Kwamba Mwenyekiti wa CCM Taifa amejipitisha kuwa mgombea urais kwa mlango wa uani/jikoni? Na Msajili kajikalia kimyaaa kama hamna kilichotokea

Kwamba Mwenyekiti wa CCM Taifa amejipitisha kuwa mgombea urais kwa mlango wa uani/jikoni? Na Msajili kajikalia kimyaaa kama hamna kilichotokea

mkuuwakaya

JF-Expert Member
Joined
Mar 18, 2013
Posts
1,195
Reaction score
1,626
Kama kichwa cha mada kinavyojieleza. Hali hii ndugu zangu haitapita hivi hivi, hata kama mgombea ambaye amepitishwa na JK atapita hapo Oktoba. Hali hii itaendelea kukitafuna chama chetu na kuleta mgawanyiko mkubwa.

USHAURI: Tufuate utaratibu wa watu kwenda kuchukua fomu, na kama tutakubaliana Mama aendelee hakuna shida. Ila utaratibu ufuatwe na sio janja janja ya kutumia mlango wa uani.

Hii vijana wanaita KUKABIA JUU. Yaani Mama na JK wake wamekabia juu kabisa aisee dhambi mjue.
 
FB_IMG_1748852351669.jpg
 
Hatari hiyo.Jaji senior anapokaa kwenye kigoda cha "Masalakulangwa" au "Mangungo" na hana aibu.Anyway,kule wanasema ugali mnono hapa wanaimba bia tamu.
 
Kama kichwa cha mada kinavyojieleza. Hali hii ndugu zangu haitapita hivi hivi, hata kama mgombea ambaye amepitishwa na JK atapita hapo Oktoba. Hali hii itaendelea kukitafuna chama chetu na kuleta mgawanyiko mkubwa.

USHAURI: Tufuate utaratibu wa watu kwenda kuchukua fomu, na kama tutakubaliana Mama aendelee hakuna shida. Ila utaratibu ufuatwe na sio janja janja ya kutumia mlango wa uani.

Hii vijana wanaita KUKABIA JUU. Yaani Mama na JK wake wamekabia juu kabisa aisee dhambi mjue.
Nacheka kama vile mazuri, Msajili ni takataka tu, sometimes nawaza heri kuwa kibaka kuliko kuwa msomi ambaye huwezi kusimamia unachokiamini
 
Nacheka kama vile mazuri, Msajili ni takataka tu, sometimes nawaza heri kuwa kibaka kuliko kuwa msomi ambaye huwezi kusimamia unachokiamini
Alipaswa kumshauri kama kweli nayeye ni muelewa

Nadhani Msajili ni mbumbumbu alipaswa kulisovu kabla sisi mambumbubu kusanuliwa na Slowslow

Aibu naona mimi
 
Kama kichwa cha mada kinavyojieleza. Hali hii ndugu zangu haitapita hivi hivi, hata kama mgombea ambaye amepitishwa na JK atapita hapo Oktoba. Hali hii itaendelea kukitafuna chama chetu na kuleta mgawanyiko mkubwa.

USHAURI: Tufuate utaratibu wa watu kwenda kuchukua fomu, na kama tutakubaliana Mama aendelee hakuna shida. Ila utaratibu ufuatwe na sio janja janja ya kutumia mlango wa uani.

Hii vijana wanaita KUKABIA JUU. Yaani Mama na JK wake wamekabia juu kabisa aisee dhambi mjue.
Sasa ndani kwao wakabie juu,kwa walalahoi wakabie juu,kwa wazalendo wakabie juu,kwenye chafuzi wakabie juu,hapa tunajenga taifa la namna gani?
 
Nacheka kama vile mazuri, Msajili ni takataka tu, sometimes nawaza heri kuwa kibaka kuliko kuwa msomi ambaye huwezi kusimamia unachokiamini
Na hiyo ndo tofauti yetu na wazungu waafrika usomi wao ni kwa ajili ya matumbo not else.
 
Ofisi ya msajiri wa vyama iliundwa na ccm kudhibiti vyama vipya.

Hao hao ccm wanaweza kuiondoa/ kuifuta hiyo ofisi.

Msajiri anateuliwa na mwenyekiti wa ccm ambaye ndiye rais.

Sasa jiulize nani mkubwa kwa mwenzie ni ccm au msajiri?

Bado unadhani msajiri anachakufanya juu ya ccm?

Msajiri ni kwa ajili ya vyama vyooote vya siasa lakini siyo ccm.
 
MKUKI KWA CHADEMA KWA CCM MCHUNGU!

Ukurasa wa Askofu Mwamakula unatoa fursa adimu ya watu kuona 'haramu' iliyofanywa na viongozi wakuu wa CCM wakati Rais mstaafu Jakaya Kikwete ambaye anakalia kiti muhimu cha 'Mzee wa Taifa' na 'Mlezi wa CCM' akiikalia kimya haramu hiyo. Fuatana na Martin, M. M ili ujionee uchambuzi wake unavyoianika CCM.
Je, nini kimekushangaza? Je, nini maoni yako?

Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!
Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula
Itunge, Dar es Salaam; 22 Julai 2025; saa 3:22 usiku

CCM NA MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA WANACHEKESHA.

Kuna jitihada zinazoendelea kufunika dosari kubwa za kikatiba, kikanuni, na kisiasa katika mchakato wa kumteua mgombea Urais CCM mwaka 2025. Mchakato huo ulikuwa na dosari za msingi na kimantiki‬.

‪Wachambuzi na wapambe wa DOLA wanatumia historia ya chama na “mshikamano wa wanachama” kama mbadala wa uhalali wa mchakato. Wanadogodesha hoja ya msingi ya uteuzi wa mgombea Urais CCM.‬

‪Lakini hoja ya Balozi Humphrey Polepole, inapaswa kutazamwa kama kumbusho la msingi la maadili, utaratibu, kanuni za CCM na misingi ya kikatiba ndani ya CCM, si vinginevyo. Asuchukuliwe kama muasi.‬

‪Katika fukuto hilo ka kuvunja Katiba ya CCM, tunapata nafasi ya kuona ‘double standards’ za utendaji na maamuzi ya ofisi ya msajili wa vyama vya siasa. Ofisi ya umma inayotakiwa kusimamia vyama vya siasa. ‬

‪Ingawa Katiba ya CCM ya mwaka 1977 (Toleo la 2022) ibara ya 39(1) inasema kuwa mgombea wa nafasi ya Rais hupendekezwa na Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) na kuidhinishwa na Mkutano Mkuu wa CCM Taifa.‬

‪Katiba hiyo ya CCM inaweka mchakato mzima wa uteuzi mgombea wa nafasi ya Rais unaoanzia ngazi za chini: kuanzia ngazi ya mikoa, ngazi ya Kamati Kuu (CC), hadi ngazi ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC).‬

‪Katika mchakato wa 2025, hatua hizo muhimu hazikufuatwa. Hakukuwa na kikao cha Kamati Kuu kilichopitisha jina, hakukuwa na mapendekezo kutoka mikoa, wala mashauriano ya wanachama. ‬

‪Mchakato uliruka hatua na kupelekwa ghafla Mkutano Mkuu. Huu ni ukiukwaji wa utaratibu, hata kama mwisho wa mchakato huo ulikuwa chombo halali. Uhalali wa chombo hauna maana ya uhalali wa mchakato.‬

‪Ni kweli kuwa katika historia ya CCM, Rais aliyepo madarakani mara nyingi anagombea muhula wa pili bila upinzani mkubwa. Hayo ni mazoea, si katiba. Mazoea hayawezi kuchukua nafasi ya katiba ya chama.‬

‪Ikiwa CCM inataka kuhalalisha “kupitisha Rais aliyepo” moja kwa moja, ibara ya katiba inayoruhusu ushindani ifutwe. Vinginevyo, kila hatua lazima iheshimiwe hata kama mgombea wa mwisho atakuwa mmoja tu.‬

‪Uamuzi wa kupitisha jina la mgombea nafasi ya Rais ulichukuliwa katika Mkutano Mkuu uliokuwa na ajenda moja: kujaza nafasi ya Makamu Mwenyekiti aliyekuwa amejiuzulu. Ikaingizwa hoja ya mgombea Urais‬

‪Hakuna tangazo la chama au taarifa ya maandalizi ya uteuzi wa mgombea nafasi ya Rais. Mchakato wa kutafuta mgombea Urais (hata wa jina moja) haukuzingatiwa. Hii ni kasoro ya wazi ya kikanuni.‬

‪Katika taasisi nyingine – iwe ni kampuni, taasisi ya kiraia au chama cha siasa – maamuzi makubwa hayawezi kuchukuliwa nje ya ajenda rasmi. Ajenda za kikao zinatumika kuongoza na kuendesha kikao.‬

‪Kukosekana kwa ajenda hii ni ushahidi wa kufanyika kwa mchakato wa kificho, jambo linalodhoofisha uwazi, ushirikishwaji na uwajibikaji wa chama kwa wanachama wake. Wanachama wa CCM hawakuheshimiwa. ‬

‪Hoja kuwa Humphrey Polepole alishiriki uteuzi wa 2020 wa John P. Magufuli, na sasa anahoji mchakato wa 2025, ni hoja yenye udhaifu mkubwa. Tofauti kubwa ipo katika mazingira na namna mchakato ulivyofanyika.‬

‪Mwaka 2020:‬ Majina yalitolewa kutoka mikoa;‬ Kamati Kuu ilikaa;‬ Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ilipitisha;‬ Mkutano Mkuu ulithibitisha kwa taratibu zote.‬

‪Mwaka 2025:‬ Hakuna mapendekezo ya mikoa;‬ Hakuna kikao cha CC kilichojadili jina;‬ Hakuna tangazo la uteuzi;‬ Ajenda ya Mkutano Mkuu haikuwa uteuzi wa mgombea.‬

‪Kwa hivyo, Polepole hakupinga mchakato wa mwaka 2020 kwa sababu ulikuwa HALALI. Leo anapinga kwa sababu mchakato ni BATILI. Hili ni jambo la kiadilifu, si uasi wa kisiasa kama ambavyo inawekwa sasa.‬

‪Kauli ya mchakato unaakisi “mshikamano wa chama” haina mashiko ya kikatiba. Mshikamano hautumiki kama kigezo cha kuruka mchakato, kupuuza ushauri wa wanachama na kuvunja misingi ya uwazi.‬

‪Chama cha siasa chenye mshikamano hakihitaji kukwepa mchakato wa uteuzi. Kinaamini kwamba kupitia ushindani au mchakato kamili, mgombea wake atapita kwa kishindo, kwa kuwa anakubalika.‬

‪Ukweli ni kuwa kilichotokea si mshikamano – ni ukimya wa hofu au wa mkakati ulio nje ya misingi ya demokrasia ya ndani ya chama. Ni woga wa (labda) kujitokeza wagombea wengine waliokuwa na nia hiyo.‬

‪CCM, kwa kupitisha jina moja bila mchakato shirikishi, CCM inatuma ujumbe kwamba: Wanachama wa CCM hawana tena nafasi ya kushiriki uamuzi mkubwa kama wa kuchagua kwa ushindani mgombea Urais.

‪CCM, kwa kupitisha jina moja bila mchakato shirikishi, CCM inatuma ujumbe wa hatari kwamba: Katiba ya chama ni nyaraka ya mapambo tu, si mwongozo hai wa chama chao; Ushindani wa ndani ni kosa, si fursa.‬

‪Huu ni msiba wa kisiasa kwa chama kikongwe cha siasa kama CCM, ambacho ndicho kilianzisha mfumo wa vyama vingi – sasa kinakuwa mfano wa kuvunja ushindani wa kidemokrasia ndani kimyakimya.‬

Kwamba, kama CCM wameshindwa kuheshimu na kufuata utaratibu, mwongozo, kanuni na katiba ya CCM, wataweza kuheshimu na kufuata kanuni na sheria za uchaguzi na katiba katika uchaguzi mkuu?

‪Katika hali ya kushangaza, Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa haijatoa tamko lolote kuhusu ukiukwaji wa wazi wa katiba na mchakato wa CCM. Kwamba Msajili wa Vyama vya Siasa hayupo nchini? Yupo likizo?‬

‪Hii ni tofauti na jinsi ambavyo ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa inavyokuwa na haraka, kiherehere na msimamo mkali jambo linapohusu vyama vya upinzani ambavyo ni tishio kwa CCM kama CHADEMA.‬

‪Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi amewahi kutaka CHADEMA watoe maelezo ya kina kwa nini waliwafukuza na kuwavua uanachama wanachama 19 ambao walikuwa wabunge wa viti maalumu.‬

‪Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa imewahi kutengua uteuzi wa wajumbe wanne wa Sekretarieti ya CHADEMA na kamati kuu ya CHADEMA waliothibitishwa na Baraza Kuu la CHADEMA ambalo liliketi Januari 22, 2025. ‬

‪Msajili wa Vyama vya Siasa akatoa maelekezo kwa CHADEMA kuitisha Baraza Kuu Jipya lenye akidi stahiki, ili kufanikisha uteuzi wa viongozi kwa mujibu wa Katiba ya CHADEMA na Sheria ya Vyama vya Siasa. ‬

‪Msajili wa vyama vya Siasa amewahi mara kadhaa kuingilia mijadala ya ndani ya kikatiba ya CHADEMA. Msajili amewahi kuingilia migogoro ya kisiasa ndani ya Civic United Front (CUF) na NCCR - MAGEUZI.‬

‪Msajili wa vyama vya Siasa alisema uamuzi wa Kikao cha Halmashauri ya NCCR -Mageuzi wa kumsimamisha mwenyekiti James Mbatia na Sekretarieti uote kutojihusisha na siasa ndani ya NCCR ni halali.‬

‪Uamuzi ambao ulibatilishwa na Mahakama Kuu ya Tanzania baada ya kufuta maamuzi ya kumfuta uanachama na kumuondoa James Mbatia nafasi ya uenyekiti ikisema maamuzi yalikuwa BATILI.‬

‪Ofisi ya Msajili wa Vyama vya siasa ilimuandikia barua Katibu Mkuu (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad kufuatia mvutano wa kusimamishwa uanachama aliyekuwa Mwenyekiti wa CUF, Prof. Ibrahim Lipumba.‬

‪Ofisi ya msajili iakutaka uongozi wa CUF kueleza kwa kina hatua ilizopitia hadi kufikia uamuzi huo kwa mujibu wa katiba ya CUF, na iwasilishe barua hiyo kufikia September 02, 2016 majira ya saa 9:30 alasiri.‬

‪Lakini kwa CCM, ambapo uteuzi wa mgombea wa kiti cha Rais umeruka hatua zote za msingi, Msajili amekuwa kimya kama hakuna kitu kilichotokea. Msajili amekula ‘kotapini’ na kujifanya kipofu na kiziwi.‬

‪Ukimya kutoka katika ofisi inayotakiwa kusimamia Vyama vya Siasa unatoa taswira ya upendeleo wa wazi, na kudhoofisha uhalali wa ofisi ya Msajili kama msimamizi wa haki na usawa wa vyama vya siasa. ‬

‪Msajili wa Vyama vya siasa anapaswa kutoa tamko kwa CCM kuvunja Katiba na Kanuni za chama kama kweli analinda Katiba ya nchi na sheria ya vyama vya siasa, si CCM pekee. Lasivyo anaonekana MCHEKESHAJI.‬

‪Maneno ya Humphrey Polepole si uasi wa chama chake. Ni kauli ya kuikumbusha CCM kuheshimu misingi ya katiba, demokrasia. Kukataa kusema ukweli katika makosa ya wazi ni kushiriki kuua misingi ya chama.‬

‪Chama cha siasa chenye nguvu si kile kinachokandamiza mijadala, bali kinachoweka hoja mezani na kuzitatua kikatiba. Hoja za wanachama zijibiwe na siyo kutumia DOLA kuzijibu.

‪CCM si tu imevunja utaratibu wa uteuzi wagombea wake, bali imefungua mlango wa hatari wa kutengeneza uongozi usio na ridhaa ya ndani ya chama. Hapo sasa ndipo ilipojikita hoja ya Humphrey Polepole. ‬

‪Msajili wa Vyama vya Siasa, kwa kukaa kimya hata baada ya hoja ya msingi ya kutofuata taratibu ndani ya CCM kuwasilishwa anahatarisha uhalali wa ofisi yake na kuchochea uhalisia wa upendeleo wa kisiasa..‬

‪MWISHO; Wananchi wanaopenda mustakabali bora wa kisiasa, watambue kwamba; kukosoa si usaliti – ni ishara ya dhamira safi ya kujenga taasisi yenye msingi imara wa demokrasia, sheria na uongozi wa haki.‬

Martin M. M.; 22 Julai 2025.
 
Nacheka kama vile mazuri, Msajili ni takataka tu, sometimes nawaza heri kuwa kibaka kuliko kuwa msomi ambaye huwezi kusimamia unachokiamini
Msomi wa Tanzania ana tofauti sana na Darasa la saba ndo maana Msukuma uwa wanawatukana Wasomi Bungeni Wanatoa Kama wasomi wenyewe wameshidwa kutunga na kusimamia Sheri Wanatofauti gani na darasa la saba hii yote Siasa na katiba Mwanasiasa hatakiwi kua juu Msomi hata siku Moja
 
Msajili, DPP, IGP, Jaji Mkuu, Mwenyekiti wa Tume Uchaguzi na Mkurugenzi wake pamoja na Makamishina wote ni wateule wa Rais ambaye ndiye Amri Jeshi Mkuu, Mwenyekiti wa CCM Taifa na ndiye Mgombea wa Urais..

Sasa ndugu hivi kuna uchaguzi hapo kweli hata kama umeishia la kwanza B kule Kidogozero kata ya Dutumi.
 
Back
Top Bottom