Na si kweli kuwa kutokana na kufahamu hivi, ndipo watawala hufanya maovu yeyote kwa hoja ya kuwapatia Maisha bora raia?

Hebu niambie, baada ya miaka mitano Stigglers Gorge ikawa imekwisha, reli ya umeme hadi Kigoma imekwisha, Pato la Serikali likafikia dola bilioni 100 kutoka 60 hivi sasa, na pato la mtu likafikia dola 2000 kutoka 1100 sasa je kuna atakayekumbuka uchaguzi haukuwa huru au Tundu Lissu alipigwa risasi, na Lema ilibidi akimbie nchi?

Nani anayekumbuka hivi sasa kuwa ili kufika ilipofikia China hivi sasa, takriban binadamu milioni 300 walikufa kwa njaa na mateso mengine wakati wa Cultural Revolution?

Na hata siye wenyewe Tanzania, nani anayekumbuka excess za Ujamaa kiasi watu waliliwa na Wanyama pori na njaa kubwa iliyosababisha foleni ndefu za chakula? Tumeyasahau hayo ingawaje hata hatukufanyiwa kama ambayo yanaweza kufanyika chini ya uongozi huu?

Ama kweli raia kigeugeu!
 
Hata siku moja mbuzi na mziki hawana ukaribu.

Ni either umeamua kupoteza muda na gitaa lako,au unalipwa kwa kazi hiyo ya kumpigia mbuzi.

Afrika ni nchi masikini, duni. Tunatakiwa kuondoa hali hiyo kwanza ndipo tuje kwenye mambo mengine kama, uhuru na nk.
 
I
Ili iweje,au sijakusoma.
Huko tunakoelekea unakosema kuna maendekeo makubwa ( kama tutafika ) tayari Ethiopia wako huko.

Wana Ethiopia Airlines, SGR ya kisasa na Bwawabla Umeme ( Na wanajua biashara, wakati sisi ni utopilo mtupu na siasa za kikatili )

Na Raia wao kila siku wanakamatwa Morogoro kwenye maroli wanakimbilia Africa Kusini.
 
Huko tunakoelekea unakosema kuna maendekeo makubwa ( kama tutafika ) tayari Ethiopia wako huko.

Wana Ethiopia Airlines, SGR ya kisasa na Bwawabla Umeme (Na wanajua biashara, wakati sisi ni utopilo mtupu na siasa za kikatili)

Na Raia wao kila siku wanakamatwa Morogoro kwenye maroli wanakimbilia Africa Kusini.
Pia wanafia kwenye hayo malori,kama kuku waliokumbwa na mdondo, lengo watoroke kwao.
 
Huko tunakoelekea unakosema kuna maendekeo makubwa ( kama tutafika ) tayari Ethiopia wako huko.

Wana Ethiopia Airlines, SGR ya kisasa na Bwawabla Umeme ( Na wanajua biashara, wakati sisi ni utopilo mtupu na siasa za kikatili )

Na Raia wao kila siku wanakamatwa Morogoro kwenye maroli wanakimbilia Africa Kusini.
Labda bado walivyofanya havitoshi. Wako Zaidi ya milioni 80 kama nakumbuka vizuri. Kwa Tanzania, vitu hivyo vikifanyika, vitabadili hasa Maisha ya Mtznia. Ila nakuunga mkono sana kuwa maendeleo bila ya uhuru ni sawa na ushuzi, hauendelei kunuka!
 
TUMIA AKILI YA KUZALIWA ACHA UZWAZWA HAKUNA MRADI WOWOTE UTAKAO KAMILIKA HAPO HAKUNA CHA (sgr) Hakuna cha (stigres) wala nini

NA TAKWIMU HIZO NI ZA KUPIKA

Dodoma tuliahidiwa kabla ya 2020.
1. Ujenzi wa uwanja wa michezo hola.
2. Ujenzi wa uwanja wa ndege msalato hola.
3. Ujenzi wa hospital kubwa ya Uhuru, anajenga kazahanati.
4. Ujenzi wa barabara ya pete HOLA.

Na bila misaada ya wafadhili tegemea umasikini uliotopea.

JIWE JONGO USIDANGANYIKE.
bilabila.
 
TUMIA AKILI YA KUZALIWA ACHA UZWAZWA HAKUNA MRADI WOWOTE UTAKAO KAMILIKA HAPO HAKUNA CHA (sgr) Hakuna cha (stigres) wala nini

NA TAKWIMU HIZO NI ZA KUPIKA.
Dodoma tuliahidiwa kabla ya 2020.
1. ujenzi wa uwanja wa michezo hola.
2. ujenzi wa uwanja wa ndege msalato hola.
3.Ujenzi wa hospital kubwa ya Uhuru....anajenga kazahanati.
4. ujenzi wa barabara ya pete HOLA.

na bilq misaada ya wafadhili tegemea umasikini uliotopea.

JIWE JONGO USIDANGANYIKE.
bilabila.
AKILI YANGU YA KUZALIWA YANIAMBIA ALISEMA ATAFANYA ELIMU BURE WAKATI RAIS ALIYEMTANGULIA ALISEMA JAMBO HILO HALIWEZEKANI....AKAFANYA. KAMA AKILI YAKO YA KUZALIWA YASEMA HILI HAKULIFANYA, ONGEZA MARADUFU HICHO UNACHOKIVUTA!
 
Kwani aliyewaambia kuwa ushoga ni hitaji letu la msingi ni nani?
Ni nani aliyewaambia kuwa hatuhitaji zahanati mpaka mkaanza kuzipinga?
Ni nani aliyeaambia kuwa barabara za uhakika siyo hitaji letu?
Ni nani aliyewaambia kuwa miradi ya maji siyo hitaji letu la msingi?
Mnataka tumkumbuke lissu, kwani katufanyia nini cha maana, kutaka kutufanya mashoga?
Tutamkumbuka yule aliyetujali na kujishughulisha na mahitaji yetu ya msingi. Nyie wengine wote mtapita tu!
 
Back
Top Bottom